Udini na rasimu mpya ya katiba

Profesa

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
905
624
SURA YA NNE
HAKI ZA BINADAMU, WAJIBU WA RAIA NA MAMLAKA ZA NCHI SEHEMU YA KWANZA
HAKI ZA BINADAMU
....
"(5) Ni marufuku kwa mtu, kikundi au taasisi ya dini kutumia uhuru
wa kutangaza dini kwa kukashifu imani na dini nyingine, kujenga chuki au
kuchochea vurugu na ghasia kwa madai ya kutetea imani au dini.
(6) Dini na imani ya dini haitatumika kwa namna yoyote
itakayowagawa wananchi, kuleta uhasama au kuharibu amani miongoni
mwa wananchi.
(7) Neno “dini” kama lilivyotumika katika Ibara hii litatafsiriwa
kwamba maana yake ni pamoja na madhehebu ya dini, na maneno
mengine yanayofanana au kuambatana na neno hilo nayo yatatafsiriwa
kwa maana hiyo."
 
Maana ya kukashifu ndipo lilipo tatizo.

Hapo ndipo patakua patashika.

Hiki Kipengele kisipoangaliwa kitazua kizaa zaa sana

Yapo Mambo Mengi maovu yaliyofanywa na mojawapo ya waanzilishi wa dini fulani,ambayo hayakubaliki kijamii, Hayakubaliki kiutu, Hayakubaliki na Mungu wa Kweli na Hayakubaliki na Hata wapagani...Lakini cha ajabu ni kwamba kipengele hiki cha katiba kitawalazimisha wapenda maendeleo na ukweli wasiyakemee kwa kuhofia kukashifu watu waliokataa kutumia ubongo wao waliopewa na mungu kufikiri....
 
Back
Top Bottom