Udini ni state of mind. Tatizo Tanzania tumekuwa kwenye state of denial!

Nafikiri huu ni wakati muafaka. Tukigundua kama upo baada ya kujadiliana, tunaweza kuamua kitu na kukiingiza kwenye katiba mpya 'anti udini law' na adhabu yake, ili kulichinjia mbali hili dudu 'UDINI'

Mkuu Wewe ni Mdini tena Inawezekana ndio wale ambao hawatakiwi CCM

"UAMSHO Bye Bye" Nnape Nnauye
 
zitto sio mkweli. anatwambia tz kuna udini maaskofu wangapi wamewekwa ndani? labda atambie CCM ithamini maisha ya waislam kama wanavyofanya kwa wakiristo

Kwa hiyo unataka kuwe na usawa hata katika kuwekwa ndani kati ya Wakristo na Waislamu hata kama Maaskofu hawajafanya kosa?
 
Naamini Prof Lipumba anaweza kushirikiana na viongozi kama hawa (Zitto) kufanikisha ile ajenda ambayo aliianzisha hivi karibuni.
Binafsi namuunga mkono zitto katika hili.

LET US SAVE TANZANIANS FROM MASSACRE!

Umezunguuuuka Mwisho wako umeonesha your true Identity
 
Mkuu Wewe ni Mdini tena Inawezekana ndio wale ambao hawatakiwi CCM

"UAMSHO Bye Bye" Nnape Nnauye

I respect your opinion kama huo ndio mwisho wa upeo wa mchango wako! Wewe unatakiwa na nape. Nenda CCM!
 
I respect your opinion kama huo ndio mwisho wa upeo wa mchango wako! Wewe unatakiwa na nape. Nenda CCM!

Yaani Katika yooote umemegua la Udini halafu Ukalibold Kidini. Tanzania Kuna Magaidi Wachache tu ambao Serikali ya Dr. Shein ina deal nao Vizuri huku Bara Kova akila nao sahani Moja. Acha kuendekeza Ugaidi Bana
 
Amezungumza yaliyo moyoni mwake.
Moto wa chadema hata wangeazisha chama cha namna gani wasingeweza chochote, kwa sababu hata viongozi siyo wa kukodi kutoka nje, bali wanaotoka ndani ya ccm
 
Sura halisi ya ujumbe wa Zitto Kabwe uko katika maneno haya hapa chini:

"Ukiwa na Serikali inayotenda haki kwa watu wote bila kujali wana Sali au wanaSwali hapatakuwa na malalamiko haya."

Haya maneno yana tofauti gani na kaulimbiu ya CUF (ambao ni vibaraka wa UAMSHO) yaani HAKI SAWA KWA WOTE? Au Zitto atufafanulie juu ya hili maana "birds of the same feather fly together!"
 
I doubt the motives of his answer. Kumbuka premise ya swali "...ikiwa wewe ni Rais...." that tells a lot more than what spilled
 
zitto sio mkweli. anatwambia tz kuna udini maaskofu wangapi wamewekwa ndani? labda atambie CCM ithamini maisha ya waislam kama wanavyofanya kwa wakiristo

Maaskofu wawekwe ndani kwa lipi? Ni lini walivunja misikiti, ni lini waliandamana, ni lini walipora viwanja vya wengine? Ndani si mahali pa kila mtu bali ni kwa ajili ya wahalifu katika jamii.
 
Kwa kutamka hilo angalau zitto anafaa kuwa rais wa awamu ijayo

Zitto ni Mwislam, zamu ya Waislam kukaa ikulu inaisha 2015 hivyo kwa awamu ijayo hafai kuwa rais. Waislam wajipange kwa awamu ya 6 mwaka 2025. Sina shaka rais ajaye hatakuwa Mwislam bila kujali chama chake.
 
Umezunguuuuka Mwisho wako umeonesha your true Identity

What is my true identity according to you? Mimi sioni ni kipi unapinga! Unapinga kwamba Zitto hakusema niliyoyapaste hapo, unapinga hakuna udini nchini? Naona unalalamika tuuuu, true colour, hiyo ya uongo iko wapi? Jadili hoja kwa maoni yako sio kujadili mtu boss, ebo.
 
Zitto ni Mwislam, zamu ya Waislam kukaa ikulu inaisha 2015 hivyo kwa awamu ijayo hafai kuwa rais. Waislam wajipange kwa awamu ya 6 mwaka 2025. Sina shaka rais ajaye hatakuwa Mwislam bila kujali chama chake.

Hii ni sera ya chama gani mkuu?
 
Zitto anazungumzia "usawa" kama suluhisho la udini! Ukweli ni kwamba Waislamu malalamiko yao huwa hayaishi, wakibandua ganda moja la kitunguu hutaka kubandua na jingine hadi kitunguu chote kiishe!
Zitto atoe mfano ni Waislamu wa nchi ipi ambao pamoja na wingi wao wamekaa raha mustarehe bila malalamiko! Mbaya sana malalamiko yao hata kama hayawahusu Wakristo (km Muungano) hubambikiziwa Wakristo!
 
Sura halisi ya ujumbe wa Zitto Kabwe uko katika maneno haya hapa chini:

"Ukiwa na Serikali inayotenda haki kwa watu wote bila kujali wana Sali au wanaSwali hapatakuwa na malalamiko haya."

Haya maneno yana tofauti gani na kaulimbiu ya CUF (ambao ni vibaraka wa UAMSHO) yaani HAKI SAWA KWA WOTE? Au Zitto atufafanulie juu ya hili maana "birds of the same feather fly together!"

Kama unamawazo kulingana na jina lako, nafikiri hii itakusaidia. Nimegoogle hiyo kauli mbiu hapo kutafuta maana yake hasa ni nini: The Civic United Front (CUF – Chama cha Wananchi) « Haki Sawa kwa Wote Sioni kama kuna tatizo kwenye kauli mbiu au wanao isupport. Labda kama unamaanisha kitu kingine.
 
Bayana, Lunyungu,

..kuna baadhi ya watu UDINI ndiyo ajira yao.

..UDINI ndiyo unaowaweka mjini, na kuwapatia mlo.

..nadhani hilo ni tatizo kuliko "udini" wenyewe.

mkuu kama hiyo inaukweli ni hatari zaidi. Tuwaombee wapate kazi halali ya kufanya kuliko upuuzi huu.!
 
Hii issue ipo ila ukiangalia mitaani tunavyoishi huwezi kugundua maana kuna kitu kimejificha nacho si kingine bali ni mgawanyo wa madaraka baina ya hizi dini though kwa sie Mabudha hatuna shida (hapa ni uroho wa madaraka kwa misingi ya dini tu kwani mbona katika maisha ya kwaida mitaani kwetu hii issue ni ngumu kui-verify kama kweli kuna una udini)
 
Back
Top Bottom