Udin na ukabila kuisambaratisha jamii ya wa tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Udin na ukabila kuisambaratisha jamii ya wa tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fungu la kukosa, Feb 4, 2011.

 1. F

  Fungu la kukosa Member

  #1
  Feb 4, 2011
  Joined: Jun 16, 2009
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu wana JF, mimi sipo hapo nyumbani kwa karibu miaka kumi sasa, na matukio mengi yamefanyika bila ya mimi mwenyewe kuyashuhudia. Hatahivyo, hivi karibuni nimekuwa nafuatilia malumbano ya Masheikh wa Bakwata chini ya uongozi wa sheikh Ali Baswalehe na Viongozi wa Kanisa kule mkoani Arusha. Kwakweli chanzo cha malumbano yao haswa mimi sikijui, lakini matamshi yao yanaashiria kuibuka kwa ufa mkubwa sana utakao wagawa wa Tanzania kwa misingi ya udini na ukabila.Kibaya zaidi, na hata sisi wana JF, tumezusha mtindo wa kutukanana na kukashifiana wenyewe kwa wenyewe ndani ya blgo hii kwa misingi ya udini badala ya kushauriana mambo mema yenye kujenga mshikamano na upendo miongoni mwetu kama wana jamii.Kwamfano, pale mtu anaposema ati waislaam hawajasoma, au ni ma-terrorisists hao,nk,hii ni ishara ya kugawanyika kwa wana JF na wa tanzania kwa ujumla.Hivi mtu hawezi kutoa maoni yake bila matusi akawa ni mwenye kueleweka? Ninayo mengi ya kusema lakini kwa leo ni vizuri nijifunze kwanza toka kwenu wana JF tatizo kati ya waislaam na wakristo hapo Bongo ni nini? Mungu iepushe Tanzania isije ikawa Nigeria ya pili?
   
 2. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #2
  Feb 4, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,365
  Likes Received: 6,997
  Trophy Points: 280
  Watanzania Hwana Udini kabisa, Udini huko Midomoni mwa Viongozi waliofirisika sera kichwani ,Viongozi wa dini wasio na upeo,pamoja na Waandishi uchwara wa HAbari
  Mimi nilikuwa Uswazi kabisa lakini unakuta Wakristo na Waislamu wanashirikiana kwenye MIsiba, HArusi na matatizo mengine bila kubaguana kabisa

  Huwezi kuniambia kura alizopata Mnyika pale ubungo kapigiwa na Wakristo pekeyake au kra alizopata Lipumba zilikuwa ni za Waislamu Pekeyao, kweli kama serikali haitachukua hatua udni utaingia kwa kasi kubwa kwani watu mara nyingi wanafuata kauli za viongozi,
   
 3. Raia Mwema

  Raia Mwema JF-Expert Member

  #3
  Feb 4, 2011
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  viongozi wengi wa dini wanatumika kisiasa si wito wao kwa Mungu, wengi wana njaa ya kurubuniwa
   
 4. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #4
  Feb 4, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Your in different world! Statistics don't back your arguments.
   
 5. T

  Topical JF-Expert Member

  #5
  Feb 4, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Statistics is not the only measure of reality! be informed
   
 6. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #6
  Feb 4, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Tatizo ni kikwete na ccm yao baada ya kuona hawakubariki tena na jamii wakaona
  kheri waingize udini bai
   
 7. P

  Paul J Senior Member

  #7
  Feb 4, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kimsingi udini ni propoganda inayoenezwa na ccm pamoja na viongozi wake kupitia kwa baadhi ya viongozi wetu wa dini bila kujali madhara yake kwa taifa la watanzania siku za usoni. Wapo waumini wanaoelewa kabisa kuwa hizi ni propoganda kama ilivyo ada ya ccm lakini wapo wasioelewa kabisa na kuamini kuwa kuna udini. Kushindwa uongozi kwa ccm kimetafsiriwa na utawala wa ccm kuwa kunasababishwa na Chadema ambayo wanadai ina backup ya kundi fulani la dini. Huu ni upuuzi mtupu na ufilisi wa fikira na kushindwa kabisa kuongoza. Mifano iko dhahiri kabisa ukiangalia Misri, Tunisia na sasa yemeni wote ni dini moja na nchi hizi zinaongozwa kwa misingi ya kidini lakini kwa sababu ya kutowajibika kwa viongozi wa serikali kwa raia wao tunashuhudia ni jinsi gani watu wameingia mtaani kuupinga uongozi. Kwetu TZ raia wakilalamika maisha magumu, serikali hawajibiki mnasema udini, je misri, tunisia na yemen wasemeje? Viongozi wetu mafisadi wasitumie udini kulinda udhaifu wa uongozi wao, tanzania ni mija na kila mtu bila kujali imani yake ya dini anaumia na ugumu wa maisha ulivyo sasa!
   
