‘Udikteta’ wa Magufuli na uhuru wa kujieleza

kangomba walikuwa wanadhulmu wakulima. idea ya dr. magufuli ilikuwa njema tu lakini utekelezaji wake ulikuwa mgumu sana kutokana na kile alichokuwa anakiongea kila siku bila watu kukitilia maanani: 'vita ya kiuchumi ni ngumu'
Huwezi kuvuruga utaratibu bila utaratibu. Kwa swala korosho, mbaazi na democracy. Maghufuli alikosea big time

Odhis *
 
Sio rahisi mijizi impende magufuli. Sema kadili uwezavyo ila yule mtu huwezi mchafua kwa maneno mabaya.

Asante mungu kutuletea chuma kilichonyoosha majizi yote.

Ila magufuli kawanyoosha mpaka hamchoki kumsema?
Mungu wabariki "wale watu walee" wanaomchukia magufuli nao uzao wao utoe rais tuone nae atanya yapi?

Tunataka vitendo sio maneno.
Magufuli alikuwa kila wakati anasema "NIOMBEENI", baada ya hapo anaua watu, ana dhulumu, anasema uwongo na anaiba fedha za Watanzania. Watu kweli WAKAMUOMBEA afe na apotee. Ogopa sala za watu wengi waliodhulumiwa wakiomba kwa pamoja
 
Sisi ni tofauti , hatufungi Internet Bali tunakufunga kwenye "likiloba" na kukutupa huko.

Au unakula shaba zaidi ya 30.
Wewe unafikiri mtu anaehatarisha usalama wa nchi dawa yake ni ipi?, bira hicho kufanyika,mauaji ya kibiti yasingekona,na nyie ndio mlikuwa mnashangilia
 
Hela zipi alizoiba Magu....
usiwe bendera fata upepo utatikitwa kama mtoto wa kike
99% of antmagufuli wanatumia speculation ama assumption ama assuming ama hearsay ama mihemko, ama chuki waliyolishwa ama ujinga ama wahanga wa mifumo hewa ama ushabiki... Lakini sio facts.

Hawana ushahidi....zaidi ya kutumia niliyokwisha eleza hapo juu.

Dr JPM atabaki kuwa Rais pekee aliyesimamia na kufuatilia kwa karibu sana alichokisema na kuona matokeo katika muda mfupi wa uongozi wake. Anaweza asiwe na kauli za kupendeza ila atabaki kuwa nembo ya mtu anayeamini kuwa ukijiamini unaweza sio lazima aje mtu mwingine kufanya unayoweza kufanya mwenyewe. Huu ni ushawishi madhubuti sana kwa vijana wetu.

Ni kazi ngumu sana kuwa rais wakati unawatu wa kariba ya wapinzani na baadhi ya watendaji warafi na wabinafsi aliokuwa nao JPM but aliyosimamia yatawapunguzia sana mzigo marais wajao kwa miaka mingi.
 
Wiki iliyopita serikali mpya ya Zimbabwe iliamua kufunga upatikanaji wa intaneti nchini humo kama malipizo ya maandamano ya watu kupinga upandaji wa bei ya mafuta....
Dictator ni mtawala asiyeheshimu katiba na sheria za nchi. Unapaka rangi upepo!
 
Wiki iliyopita serikali mpya ya Zimbabwe iliamua kufunga upatikanaji wa intaneti nchini humo kama malipizo ya maandamano ya watu kupinga upandaji wa bei ya mafuta...
Panua wigo, udikiteta wa Magu haupimiki kwa kigezo kimoja kama hicho, udikiteta wa magu ulikuwa all round, na kibaya zaidi hakuthamini uhai wa binadamu. Mauaji, ukatili wa waziwazi, unyang'anyi na uporaji, kuminya demokrasia, utawala msonge na uchafu mwingine mwingi! Akaigeuza Nji kama kampuni ya baba yake!
 
Wiki iliyopita serikali mpya ya Zimbabwe iliamua kufunga upatikanaji wa intaneti nchini humo kama malipizo ya maandamano ya watu kupinga upandaji wa bei ya mafuta.

Hapa Tanzania kuwekuwepo na kila aina ya lawama kwa utawala wa Rais Magufuli.

Rais Magufuli keshaitwa kila aina ya majina. Jina ambalo limekuwa likijirudia rudia ni ‘dikteta’.

Nikiri kuwa hata mimi mwanzoni mwanzoni mwa utawala wake kuna mambo sikuyapenda na niliutumia huo utambulisho wa ‘dikteta’ kuelezea kutopendezwa kwangu na baadhi ya mambo .

Lakini kwa kadri siku zinavyokwenda, yajiriyo hapa nchini na nje ya nchi, yananifanya nianze kujiuliza kama ni jambo sahihi kumwita Rais Magufuli dikteta.

Kuna watu humu mitandaoni wanapenda kulalamika kuwa eti Tanzania sasa hivi hakuna uhuru wa kutoa maoni na uhuru wa kujieleza.

Mara nyingi watu hawa hutoa malalamiko yao kupitia mitandao ya kijamii.

Sasa kilichotokea huko Zimbabwe wiki iliyopita kimenfanya nijiulize upya kuhusu huu udikteta wa Rais Magufuli.

Hivi ni lini hapa Tanzania tumewahi kufungiwa kabisa huduma ya intaneti kutokana na maandamano au sababu ingine yoyote ile?

Kilicho ironic ni kwamba hao wakosoaji wa Magufuli kuhusu uminywaji wa haki za kidemokrasia za kutoa maoni na kujieleza, hutumia intaneti kutoa maoni yao wakiwa hapa hapa nchini.

Huyu Magufuli ni dikteta gani anayeruhusu watu wamkosoe, kumpinga, na hata kumtukana huko kwenye mitandao ya kijamii lakini hachukui hatua kali za kuifungilia mbali intaneti kama alivyofanya Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe ambaye kaingia madarakani majuzi tu hapa?

Watanzania wakati mwingine huwa tunabweteka sana na uhuru tulionao!
Tatizo upinzani wanataka wawe kambale na madevu kama serikali. Serikali wakisema twende huku lissu na mbowe wanasema geukeni huku eti ndio uhuru wa maoni? Serikali ndio dola ina majeshi lazima itawageuza watu kuelekea chama chenye ridhaa ya wananchi kinavyotaka.
 
Panua wigo, udikiteta wa Magu haupimiki kwa kigezo kimoja kama hicho, udikiteta wa magu ulikuwa all round, na kibaya zaidi hakuthamini uhai wa binadamu. Mauaji, ukatili wa waziwazi, unyang'anyi na uporaji, kuminya demokrasia, utawala msonge na uchafu mwingine mwingi! Akaigeuza Nji kama kampuni ya baba yake!
Ukishagusa nafasi ya urais ...kuwafunga baadhi ya watu midomo ni jambo lisilo epukika duniani kote.
 
Walinyamazishwa wangefanya nini? Hadi viongozi wakuu wastaafu waliambiwa "waache kuwashwawashwa" Hivi huamini kwamba jamaa alikua mbabe? Dictator?
JK alikuwa na mpaka sasa anawashwawashwa... Na Samia akijichanganya mkwele hachelewi kumpanda kichwani kwa kisingizio cha u mentor. Mpango hana say zaidi ya kufuata maelekezo ya boss... na vile mnyenyekevu atakuwa anakimbia kimbia tu.
 
Ulimpenda wazi sana marehemu wewe zee!! hao wazimbabwe si wanafungiwa tu basi! but wako hai,

lkn huku kwetu wana hack mazungumzo yako ikibidi ufe kimya anzori gwanda, sometimes na usijulikane!! kama yalee ya January na babake!!! pia ilikuwa ni risasi tu!!!... kifo!!! kifo na wewe! kutupwa ndani bila maelezo!! kupotezwa mazima!!! mpaka watu wengine humu wameponea chupuchupu kupotezwa,

na wengine wamepotea mazimaa hatujui wako wapi japo wameacha alama!! lile jamaa hata ujipendekeze vipi km hivi unavo fanya wewe likikuhisi tu!! umeondoka mazima! lilikuwa halijali. Bulldozer bovu!
 
36 Reactions
Reply
Back
Top Bottom