Udom chumvi zamwagwa milangoni na kwenye corridor jengo kuu la utawala..........

bushman

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,411
743
Jengo kuu la utawala udom wafanyakazi wake wamekumbwa na hali ya sintofahamu toka juzi baada ya chumvi ya kuwekwa kwenye mboga kumwagwa milangoni na kwenye macorridor huku kukiwekwa alama ya msalaba,kitendo hicho kimeaacha minong'ono ya chini kwa chini yakuwa inawezekana ni ushirikina au watu wanajiimarisha kimadaraka,chumvi ya kuweka kwenye mboga imefuta nini kwenye milango na makorridor ya ofisi? Inazua maswali mengi sana
1.je udom kama tasisi ya umma inaongozwa na proffessionalism au ushirikina?
2.nini hatma ya udom kwa siku zijazo?
3.chumvi ya mboga inauhusiano gani na utendaji kazi wa kila siku?

Tujadili
 
Pengine hata huyo/hao walioweka hiyo chumvi hakukusudia kufanya ushirikina bali kueneza hofu ili aliyemshirikina aanze kusumbuka. Fikiria asubuhi mbele ya mlango wako wa nyumbani au ofisini, mtu kwa kutaka kukujaribu tu, ameweka kinyago cha binadamu kimevikwa kitambaa (sanda) cheupe? Ikiwa wewe ni mshirikina utaanza kuhaha na kupoteza mali ili kujikinga kujitibu.
 
Mamamia hilo nalo neno!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
chumvi husaidia kuua sisimizi na pia chumvi hutumika katika kutegulia mazindiko.............karibu ukikuwa utajua
 
walinzi wapo pale na chumvi inamwagwa mchana kweupe,ila anayemwaga hajulikani,au mabomu/zindiko yalikuwa yanateguliwa,duu CHUO KIKUU NA USHIRIKINA TENA?NINACHOJUA MIMI MAZINDIKO HUFANYIKA KWENYE KITU BINAFSI LAKINI TASISI YA UMMA UNAZINDIKA ILI WAKUPOKEE WANAO KUONGOZA?
 
wanayataka wenyewe ngoja wauane.. solution ni ndogo na rahisi sana . wanunue kamera(cctv) waziweka wanakuwa wamemaliza kila kitu. tatizo wanaendekeza pombe na wizi,,ngoja walogane
 
Back
Top Bottom