Udini ni ugonjwa!

Anfaal

JF-Expert Member
Jan 19, 2010
1,154
113
Hivi karibuni kumeibuka malumbano makubwa saana ambayo yanalenga kuigawa jamii yetu. Malumbano hayo kwa kiasi kikubwa saana yamechangiwa na wasomi na wanasiasa hasa wakati na baada ya uchaguzi mkuu.
Wapo wanasiasa kutoka vyma mbalimbali wamenukuliwa kulizungumza hili na wengine pia wamejaribu kulimekea. Kiuhalisia kadri miaka inavyozidi kwenda jambo hili ndiyo linazungumzwa zaidi. Jambo hili limekuwa wakati wa Tawala za marais woote kuanzia mwl Nyerere mpaka sasa hivi kwa Kikwete. Uwepo wa tatizo hili umesababisha hata kujadili issues zinazolenga Taifa letu kuwe hatarini. Leo hii, wengi wakitaka kujadili issues wataangalia nani anajadiliwa kwa dini yake kabla hata ya kuwaza hoja inayozungumzwa. AU ukifanyika uteuzi wowote serikalini, watu wataanza kuangalia dini ya aliyeteuliwa kabla hata ya kuangalia uwezo na vigezo vya Mtanzania.
Zipo hoja mbalimbali zimekuwa zikitolewa ili kupunguza makali ya mijadala hii. Mf; MODS wamekuwa wakichukua hatua ya kutoa thread au post zinazozungumzia udini, huko nje ya JF wanasiasa wamekuwa wakilizungumza hili na mengineyo. Binafsi naamini uadilifu na ukweli kwanza ndiyo inaweza kuwa misingi ya maendeleo kwa Taifa letu.
Kwa kutambua kuwa mijadala ya kidini imekuwa ikizuiliwa hapa JF, naamini kijiwe hiki na cha watu waelevu licha ya ukweli kwamba tatizo hili lipo zaidi JF kuliko mitaani.
Tujadili basi kwa nini hali hii imekuwa kwa kasi kiasi hiki? Tujadili namna ya kuweza kuendesha mijadala kwa Tija bila dharau kwa makundi mengine. Na ninaomba tuamue kwamba sasa kukashifiana inatosha na kama itabidi kuzungumza basi facts ziwekwe mbele kuliko hisia. Tusiogope kujadili ili tuzuiwe hii mbegu tunayoipanda isiote mitaani.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom