Pundamilia07
JF-Expert Member
- Oct 29, 2007
- 1,439
- 54
Udokozi unawaponza Wabongo kupata ajira
Na Ramadhan Mbwaduke
20th July 2009
Serikali imesema tatizo la uaminifu kwa vijana walio wengi nchini linachangia kwa kiasi kikubwa tatizo la ajira nchini kwani huwafanya baadhi ya wenye makampuni kulazimika kuja nchini na watu wao walio na moyo safi na kuwaajiri.
Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya, amesema hivi sasa, kuna matukio mengi ya aibu yahusianayo na wizi wa pesa, mali na vifaa vya makampuni, ambayo hujikuta yakiingia hasara kubwa.
Kwa sababu hiyo, Waziri Kapuya akasema wahusika wanaoendesha kampuni hizo hulazimika kuajiri watu wa kwao ili kushika nafasi ambazo Watanzania wangeweza kuzitumikia kwa uwezo sawa au hata zaidi ya wageni wanaowaleta.
"Inafikia mahala hata kijisimu tu (cha mkononi) kinaposahauliwa kidogo tu, kinakwapuliwa... Kwa kweli hili ni tatizo ambalo limeanza kuwa kubwa na linasikitisha sana," akasema Waziri Kapuya, huku akitaja sekta mojawapo inayokumbwa zaidi na tatizo hilo kuwa ni ya huduma za hoteli.
Akitolea mfano zaidi, Waziri Kapuya ameema hata Wachina wanaoendelea na ujenzi katika Chuo Kikuu cha Dodoma wamekuwa wakikumbana na matatizo ya kuibiwa mali zao na vifaa vya ujenzi kila kukicha, hali ambayo inawafanya walalamike kila mara kutokana na hasara wanayoipata.
"Nenda pale UDOM (Chuo Kikuu cha Dodoma)... Wachina wanaibiwa stoo kila siku. Je, Mchina Mjenzi akisema anataka meneja anayesimamia vifaa awe Mchina mwenzie kwa sababu waliopo sasa wanamuibia sana, halafu we ukiwa Waziri utasemaje? Ni tatizo kubwa kwa kweli," akasema Waziri Kapuya.
Aidha ameongeza kuwa hivi sasa, Wizara yake imewasiliana na Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi nchini, VETA ili iweze kuongeza somo la uaminifu katika mtaala wake ili walau kupunguza tatizo hilo ambalo linaleta athari kubwa katika sekta ya ajira.
"Nashukuru kwamba baada ya kuzungumza na VETA, hivi sasa suala hilo limekubaliwa na litawekwa katika mitaala yao ili kuondokana na tatizo hili la uaminifu," akasema Waziri Kapuya.