Kiherehere
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 1,806
- 622
Kuna waandishi wengine wanapaswa kuwa na akili, yawezekana hata kazi yake ni ya kuchomekwa tu!! Huwezi kusema UDOM ndo wamesema haya kwa kupitia kapuuzi kamoja kalikokuwa na Ridhwani kwenye kuomba udhamini wa baba yake eti ni UDOM.
UDOM ina uongozi, so kama kiongozi wa chuo kasema ilikuwa inasound safi lakini Mwanafunzi aliyekutwa analewa ndo anawakilisha UDOM?
Vyuo vingine!!! yaani hapa hili gazete haliwezi kufunguliwa mashitaka na CHUO? au chuo (uongozi na msemaji wa chuo) wanaipenda hii??
SOMA HAPA CHINI ni habari ya nipashe trh 21/11
UDOM yaitaka Chadema kuomba radhi
Na Sharon Sauwa
21st November 2010
B-pepe
Chapa
Maoni
Baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani Dodoma, wamewataka wabunge wa Chama cha Maendeleo na Demokrasia (Chadema), kufikiria upya msimamo wao wa kutomtambua Rais Jakaya Kikwete, ili kulinda maslahi ya wapigakura wao.
Kauli hiyo ilitolewa na wanafunzi wa vyuo vikuu mjini hapa jana wakati wakizungumza na waandishi wa habari kuhusiana wabunge hao kususia hotuba ya Rais.
Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake wa vyuo vya Mipango, St. John, CBE, Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Thobias Richard, alidai kuwa lengo la wabunge hao ni kutaka kuhamisha wananchi katika ajenda ya msingi ya maendeleo na kubaki kwenye malumbano ya kisiasa.
Richard ambaye ni mwanafunzi wa UDOM, alisema kitendo hicho ni kinyume na matarajio ya wapiga kura waliowachagua wabunge hao.
Kama hawamtambui Rais maana yake hawana kazi ya kufanya ndani ya Bunge kwani kazi yao kubwa ni kuishauri na kuisimamia serikali sasa kama hawatambui serikali hiyo hawana sababu ya kuendelea kuwepo bungeni, alisema.
Aliwataka wabunge hao kutafakari upya kama kweli wanataka kuwawakilisha bungeni wananchi.
Aliwataka wawaombe radhi Watanzania kwa kuvuruga taswira safi ya Bunge lisilo na ubaguzi na itikadi za kisiasa. Alisema kwa kutowaomba radhi wananchi ni kuwadharau Watanzania waliowachagua wakidhani kwamba ni waadilifu kwa taifa na sio chama chao.
Wabunge wa Chadema, walitoka nje ya ukumbi wa Bunge, Ijumaa wiki iliyopita, lengo likiwa ni kuonyesha kuwa hawamtambui Rais Kikwete