R.B
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 6,296
- 2,573
[h=2] [/h] Debora Sanja, Dodoma
SERIKALI ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOSO), imeanza uchunguzi ili kuwabaini wanafunzi wa chuo hicho, ambao wanajihusisha na biashara ya ngono. Viongozi hao wamefikia hatua hiyo kufuatia taarifa iliyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari wiki iliyopita kuwa, baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho wanajiuza.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Rais wa UDOSO, Yunge Paul alisema, tayari kazi hiyo imeanza na watakaobainika watachukuliwa hatua za kinidhamu.
Alisema wanafunzi hao, wanashusha heshima ya chuo hicho kikubwa na kama taasisi ambayo imebeba wasomi wengi.
Alisema taarifa ya kashfa ya ngono, iliyoripotiwa na vyombo vya habari imesononesha nchi nzima ikiwemo uongozi wa chuo, wazazi na wanafunzi.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari kwa kweli, imesononesha nchi nzima ikiwemo UDOM yenyewe, wanafunzi wakiwemo wanafunzi wakina dada, alisema.
Alisema taarifa hiyo, haikutoa uzito na ushahidi wa kutosha kuwa wanafunzi wa chuo hicho wanajiuza na wamekuwa wakionekana sehemu mbalimbali za starehe mjini Dodoma.
Tunaomba vyombo vya habari, vilivyotoa taarifa hiyo warekebishe, ili kurudisha heshima na imani kwa Chuo Kikuu cha Dodoma, alisema Yunge.
Alisema wakati taarifa hiyo, inatolewa katika vyombo vya habari mji wa Dodoma ulikuwa na watu wengi na kuwa inawezekana walioonekana kufanya vitendo hivyo sio wanafunzi wa chuo hicho.
Mwanafunzi wa UDOM, anajulikana kwa kitambulisho chake na inawezekana mtu yeyote akajitambulisha anatoka katika chuo hiki kama ushahidi wa wanafunzi upo tuletewe, alisema.