UDOM yadaiwa Tshs 240m kwa kuwafukuza wanafunzi kinyume na sheria

Apr 4, 2012
6
3
leo nilikutana na rafiki yangu anaefanya kazi utawala wa Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM), akanidokeza kuwa kuna wanafunzi 24 walifukuzwa kwa sababu walikutwa wapo kwenye gari wamevaa sare za Chadema wanakwenda kwenye mkutano wa CHADEMA. wakaenda mahakamani, ikaamuru warudi. kwa kuwa Chuo kilikiuka taratibu.

Sasa nasikia wamefungua kesi, na kila mmoja anataka alipwe Tsh milioni kumi 10,000,000/=. Taarifa za ndani zinadai Uongozi wa chuo ulimtuma Afisa Sheria wa chuo akawaombe wafute kesi. Kwa kuwa Chuo kitaaibika.

MAONI YANGU. vijana wasithubutu kwenda kufuta kesi, waendelee nayo. na vyombo vya habari tunataka vitujulishe juu ya hili sakata ili iwe mwanzo na mwisho wa uonevu. Na tumeongea na viongozi wa walimu, walimu waliofukuzwa wala wasiwe na wasiwasi wakirudi pia wadai fidia kila mmoja hata ya milioni 100. ili iwe fundisho kwa uongozi huu mbovu. Na serikali ijifunze. Dawa ya moto ni moto. wao walishawaharibia maisha.

Hili liwe fundisho. hakuna aliye juu ya sheria. Kama raisi anafumbia macho, vyombo vingine vitafanya kazi.:shock:
 
leo bungeni waliongea serikali imekufa hakuna hata mtu anayejali watumishi wanapesa kuliko hata serikali yenyewe. Watu ni wezi sana wanaiiba kila sehemu. Huo uongozi wa UDOM wanatumika nao
 
Jaman, naamin kuna waandishi wa habari humu ndani wa vyombo mbalimbali! Hili suala la uongozi wa UDOM mbona hamlifuatilii na kuliweka hadharani'?? Naamin moja ya kazi kubwa ya vyombo vya habari ni kupinga uonevu kwa kubainisha yanayotendeka sehemu husika! Nawasihi fanyeni uchunguzi na kuripoti kwa raia!
 
Very good! lakini hawa wanafunzi wamekosea,ingetakiwa kila mmoja adai sh 100,000,000 (milioni mia moja@1) ili iwe fundisho. Nawashauri na wale wa UDSM,MUCCOB'S na MUHIMBILI wafuate nyayo. "Haki haiombwi, haki inadaiwa kwa nguvu"
 
Hao washkaji nao mbona wamedai pesa ndogo hvo,ilitakiwa wadai hata mil 500 kila mmoja.
 
Mbona haueleweki eleweki na chanzo chako cha habari mara unadai umesimuliwa na rafiki yako, af baadae unadai umesikia...Mwisho wa siku zitakuwa story za mitaani hiyo kesi ka ingefunguliwa tungesikia kwenye media, na hata kama wamefungua sidhani kama wanaweza kushinda, na mwisho wa siku ndo watazidi kujipoteza.
 
YEah! i Wish kila aliefutwa kwa makosa akadai milioni zake manake hiki chuo kinaendeshwa kama kituo cha daladala.
wanafunzi wake ni kama watumwa tu kwa sasa maana hata haki zao wanaogopa kudai kisa watafukuzwa. Valafu mbona matokeo hawatoi hawa pimbi? au wanaona aibu kwa jinsi walivyofelisha watoto wa wenzao? nacikia yohana mchafu kakamata sap 900 kwenye media na anajisifia!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom