Udikteta umea kwa Hatua, hizi tunazoziona ni hatua.

Kisonono

Member
Sep 23, 2016
27
45
Hali ilivyo sasa katika nchi yetu inazidi kutoa mwelekeo thabiti kabisa kwamba sasa tunaelekea katika nchi ya ubabe ( udikteta). Wengi wamekwisha eleza dhana hii na kutaadharisha juu ya athari zake za muda ama za moja kwa moja zitakazotukumba kama Nchi ( taifa).

Tumeona juhudi za kutosha kabisa zinazofanywa na watawala wetu katika kuminya Uhuru wa watu kusema, kueleza ama kukosoa mambo ambayo kimsingi wanaona hayaendeshwi sawa sawa na watawala wao.

Duniani kote na katika historia tumesoma na kujielewesha kuwa utawala wa mabavu katika nchi haujawahi kuzuka Mara moja na ukapaa, utawala wa mabavu katika nchi uja kwa hatua na kwa maandalizi, na moja ya hatua za awali kabisa katika maandalizi ya ujio wa utawala wa kimabuvu ni kwanza watawala kuhakikisha wanatunga sheria kali na kandamizi zinazotoa fursa za kuwalinda wao pekee, kisha kuminya sauti za wanaharakati ama watetezi wa jamii, zaidi kuwafumba wasomi midomo kwa kuwapa ajira nono na kuwatia njaa kali baadhi. wataendelea kwa kuwakamata na kuwabambikizia kesi vinara wa mapinduzi ya kifikra katika nchi, kama tunayoyaona yakiendelea sasa kwa ujumla Uhuru wa maoni unabanwa.


Katika hatua nilizozisema hapo juu, sina shaka kuwa zimekwishafikiwa kwa ukamilifu kiasi na hawa watawala tulionao, naendelea kusema kwamba watawala wakishafanikiwa kunyamazisha wanaharakati aidha kwa kutunga sheria hizo kandamizi ama kwa kuwapandikizia kesi zisizo halali basi uamia katika kuhimarisha misingi yao ya kiutawala ili izidi kuogopwa na wengine, hususani wanaharakati chipukizi.

Haya ninayoyasema hapa yamekuwepo na yalionekana Duniani zama zile za Adolf Hitler kule Ujerumani, Benito Mussolini akayoonyesha Italia, Mobutu Sese Seko wa Congo DRC enzi ikiitwa Zaire, Sani Abacha wa Nigeria, hata fashisti Idd Amin Dada wa Uganda alifanya hivi zama za mwanzo kabisa za utawala wake.

Makosa waliyoyafanya Wajerumani, Waitaliano, Wakongo Man, Wanaigeria ama raia wa Uganda zama hizo naona tunayarudia nasisi, wakati Hilter anaanza kupandikiza umabavu Ujerumani watu walikaa kimya ama kwa kujua ama kutokujua athari zitakazowakumba baadae. Sisi leo hatuna sababu labda tuseme tunauitaji ubabe, kitu ambacho sijafikiria kama tuna akili za namna hiyo. Nasema hatuna sababu kwasababu tunajua athari za kukaribisha utawala wa kimabavu katika taifa.

Tunaitaji mjadala mpana wakitaifa kujadili haya tunayoyaona. Nasema ni lazima tukachukulia swala hili katika uzito wake na kulijadili kwa mapana yake kuhusu mienendo hii ya watawala hawa wa sasa.

Baadhi yetu wanaweza wakaja na hoja nzito kuliko yangu, hoja yakupinga ninachosema, mnaweza kweli mkanishusha kwa hoja zenu kwamba ninachosema ni uongo ama ushabiki, ama nimetumwa na chama fulani kusema haya ninayoyasema, hakika mtaweza kuniandama kutokana na maslahi yenu na watawala. Ninaweza kweli nikashuka hoja yangu ikafa lakini historia utunzwa na itakuja kuwageuka siku za mbele.

Wapo watu amabao wananufaika hata katika hali ya namna hii, hili liko wazi kabisa kwa sababu hata zama za ukoloni wapo wa afrika hawakupenda wakoloni waondoke, hawakupenda kwasababu walikuwa wakinufaika wao binafsi na zaidi wakiwakandamiza waafrika wenzao.

Nchi hii tuliyomo ni yetu sote, sote ni wazawa wa hapa, Sote tunapaswa kuheshimiana, kupata fursa sawa za kusema, kushauri na kutaadharisha pale tunapoona mambo hayaendi sawia, lakini cha kustaajabisha watawala hawa wanataka kujipa hati miliki ya nchi. Hawataki wengine waseme, hawataki wengine washauri, hawataki wasioridhika na utendaji wao wakosoe, Je? huu sio utawala wa kimabavu?

Hatukuchagua Raisi ili aje afanya mambo hayatakayo bali tulimpa nafasi yakututumikia kwa kufanya mambo ambayo sisi wananchi kwa uwingi wetu tunayataka. Sasa katika hali kama hii ambayo huyu Raisi ( Mtawala mkuu) anafanya mambo tofauti kabisa na maagizo yetu basi tunatakiwa kuwa na nafasi ya kusema, yakukataa na kutaadharisha njia aiendayo kwamba si maagizo ya umma wetu kwake.

Mwisho namalizia kwa kurejea maneno yangu ya awali kabisa kwamba utawala wakimabavu katika dunia haukutokea kwa gafla tu, yaani watu walilala na kuamka wako katika utawala wa kimabavu, La hasha utawala wa kimabavu ulimea kwa wananchi wenyewe kulea mambo madogo madogo kama haya yakukandamiza uhuru wa watu kusema, kutafuta na kutoa habari, watawala waliachwa wakapanda hizi mbegu za ukandamizaji wa haki za watu. Polepole mazoea haya yakaendela na wakajenga tabia yakukandamiza haki hizo na zingine na mwisho watawala wakahodhi madaraka yote na hata ikafika mahala wakahodhi na haki ya mtu kuishi ( uhai) ikawa juu ya maamuzi yao.

Tunalea udikteta, tunanyamaza kwa uoga ama kwakulinda maslahi yetu ya matumbo. Athari za wazi zitakapojitokeza hazitatuacha tukiwa huru zitatuadhibu sawia na matendo yetu
 

paliemba

JF-Expert Member
Nov 21, 2016
445
250
Naogopa saana siku watu wakijenga akilini kwamba haki haipatikani kidemocrasia sijui ninikitatokea mungu tunusuru
 

mshunami

JF-Expert Member
Feb 27, 2013
3,989
2,000
Hivi na kule vijijini wanawaza na kufikiria kama mnavyofanya ninyi watu wa mjini? Mkisema fedha zimepotea katika mzunguko, wao hawaoni hivyo kwa kuwa hali kule ni kama kawaida. Mkisema vyombo vya habari vimekendamizwa wao hawana habari kabisa. Magazeti hayafiki kwao. Mkisema "jamii forum" wanaweza kuuliza kuwa huyo ni mdudu ama mnyama? Wao CCM ndiyo iliyomwondoa mkoloni...full stop. Ukisema sembe imepanda bei, kwao sio mara ya kwanza na ni suala la msimu tu. Hata sukari wao wananunua zaidi ta 2500 kwa kilo na wamezoea. Magufuli ndiye raisi wao na inawatosha. Hawa ndo ngome na watetezi wakubwa wa CCM na wanajiandaa kwa uchaguzi 2020 ili kukipa chama chao ushindi wa kishindo! Ninyi wa mjini mna taabu kweli kweli!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom