UDOM yagoma kushinikiza wenzao kuachiwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UDOM yagoma kushinikiza wenzao kuachiwa

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by kilimasera, Dec 22, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MGOGORO katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), umeibuka upya baada ya wanafunzi wa Kitivo cha Sayansi ya Jamii kugoma kuingia madarasani jana kwa lengo la kuushinikiza uongozi wa chuo kutoa agizo la kuwaachia huru wanachuo wanaoshikiliwa na polisi.

  Mgomo huo ulianza jana baada ya baadhi ya wanafunzi wa kitivo hicho kukamatwa na polisi huku ikidaiwa kuwa wapo wanafunzi walioumizwa kutokana na vurugu zilizotokea kati ya wanafunzi na Polisi juzi.

  Akizungumzia suala hilo, Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Idrisa Kikula alisema wanafunzi wamegoma kuingia darasani huku wakidai hawawezi kuingia mpaka hapo uongozi wa chuo utakapowahakikishia kwamba waliokamatwa na polisi wameachiwa huru.

  Profesa Kikula alisema pamoja na wanachuo kuandamana na kufanya mgomo kudai fedha hizo, ni wazi chuo kilishakaa na kuweka mikakati ya kuwawezesha wanafunzi wafanye masomo yao kwa vitendo.

  Alisema kikao cha kwanza kilikaa Agosti mwaka huu, kujadiliana jinsi ya kupanga bajeti ya serikali kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), kuwawezesha kupata fedha kwa lengo la kufanya masomo yao kwa vitendo.

  “Sikiliza, kwanza katika masomo hayo ya vitendo, wanafunzi wanatakiwa kuwa na walimu wao hivyo ni lazima kuwepo na pesa kwa ajili ya wanafunzi na walimu wao… tena suala hili lina utaratibu wake, siyo suala la kukurupuka tu.

  Kunahitajika utulivu na mipango ya kueleweka,” alisema Profesa Kikula. Hata hivyo, Profesa Kikula alitilia shaka mgomo huo kwa madai inawezekana umechangiwa na baadhi ya walimu, hivyo kuundwa kwa tume ya watu watano inayotakiwa kutoa majibu ndani ya siku saba.

  Alidai kuwa iwapo watabainika watumishi wa chuo hicho kwa maana ya walimu, kuwa chanzo cha mgomo na migogoro, watachukuliwa hatua za kinidhamu haraka iwezekanavyo na wengine wanaweza kuachishwa kazi kwa mujibu wa taratibu na kanuni za kazi.

  Jana, chuo kilikuwa katika ulinzi mkali ambapo kila kona kulionekana kuzingirwa na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) huku kila askari akiwa na bunduki ya kurusha mabomu.

  Wanafunzi 11 wanaodaiwa walijeruhiwa na Polisi wakati wa vurugu za juzi za kutaka kuandamana kwenda kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kudai fedha za masomo kwa vitendo, waliruhusiwa kutoka hospitalini baada ya hali zao za kiafya kuendelea vizuri.

  Kutokana na vurugu hizo, mawaziri walilazimika kufika chuoni hapo wakiwa na viongozi wote wa Mkoa wa Dodoma pamoja na maofisa usalama na kuwataka waandishi wa habari kutoweka katika eneo la chuo kwa madai kuwa wana kikao cha ndani, japo hawakuwa tayari kuzungumzia kikao hicho.

  Viongozi waliofika chuoni hapo japo ilionekana kama siri ya chuo ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha, wakiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. James Msekela, Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Elizabeth Masanga na Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Betty Mkwasa anayekaimu nafasi ya Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini.
   
 2. Click_and_go

  Click_and_go JF-Expert Member

  #2
  Dec 22, 2010
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 451
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ....I wonder whats the problem with Tanzania??? Serikali imezoea kuwa mpaka watu wagome ndo watupe haki zetu!!!
   
 3. Gobegobe

  Gobegobe JF-Expert Member

  #3
  Dec 22, 2010
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 245
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nawaonea huruma sana, nasubiri tusikie tamko jingine la wasomi hao.
   