 8. d

  dos santos JF-Expert Member

  #8
  Feb 4, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 240
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  udini upo chadema imesapotiwa sana na viongozi wa kikristo,na makanisani maelekezo yametolewa kuiunga mkono. Wanaosema udini haupo wao ndo wadini
   
 9. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #9
  Feb 5, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mkuu habari za huko ulipo.
  Udini upo Tanzania tena kwa kasi ya ajabu.
  cha kusikitisha ni kwamba wakristo wanataka kula keki ya taifa peke yao. uchaguzi uliopita viongozi wao waliwaelekeza waumini wao watu wakuwachagua. ilifikia mpaka kata wengine kushirisha ibada zao siku ya J2 ili wapate muda wakutosha kumpigia kura mtu wao. ukitaka kujua zaidi angalia kilichotokea kule sumbawanga, mwanza na mbeya. angalia ule mkutano wa mei 2010 wa jukwa la wakristo (soma hapo chini manane ya Rev. Mtikila halafu angalia na sehemu ya azimio la viongozi wa kanisa).
  mwisho wakae wasahau kutawala hii nchi peke yako otherwise patakuwa hapakaliki. Trust me.
  Maaskofu 'wagombea' waraka wa Mtikila
  MAASKOFU waliohudhuria mkutano wa siku moja wa Jukwaa la Wakristo, juzi walifanya kazi ya ziada kupata nakala ya waraka ulioandaliwa na mwenyekiti wa Chama cha Kidemokrasia (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, ambaye alitumia mkutano huoo kuusambaza.

  Mkutano huo ulikuwa wa kuzindua chombo hicho kikubwa cha mshikamano baina ya Wakristo, lakini Mchungaji Mtikila, ambaye anaongoza kanisa la Full Salvation, aliutumia kugawa takriban nakala 60.
  Alikuwa akigawa waraka ambao ulisababisha polisi kuvamia nyumba yake iliyo Mikocheni na kufanya upekuzi kabla ya kuondoka na mwanasiasa huyo ambaye pia ni kiongozi wa kiroho na kwenda kumuhoji kituo cha polisi kwa saa kadhaa zaidi ya mwezi mmoja uliopita.

  Waraka huo wenye kurasa 24 ambao Mwananchi ina nakala yake, unazungumzia harakati za kuwaamsha waumini wa dini ya Kikristo kuamka kutetea dini yao dhidi ya utawala wa sasa ambao mchungaji huyo anautuhumu kuwa unawabagua.

  Waraka huo pia unawataja watu mbalimbali, kuanzia Rais Kikwete, viongozi wengine wa kisiasa na watu maarufu ukiwahusisha na tuhuma mbalimbali kubwa.
  Maaskofu kadhaa walionekana kumfuata Mtikila ili kupata nakala ya waraka huo ambao mchungaji huyo alikuwa amebeba nakala zake kwenye mkoba wa mkononi.

  “Nilikuja na nakala chahe sana... 60 tu, zikaisha na wengine wakawa wanautaka tena," alisema Mtikila mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa kuzindua chombo hicho ambacho kazi yake kuu itakuwa ni kutetea haki za Wakristo.

  "Nimegawa hapa kwa sababu viongozi wenyewe waliutaka ndiyo nikaona niwape; nisiwe mchoyo,” alisema Mtikila.

  Mtikila alisema kuwa kuzinduliwa kwa jukwaa hilo ni kuzaliwa kwa tatizo kubwa kwa Rais Jakaya Kikwete na kumtaka ajihadhari, akidai kuwa ajira yake sasa ipo kwenye "danger zone (sehemu ya hatari).”
  Mtikila, ambaye ana ujasiri wa kutoa kauli zisizo na simile, alisema jukwaa hilo ni gharika kubwa kwa Rais Kikwete kwa sababu alizodai kuwa kiongozi huyo wa nchi ni adui mkubwa wa Ukristo.

  “Wakristo nchini tupo milioni 27 hivyo ajira ya JK hivi sasa ipo shakani," alisema.
  Viongozi wa makanisa ambayo yalishirika katika kuunda jukwaa hilo ni pamoja na Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (Tec), Jumuiya ya Makanisa ya Kikristo (CCT) na Umoja wa Makanisa ya Kipentekoste (PCT).
   
 10. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #10
  Feb 5, 2011
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,784
  Likes Received: 1,970
  Trophy Points: 280
  watakaosambaratika ni viongozi wetu wanaohubiri udini na wala sio sisi wananchì. Ole wake yule anayehimiza udini maana laana ipo juu yake.
   
Loading...