Udogo wa kizazi ni sababu ya ugumba

OCC Doctors

Senior Member
Jul 20, 2018
104
151
Mji wa uzazi hufahamika kama (Uterus), wakati mwingine msichana huzaliwa na uterasi ambayo ni ndogo sana kuliko kawaida, hali hii hujulikana kama ''hypoplastic uterus'' au ''Uterine Hypoplasia''. Dalili zake ni msichana kushindwa kuanza kuziona siku zake za hedhi, maumivu ya tumbo, kuwa na tundu dogo la uke na baadae kutokuweza kubeba ujauzito (infertility).

Sababu kubwa huwa ni shida ya kuzaliwa nayo (congenital disorder) ambapo mji wa uzazi hushindwa kuendelea kukua kikamilifu. Muda mwingine hushabihiana na hali ya kutokuwepo kwa uke na mji wa uzazi, hali hii hufahamika kama (Meya-Rokitansky-Küster-Hauser (MRKH).

normal-size-of-the-uterus.png
 
Back
Top Bottom