 4. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #4
  Dec 22, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hizo vurugu zimesababishwa na FFU. Kimsingi wanafunzi hawakua na lengo la kufanya vurugu. Tatizo uongozi wa chuo bado wana mawazo ya kukifanya chuo cha dodoma kisiwe na migomo wakati kuna matatizo chungu nzima. Lengo lao ni kujiosha kwa JK ndio maana wakisikia harufu ya mgomo wanaleta FFU kuuzima na kuwakamata wanafunzi na kuwaweka ndani na kuwapa vitisho kibao na wengine hata kusafirishwa hadi majumbani kwao. Huu ni ukandamizaji wa demokrasia. Madai ya wanafunzi ni ya msingi. Inawezekana vipi mwanafunzi anahitimu elimu ya juu bila kufanya mafunzo kwa vitendo!!? Wakati hata mwalimu wa shule ya msingi wanafanya mafunzo kwa vitendo.?? Hakuna sababu ya kuendelea kuwashikilia wanafunzi hao wakati wanadai mambo ya msingi.
   
 5. r

  roby m Member

  #5
  Dec 22, 2010
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 28
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 3
  Jamani serikali wasikilizeni basi hao wanafunzi kwasababu mgomo wao una mantiki!!!
   
 6. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #6
  Dec 22, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  mie nashangaa utakuta wanapuigwa na FFU wanamwagiwa washawasha na bado wanaifagilia CCM sijui hata wamelogwa na nani hawa wanachuo cha muhimu ni kuibwaga CCM kwasababu tabu zote hz zimeletwa na CCM na hakuna asiyejua kama project na practical ni muhimu sana kwa mwanafunzi wa chuo kwasababu akishamaliza ni moja kwa moja anaenda kuanza kazi!
   
 7. A

  Aldoff Member

  #7
  Dec 22, 2010
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  JifuNzeni kwa wenzenu UDSM, Sio kushabikia tu CCM na kujikomba , Madhara yakumchangia JK hela ndio hayo sasa......!Wenzenu ukitaja CCM tu chuoni kama ulikuwa mgombea katika serikali ya DARUSO hupati kula! Think big UDOM....!:hungry:
   
 8. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #8
  Dec 22, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  TAMKO LA VIJANA WASOMI WA VYUO VIKUU WA MKOA WA DODOMA, KUHUSU KITENDO CHA BAADHI YA WABUNGE WA CHADEMA KUTOKA NJE YA UKUMBI WA BUNGE.

  NDUGU WAANDISHI WA HABARI,
  NDUGU WANANCHI,.


  Awali ya yote nawashukuru sana kuhitikia wito wetu wa gfafla kuja kujumika pamoja nasi leo hii, akhsanteni sana.

  Sisi vijana wasomi wa vyuo vikuu mbalimbali vilivyoko mkoa wa Dodoma kwa pamoja tunapenda kuweka wazi maoni yetu juu ya kitendo kilichofanywa na Wabunge wa CHADEMA jana 18.11.2010 wakati Mhe. Rais alihutubia Bunge.


  Kwanza tumeshtushwa na kitendo hicho na kuweka wazi masikitiko yetu kwa kuwa kilichofanyika ni kinyume na matarajio ya wapiga kura waliowachagua waheshimiwa wabunge hao kuwawakilisha ndani ya chombo hicho kikubwa na chenye heshima kubwa ndani na nje ya nchi.


  Bunge ni sehemu ya kuwakilisha wananchi kwa hoja chini ya kanuni zilizopo bila kujali itikadi ya chama chochote cha siasa na kazi kubwa ya mbunge ni kuishauri na kuisimamia Serikali kwa niaba ya wananchi waliomchagua au kuwachagua.


  Kwa mantiki hiyo basi kama Wabunge hawamtambui Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania maana yake hawana kazi ya kufanya ndani ya Bunge kwani kazi yao kubwa ni kuishauri na kuisimania Serikali sasa kama hawaitambui Serikali hiyo hawana sababu ya kuendelea kuwepo Bungeni.


  Pili Baada ya uchaguzi wa Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda, wabunge hao pia walinukuliwa na vyombo vya habari na ushaidi tunao wakiweka wazi kumkubali kiongozi huyo, na kauli mbiu yake ya ‘Bunge moja’ je, kitendo walichofanya inaashiria utekelezaji wa kauli mbiu ya Bunge moja?


  Tatu msimamo wa kutomtambua Rais ni wa CHADEMA kama chama na waliotoka nje ya Bunge ni wabunge sasa ni vema wabune hao watambue na kutafakari upya kama kweli wanawawakilisha Bungeni wananchi au cha na kutekeleza misimamo yao bila kujali maslahi ya waliowachagua na kumpa kura nyingi Rais Kikwete?.


  Nne Kwa badhi ya wabunge wa CHADEMA kutomtambua Rais wakati akilihutubia bunge ni wazi kuwa hata sheria zitakzopitishwa na Bunge hawatahusika kwa kuwa mwenye mamlaka ya mwisho kukubali sheria iliyotungwa na Bunge itumike ni Rais ambaye wanadai hawamtutambui.


  Ni dhahiri kuwa watashindwa kufanya kazi yao ya uwakilishi na usimamizi wa Serikali Bungeni .


  Je wanawaonesha watanzania dalili gani kama si kutaka kuleta machafuko nchini na mgawanyiko ndani ya Bunge na kwa Jamii kwa ujumla?.


  Wananchi waliowachagua wabunge hao wanapaswa kutafakari upya wawakilishi waliowachagua kama wana uelewa wa kutosha kuhusu bunge, sisi vijana wa vyuo vikuu tunajua na tunatambua kuwa Rais ni Sehemu ya Bunge na Bunge haliwezi kukamilika bila Rais na hii ndio maana kila sheria inayopitishwa na Bunge ni lazima yeye Rais aweke sahihi yake.


  Katika mazungumo yake na waandishi wa habari wiki hii Mweneykiti wa CHADEMA MHE. Freeman Mbowe, alinukuliwa na vyombo vya habari akisema wabunge wake na madiwani wanaweza kuendelea kuwakilisha wananchi licha ya kutomtambua Rais.


  Sisi tunasema hili si sahihi bali ni upotoshaji mkubwa, kamwe mtoto hawezi kudai kuwa hamtabui Baba yake kisha anaendelea kumwita Baba na kutumia kila kitu kinachotolewa na Baba huyo huyo. Huo ni utovu wa nidhamu au kukosa maadili.


  Sisi vijana wa vyuo vikuu Mkoa wa Dodoma tunawaomba Watanzania wote wenye nia njema na Taifa letu kuwapuuza wabunge wa CHADEMA na kutambua kuwa lengo lao ni kutaka kutuhamisha kutoka kwenye ajenda ya msingi ya Maendeleo na kubaki kwenye malumbano ya kisiasa kama tulivyoshuhudia katika nchi jirani.


  Kamwe tusikubali kudanganywa na watu wachache.


  Mwisho tungependa kuwaomba Wabunge wa CHADEMA wawaombe radhi watanzania kwa kuvuruga tashwira safi ya Bunge letu lisilo na ubaguzi na itikadi za kisiasa vinginevyo wanawadharau watanzania waliowachagua wakidhani kwamba niwaadilifu wa Taifa na si cha chama chao.


  Tutambue kuwa kazi kubwa ya CHADEMA na Wabunge wake kwa sasa ni kuwachanganya watanzania ili badala ya kuendelea na shughuli za ujenzi wa taifa wabaki na malumbano ya hapa na pale kwa manufaa yao binafsi.


  Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Bunge letu na kutuepusha na ubaguzi kama huu uliofanywa na baadhi ya Wabunge wa CHADEMA.


  Aksanteni sana.


  IMESOMWA NA THOBIAS MWESIGA RICHARD

  KWA NIABA YA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU MKOA WA DODOMA
   
 9. G

  Godwine JF-Expert Member

  #9
  Dec 22, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  ni mkasa wa kisiasa na uchambuzi unawakuta wanachuo wa UDOM kwanza ni wachanga wa mambo, pili ni watu wasioweza kujieleza na ni vijana wanaofata mkumbo.kitendo cha vijana hawa kujigeuza tawi la chama kimewashusha heshima na pia kutumia pesa nyingi kumnunulia mttu fomu ya urais na kutoa manoti ya kampeni kilitafsiriwa na bodi ya mikopo kwamba ni watoto wa matajiri na hayo ni matokeo yao
   
 10. njoro

  njoro Senior Member

  #10
  Dec 22, 2010
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 178
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  we unadhani kila mwana UDOM ni ccm,.vlaza wa
  ccm ni wachache na wako kila taasisi ya uma nchi,.wao huwa wanajidai kuwa wanawakilisha mawazo ya watu kumbe wanachukiwa na kla m2
   
Loading...