Udini ni state of mind. Tatizo Tanzania tumekuwa kwenye state of denial!

Bayana

JF-Expert Member
Sep 25, 2012
433
69
Mh Zitto leo amesema mengi ya msingi katika live interview lakini ila moja ya mambo ambayo yamenigusa ni msimamo wake juu ya udini na ushauri wake kwa viongozi wa TZ kwa ujumla.

Hili ndilo swali aliloulizwa:

''Ikiwa ndani ya uwezo wako i.e tuchukulie umepata urais; ni njia gani ambayo unaweza kutumia kufuta na kumaliza Udini ambao unaanza kujidhihirisha kwenye siasa za Tanzania?''

Udini ni state of mind. Tatizo Tanzania tumekuwa kwenye state of denial.

Malalamiko ya Udini katika nchi yameanza siku nyingi sana. Njia ni moja tu, Serikali kutoshughulika na masuala ya Dini na viongozi wa dini kutojiingiza kwenye siasa za vyama bila kupoka uhuru wao wa mawazo au wa kujiunga na vyama vya siasa. Ukiwa na Serikali inayotenda haki kwa watu wote bila kujali wana Sali au wanaSwali hapatakuwa na malalamiko haya.

Hii sio mara ya kwanza tunaona vurugu za kidini kwenye nchi. Kwani mmesahau suala la maduka ya nguruwe miaka ya tisini? Mmesahau suala la mwembechai la miaka hiyo hiyo? Mmesahau mauaji ya Arumeru? Muhimu ni Serikali kuwa imara kuhakikisha tunapiga vita ‘chuki' kisheria na kutenda haki kwa watu wote bila kujali dini zao. Udini ulivyo sasa ni kansa inayotutafuna kidogo kidogo. Nimeshuhudia mwenyewe udini mkali sana wakati wa kampeni mwaka jana Jimboni kwangu ulioendeshwa na dini zote kuu - Waislam na Wakristo kila mmoja kwa mwono wake.

Nimesoma jana makala ya MwanaKijiji kuhusu namna ya kushughulika na suala hili. Kuna haja ya kuzungumza kwa uwazi bila jazba suala hili. Ningekuwa ni Rais leo ningeunda Tume ya Ukweli na Maridhiano kujadili kwa uwazi na mapana yake suala la Udini. Tusipochukua hatua nchi hii itapasuka vipande. Haya mambo ya Gesi na Mafuta haya ndio yatatumika na maadui wa nchi yetu kutugawa.

Tuwe Makini sana. Tusione tu hizi vurugu kwa juu juu. Tuzungumze

Naamini Prof Lipumba anaweza kushirikiana na viongozi kama hawa (Zitto) kufanikisha ile ajenda ambayo aliianzisha hivi karibuni.
Binafsi namuunga mkono zitto katika hili.

LET US SAVE TANZANIANS FROM MASSACRE!

Chanzo ni kwenye LIVE INTERVIEW ya JF - Mahojiano ya moja kwa moja na Mhe. Zitto Zuberi Kabwe katika JamiiForums
 
Mawazo chanya kabisa kwa mustakabali wa hatima ya taifa hili. Viva Zitto.
 
zitto sio mkweli. anatwambia tz kuna udini maaskofu wangapi wamewekwa ndani? labda atambie CCM ithamini maisha ya waislam kama wanavyofanya kwa wakiristo
 
wacha nipite kwa sababu siwaelewi vizuri. Kwani ni nchi gani hakuna udini kwa maana ya watu wa dini fulani kujaliana wao.Nenda india Wahindu wanajiona bora kuliko waislamu na wakristo, Malasyia ni hivyo pia.

Indonesia waislamu wako juu ya wakristo. Ila nakataa kuwapo kwa udini kwa maana ya watu fulani wanabaguliwa kwa dini yao tanzania haupo. Ukitaka kujua hilo fuatilia viongozi wa nchi na chama tawala kuanzia kamati kuu na viongozi wa taasisi za chama chao. Propaganda za kwamba kuna udini si sahihi.
 
zitto sio mkweli. anatwambia tz kuna udini maaskofu wangapi wamewekwa ndani? labda atambie CCM ithamini maisha ya waislam kama wanavyofanya kwa wakiristo

Mchango wako unathibitisha uwepo wa udini, ndio maana mjadala huenda ukatufikisha pahala pa kushika na kupata suluhu.
 
Suala hili hili haliwezi kuisha mpaka tutiane adbu kwanza , kwa vile viongozi wetu wanafiki sana, leo wanasema tuzibe majeraha ya udini yaliyotokana na uchaguzi mkuu, kesho hao hao utakuta wanaendeleza siasa hizo hizo za udini,
 
Sumu haijaribiwi kwa kuionja.
 
zitto sio mkweli. anatwambia tz kuna udini maaskofu wangapi wamewekwa ndani? labda atambie CCM ithamini maisha ya waislam kama wanavyofanya kwa wakiristo

Wewe unawatafutia watu ban za bure hapa jukwaani. Hivi ni lini wakristo wameandama na kuchoma misikiti au kuvamia mali za watu?
 
Mara ya kwanza Zitto kusema Tanzania kuna udini ilikuwa 2010 mara baada ya uchaguzi mkuu kuisha. Timing ya kauli hiyo didn't go down well na baadhi ya watu kwa sababu ilikuwa kama pre-emptive strategy!
 
Mimi sio mshabiki wake ila jokes aside, huyu jamaa anaonekane anaongea vitu vya maana. Hata kama hatumpendi wengine lakini, kuna vitu taifa hili litamkumbuka kwavyo. Ana kipaji katika hii medani ya kisiasa, anakitumiaje, that is another question.
 
Wewe unawatafutia watu ban za bure hapa jukwaani. Hivi ni lini wakristo wameandama na kuchoma misikiti au kuvamia mali za watu?

tatizo la watu kama hao ni kua mpaka sasa hivi hawaoni kosa walilofanya...its amazing baadhi ya akili za watanzania zilivyo
 
zitto sio mkweli. anatwambia tz kuna udini maaskofu wangapi wamewekwa ndani? labda atambie CCM ithamini maisha ya waislam kama wanavyofanya kwa wakiristo

Maaskofu na hasa wa Kanisa Katoliki wao hawana muda wa kulumbana ila wanaumia namna ya kuwasaidia watanzania wote kwenye afya , Elimu , maisha ya kiroho,nk , hawaendi kuvunja bar na kuiba bia za watu kwa jina la Muungano kumbe ni fitina za kidini .Kuna udini na unaletwa na watu wenye njaa kali wasio na kipato wala elimu wanadhani vita na vurugu itawapa future .Udini unaenezwa na CCM zaidi na KAFU
 
Wadini Bana Utawajua tu. Yaani katika Mahojiano yooote wewe "Umeamua kuliona hilo la Udini" Tena umeamua kuliweka katika Context ambayo Wewe Ulikuwa Unatamani Zitto azungumze. Acheni Mambo ya Kijinga Bana Zitto amezungumza Mambo mengi sana ya Msingi na Mahojiano yake hayawezi kuwa Summarized na Hicho cha Habari

Acheni Udini Bana
 
Bayana, Lunyungu,

..kuna baadhi ya watu UDINI ndiyo ajira yao.

..UDINI ndiyo unaowaweka mjini, na kuwapatia mlo.

..nadhani hilo ni tatizo kuliko "udini" wenyewe.
 
Huwa napata taabu sana kudeal na watu kama wewe ambao wana 'attack' personality badala ya content. Mwanzoni mwa thread nimekiri kuna mengi na ya muhimu ambayo Zitto amezungumza, ila hii ni moja kati ya hot issues. So ulitaka ni copy interview nzima na kuiweka humu? Au kuna kitu unaficha mbacho unahisi kikijadliwa utaumbuka. Unaficha nini hadi unakataa majadiliano?
 
Bayana, Lunyungu,

..kuna baadhi ya watu UDINI ndiyo ajira yao.

..UDINI ndiyo unaowaweka mjini, na kuwapatia mlo.

..nadhani hilo ni tatizo kuliko "udini" wenyewe.

Nafikiri huu ni wakati muafaka. Tukigundua kama upo baada ya kujadiliana, tunaweza kuamua kitu na kukiingiza kwenye katiba mpya 'anti udini law' na adhabu yake, ili kulichinjia mbali hili dudu 'UDINI'
 
Nimesoma mahojiano yote kati ya zito na jamii forum.lazima nikiri kuwa nimeboresha msimamo wangu juu yake.kuna mambo nilikuwa namhisi vibaya bure.kuanzia sasa sitamhisi hivyo tena na nitaomba anisamehe kwa hilo.

Lakini nina jambo ambalo nimeliona kwake ambalo si nzuri sana.inaonekana hawezi kusema wazi juu ya udhaifu wa kikwete. Hili si jema.

Vilevile, ninahisi anaposema kuwa uwajibikaji ni kila kitu ni kama vile amaanisha utawala bora (good governance) ambayo ni dhana pana na uwajibikaji ni kipengele kimoja tu kati ya vingi vinavyofanya (katika umoja wake) maisha katika nchi yawe bora.
 
Ni kweli udini unaitafuna nchi taratibu, Vinara wa udini ni chama kilichopo madarakani. Kimeulea na kuutumia udini kujikita madarakani.

Kumbuka suala la Shule ya Shauritanga ilipochomwa moto. Wanafunzi 40 wakateketea. Alli Mwinyi akalifutika kibindoni. Lika la Mabucha ya nguruwe nk nk. Serikali ina nafasi ya kuliangalia hili nakutolifanya credit ya kuwa-win wapiga kura waislam wakati wa chaguzi.

Zitto kasema kweli, dawa ni mhadhara wa kitaifa ili kila mtu aseme dukuduku lake.
 
Back
Top Bottom