Mh Zitto leo amesema mengi ya msingi katika live interview lakini ila moja ya mambo ambayo yamenigusa ni msimamo wake juu ya udini na ushauri wake kwa viongozi wa TZ kwa ujumla.
Hili ndilo swali aliloulizwa:
''Ikiwa ndani ya uwezo wako i.e tuchukulie umepata urais; ni njia gani ambayo unaweza kutumia kufuta na kumaliza Udini ambao unaanza kujidhihirisha kwenye siasa za Tanzania?''
Naamini Prof Lipumba anaweza kushirikiana na viongozi kama hawa (Zitto) kufanikisha ile ajenda ambayo aliianzisha hivi karibuni.
Binafsi namuunga mkono zitto katika hili.
LET US SAVE TANZANIANS FROM MASSACRE!
Chanzo ni kwenye LIVE INTERVIEW ya JF - Mahojiano ya moja kwa moja na Mhe. Zitto Zuberi Kabwe katika JamiiForums

Udini ni state of mind. Tatizo Tanzania tumekuwa kwenye state of denial.
Malalamiko ya Udini katika nchi yameanza siku nyingi sana. Njia ni moja tu, Serikali kutoshughulika na masuala ya Dini na viongozi wa dini kutojiingiza kwenye siasa za vyama bila kupoka uhuru wao wa mawazo au wa kujiunga na vyama vya siasa. Ukiwa na Serikali inayotenda haki kwa watu wote bila kujali wana Sali au wanaSwali hapatakuwa na malalamiko haya.
Hii sio mara ya kwanza tunaona vurugu za kidini kwenye nchi. Kwani mmesahau suala la maduka ya nguruwe miaka ya tisini? Mmesahau suala la mwembechai la miaka hiyo hiyo? Mmesahau mauaji ya Arumeru? Muhimu ni Serikali kuwa imara kuhakikisha tunapiga vita ‘chuki' kisheria na kutenda haki kwa watu wote bila kujali dini zao. Udini ulivyo sasa ni kansa inayotutafuna kidogo kidogo. Nimeshuhudia mwenyewe udini mkali sana wakati wa kampeni mwaka jana Jimboni kwangu ulioendeshwa na dini zote kuu - Waislam na Wakristo kila mmoja kwa mwono wake.
Nimesoma jana makala ya MwanaKijiji kuhusu namna ya kushughulika na suala hili. Kuna haja ya kuzungumza kwa uwazi bila jazba suala hili. Ningekuwa ni Rais leo ningeunda Tume ya Ukweli na Maridhiano kujadili kwa uwazi na mapana yake suala la Udini. Tusipochukua hatua nchi hii itapasuka vipande. Haya mambo ya Gesi na Mafuta haya ndio yatatumika na maadui wa nchi yetu kutugawa.
Tuwe Makini sana. Tusione tu hizi vurugu kwa juu juu. Tuzungumze