Udini ni mtaji wa mafisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Udini ni mtaji wa mafisadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mamajack, Jun 18, 2012.

 1. m

  mamajack JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Habari zenu wana jamvi,naomba nieleze ambacho nimekuwa nikikifanyia kazi kwa ukaribu zaidi na kupata maoni ya wadau mbalimbali.suala hili la udini limekuwa likiongelewa na kuonesha dalili zote za kutugawa watanzani kwa misingi ya ukristo na uislamu.huu ni mpango kabambe wa mafisadi ambao wanatumia nguvu na pesa nyingi kuhakikisha wanalipandikiza suala hili katika akiri za watanzani.wanajaribu kututumia ili waendelee kufaidika na mipaango yao ya kuiibia nchi.kabla ya kisa cha udini,walitumia neno 'amani' kila mara watu walipotaka kuhoji masula mhimu ya nchi yao,au kuandamana kuhusu mambo machafu ya ufisadi,walionekana kama wanataka kuvunja amani,hivyo jeshi la polisi liliwadhibiti vikali,hata viongozi wetu wa kitaifa walisimama na kukemea waziwazi kwa kudai ni uvunjifu wa amani.kauli hii kwa sasa hainanguvu tena.wamekuja na hili la kutangaza udini ili watu wagawanyike na kushindwa kufanya maamuzi sahihi juu ya mstakabali wa taifa hili.tunaoumia ni sisi wakristo,waislamu na wale wasio na dini.wakati huo wao na familia zao wako salama wanakula bata(kama vijana wasemavyo),suala hili ni hatari sana kwetu hata kwa vuzazi vijavyo,hivyo basi,watanzania wenzangu tuwapuuze na mpango wao ambao hauna maslahi kwetu zaidi ya kutuharibia umoja wetu.

  MUNGU IBARIKI TANZANIA.
   
 2. Comi

  Comi JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 3,347
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  Sikubaliana na wewe ila ujinga wa viongozi wa kidini ndiyo chanzo kwani huruhusiwi kuchanganya dini na siasa, angalia uamsho je fisadi gani aliyetia mkono?angalia misri,syria,lebanon n.k je ni ufisadi ndiyo chanzo cha vurugu? Tabu ni kuchanganya dini na siasa
   
 3. m

  mamajack JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  uamsho wanamkono wao,ndiyo maana wanjeuri kiasi kile.
   
 4. Comi

  Comi JF-Expert Member

  #4
  Jun 18, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 3,347
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  ni kweli ndiyo maana nikamwambia mtoa mada udini si ufisadi isipokuwa wao wanachanganya dini na siasa kutokana na kutokuwa na upeo
   
 5. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145

  Lakini UDINI sasa hivi linaongelewa kwa mantiki ya Muungano kati ya

  Tanganyika na Zanzibar na Halijaikabili Tanganyika kiasi hicho cha

  kutugawa mpaka Mafisadi wafaidike; Sasa hivi Mafisadi wanakula mali bila

  Udini na Wanatunzwa na Chama Tawala na ni bila tatizo la UDINI.

  Kwanini Unatuazishia haya Matatizo ya UDINI kuwa ndio kasoro ya UFISADI

  BARA? WEWE NDIO NADHANI UNATAKA KUTAPAKAZA UDINI HADI BARA; ZANZIBAR

  WANATUMIA DINI TU ILI KUJINASUA NA MUUNGANO NA SIO

  KUWAFURAHISHA MAFISADI... JAMANI TUACHE HIZO FIKIRA NI MBAYA...
   
 6. m

  mamajack JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  nngu007,dhumuni halikuwa muungano,maana hili suala halikuanzia zanziba,ila imprimantation strategies zimeenda nje ya matarajio yao,ndiyo maana kimeanza kilipuka zanziba.cha msingi hapa ni kwa wale wenzetu ambao wanpenda kusikia na kunakili,hili sio la kufanyia mzaha,kwa nguvu moja na tiliteketeze kabisa.
   
 7. M

  Masabaja Senior Member

  #7
  Jun 18, 2012
  Joined: Mar 4, 2012
  Messages: 139
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Namuunga mkono mtoa hoja, ni hivi hawa jamaa wanajua wananchi wana maisha magumu. Hivyo njia pekee ni kuwagawa kwa misingi ya udini ili wasiwe na lugha moja kuwakemea juu ya uovu wao. Na wanajua fika kama wananchi wakisimama kwa pamoja ufisadi utakuwa hauna nafasi hivyo njia pekee ni kuwachanganya kwa kucheza na imani maana wanajua imani ni kitu sensitive ambacho mtu akisikia atamchukia wa imani nyingine na wao watakuwa wamefanikiwa mpango wao maana wanajua hamwezi kuwa wamoja kuuliza maendeleo ila mtakuwa busy kusotana vidole huku wakiwa wanakula kwa kwenda mbele.
   
Loading...