Udikteta wa Serikali kwa Bunge na Mahakama

Toosweet

JF-Expert Member
May 27, 2012
2,141
1,982
Salaam Wanajamvi.
Toka kuingia serikali ya awamu ya nne mambo mengi yametokea,mengine ya kufurahisha na mengine ya kutia shaka.Miongoni mwa mambo ya kutia shaka ni tabia ya serikali na watendaji/wanasiasa wake kufanya kazi bila kuzingatia utawala wa sheria,demokrasia na haki za msingi za wananchi na maofisa wa serikali "wanaotumbuliwa".
wakati sakata la sukari lilipoanza kuvuma,Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo Mifugo na Maji alitoa ushauri kuwa ni vema Mh.Rais akatoa vibali kwa wafanyabiashara wa sukari ili sukari iagizwe na kuondoa uhaba.Badala ya kuzingatia ushauri,mbunge huyu alikamatwa na TAKUKURU kama vile yeye ndiye alisababisha uhaba wa sukari!Bila shaka alikamatwa kwa amri ya Mh.Rais
Kama hiyo haitoshi,Wabuge Mh.Zito,Mh.Waitara na Mh.Kubenea walipewa barua za kuitwa na Kamati ya Maadili ya Bunge kuhojiwa kwa nini wanang'ang'ani Bunge lioneshwe laivu!Serikali sasa kupitia Spika inataka Wabunge waseme kile kinachoifurahisha.
Nimeshangaa pia Naibu Spika alipotangaza kumkabidhi Mh.Rais fedha za kuendesha Bunge zilizoidhinishwa na Bunge kwa matumizi ya ke ili zikanunue madawati!Huku si kujipendekeza na kuchongea wengine?
Mkuu wa wilaya ya Babati naye kaja na yake,anaamuru Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo awekwe ndani kwa kuwa ametoa hukumu ambayo haikumfurahisha.Jaji Mkuu amenyamaza kimya na Tanganyika Legal Society sikuwasikia kupinga kitendo hiki.
Hivi tunaelekea wapi?Ni hatari sana kwa Serikali kuitawala mihimili mingine ya dola.Huu ni mjadala,tunaweza kujadili kwa afya ya Tanzania.
 
Back
Top Bottom