Luteni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 2,274
- 301
Mwenyekiti wa CCT, Askofu Peter Kitula amesema tatizo la udini lilianza mwaka 1986 na hakuna kiongozi wa serikali aliyejitokeza kulikemea badala yake Chama Cha Mapinduzi (CCM) ilizidi kufanya makosa kwa kuingiza suala hilo katika Ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2005.
"Kuanzia miaka ya 1986 kulianza kujitokeza mihadhara ya kidini na kidhehebu katika jamii ambayo hatukuwa tumeizoea lakini jambo hili halikukemewa wala kuchukuliwa hatua za kisheria".
Ilani ya uchaguzi ya CCM 2005 ilitamka bayana kuwa suala la Mahakama ya Kadhi litashughulikiwa na kupatiwa ufumbuzi, ikumbukwe kuwa mahakama ya kadhi ni jambo la kidini na kiibada katika dini ya kisilamu, jambo hili ni kinyume cha Katiba ya nchi na sheria ya vyama vya siasa hakuna aliyeona hatari yake na kwamba litakuwa chanzo cha udini ndani ya siasa za Tanzania, "alisema.
Kwa maneno ya Kitula umefika wakati sasa tuache unafiki tuanze kuwataja kwa majina yao wote wanaohusika kulipeleka taifa kusiko bila kumng'unya maneno, kwa kuanzia nitaanza na Mwenyekiti wa NEC anakotupeleka siko. Ni ukweli mchungu.