Udini, Ukanda, dhuluma na Ufisadi wa CHADEMA ni upi jamani?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Udini, Ukanda, dhuluma na Ufisadi wa CHADEMA ni upi jamani??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyami2010, May 17, 2011.

 1. Nyami2010

  Nyami2010 JF-Expert Member

  #1
  May 17, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wapendwa wana JF, nimesikia mara nyinyi CHADEMA wakihusishwa na Udini, Ukanda, Dhuluma na sasa Ufisadi. Inaniumiza sana, maana nina imani sana na CDM, lakini kama hizo hoja ni za kweli……....mmmmm.
  Jana nilikuwa na mkongwe wa siasa na mwanazuoni maarufu sana hapa Tanzania, katika zungumza yake alisema na ninamnukuu “CHADEMA is a gang of criminals, am just deeply sorry for Dr. Slaa, Zitto Kabwe and my great comrade Prof. Baregu……You know, CDM is not a political party rather…..a group of frustrated and desparate individuals under the umbrella of politics….”. Ukweli niliumia sana kimoyomoyo na nikaamua kutoka mahala pale. Kwa hiyo nimeona ni vema nijaribu kujua zaidi juu ya CDM.
  Kwa yeyote mwenye takwimu au ufahamu naomba anisaidie kujua yafuatayo:
  1. Uwiano wa waislamu kwa wakristo miongoni mwa wabunge wa CDM
  2. Uwiano wa waislamu kwa wakristo miongoni mwa wajumbe wa Halmashauri Kuu na Sekretariat ya CDM
  3. Kati ya wabunge wote wa CDM ni wabunge wangapi wa CDM wanatoka Kanda ya Kaskazini hususani mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara+ na Singida?
  4. Je ni kweli Mh. Mbowe kawauzia CDM magari 3 yaliyotumika kwa TSh 480,000,000?
  5. Kama ni kweli, ni magari mangapi, aina gani (kama ni Fuso truck, je ni 4ton au 10ton) na ya mwaka gani?
  6. CHADEMA ati wamewadhulumu watu wengi waliojitoa kupiga kampeni kwa matarajiyo ya kurudishiwa japo kidogo walichotumia, hii ni kweli? Mfano ni yule M/kiti wa CDM aliyekimbilia CCM majuzi...na wengine wengi wanalalamika....
   
Loading...