"Udikteta uchwara" Tujipime kweli na sisi ni wapenda Demokrasia ....?

2kimo

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
2,029
2,071
Hii imekuwa ni changamoto kwa tawala nyingi za Africa kushutumiwa kwa udikteta.
Ukweli unabaki kuwa jinsi unavyotaka kuwa na mtazamo tu juu ya kiongozi wa Nchi na si lazima iwe kama Wengi wanavyotafsiri!
Hulka binafsi za watawala ndizo zinazoleta changamoto hapa na baadhi ya sababu kuu ktk hilo ni hizi:-
  1. Mila na tamaduni
    • Tamaduni na makuzi ya kiongozi yanaweza kuathiri kwa kiasi kikubwa aina ya utawala wake. Tutumie mifano ya viongozi wetu wa Nchi na wanne wanaweza kutupa taswira nzuri zaidi.
    • Kikwete na Mwinyi
    • ni maraisi wanaotoka pwani, hawa wameishi kwenye matrilineal society ambapo kinship ya mwanamke ni dominant, sio wanatawaliwa na wanawake, lkn mjomba kwa mfano anasauti sana kwenye familia pamoja na uwepo wa baba. So Kuna kiasi baba anakosa absolute power kwenye maamuzi ndani ya familia yake. So through upbringing mkuu wa kaya anajifunza diplomasia Kwani maamuzi yake sio final. The same kwa mjomba naye hana maamuzi 100% kwenye familia ya dada yake naye analimitations.
    • Magufuli na Nyerere
    • Hawa wanatoka kanda ya ziwa ambapo ni patrilineal societies, huku baba ana absolute power, yeye ni final na hakuna wa Kum contradict, kujadili ni maamuzi yake lkn hiyo haiwi entertained sana. Wengi wako less diplomatic kwa kuwa si kitu ambacho wamewahi kukiishi au hata kukishuhudia nyumbani. Huku ukiwa na power hakuna wa kukugusa na ni jambo la ajabu kumchallenge mtu mwenye power na halikubaliki hata kidogo.
  2. Dini
  3. Dini zimekuwa na athari kubwa sana kwenye kutabiri aina ya uongozi, ingawa Dini haibadili sana Ila mchango wake wakati mwingine ni significant.
    • Uislam kwa mfano huwa unakataza sana mtu kuwa na kiburi na maringo, uislam unamhukumu Moja kwa Moja kiongozi dhalim na pia kwa hadithi nyingi zinazoonesha watu walioangamia kutokana na kiburi, kuonea watu au kufanya dhulma! Ukatili wowote hata kwa mdudu, mfano kumchoma moto mdudu kwa lengo la kumtesa au kuua mnyama mwenye kiu akiwa anakunywa maji (huruhusiwi hata kuwinda mnyama anayekunywa maji mpaka atoke hapo anapokunywa maji Kwani ni ukatili kumkatisha mwenye kiu kunywa maji). Siwezi kuelezea sana kuhusu teachings za kikristo kuhusu maisha ya kijamii, nitahitaji msaada kwenye kujazia hili, Ila najua zinachangia pia kumbadili msimamo kiongozi.
  4. Elimu
  • Kwa kiwango kikubwa elimu inachangia jinsi mtu kuweza kukabiliana na changamoto. Kwenye elimu Kuna kujifunza kuchanganyika na watu, kunakufundishwa taratibu za uongozi na wakati mwingine kusafiri nje ya eneo lako la asili kunakufanya ujifunze tamaduni nyingine hivyo kukuacha ulegeze misimamo ya maisha kulingana na malezi yako kama nilivyoainisha kwenye namba 1. above.
Kulingana na msukumo mkubwa wa kiasili na malezi kwenye maeneo yetu ya asili hasa wakati wa ukuaji, tabia za ndani ya jamii tunazoishi zinatuathiri zaidi kuliko Mambo mengine! Malezi hasa unapoishi hasa kwenye umri mdogo zinatuathiri zaidi ya asili ya maeneo yetu tuliyo-originate though Kuna some elements bado tutaendelea kuwa nazo. Mfano mzaramo au mmasai aliyelelewa New York hatoishi kulingana na asili yao labda mutrilineal au patrilineal au zile Mila za kimasai au kizaramo hazitokuwa maintained na zile za New York ndio zitamkaa zaidi. Hivyo utaona tamaduni za eneo unalolelewa (hasa ndani ya familia na sio nje ya familia, ingawa jamii pia itachangia) ndizo zitakuathiri kuliko kitu chochote kwenye maisha yako.

Back to msingi mkuu wa our topic, viongozi Wengi wa kiafrica wataonekana kwenye macho ya wengine kuwa ni madikteta, Kwani hata baba au mume wa kiafrica huonekana katili kwa aina ya mifumo tunayoishi.
So tuache kelele, tusishikiwe akili na watu wa magharibi ambao wanatamaduni tofauti sana na hizi za kwetu, kila mmoja ajitazame anapokuwa na power anazitumiaje?
Ukiwa mume je ni Kweli unaruhusu demokrasia kwenye ndoa yako? Kwa kiasi gani? Baba au mama ni kiasi gani cha demokrasia una exercise? Boss vs watu wa chini etc.... Ni rahisi kudeal na kibanzi cha mwenzio na kusahau boliti yako....
Sioni udikteta wa viongozi wetu, Ila it's true Kuna wakati wanakosa ku-sikiliza watu na there are times wanakuwa wapole mno kwa kadri maumbile na makuzi yao yanavyowaongoza na kutufanya tuwaite wadhaifu! Lakini yote hayo hayajengwi na ukatili au dhamira mbaya bali zile hulka za kawaida za kwetu kuwa kiongozi lazima uwe mkali watu wasikuchezee kama baba/mama anapokuwa hataki mchezo na watoto......
Kama waafrica wote tunavyochapa watoto, Kuna Mila mwanamke anapigwa akikosea etc, Sisemi kuwa ni sahihi Lakini wenzetu huona wazazi wa kiafrica ni wakatili au waume wa kiafrica ni wanyama.. ingawa sisi husema kuwa hizi ni tamaduni zetu wasituingilie, so hata raisi wetu hawawezi kumuelewa kama wanavyoshindwa kuelewa ndoa zetu na malezi yetu ya watoto..... Tusikubari kupangiwa!!
 
Tusishabikie udikteta kwa kigezo chochote!! Tatizo tulilonalo ni katiba yenye elements za kikoloni iliyorundika madaraka ya ki Mungu kwa Rais na kuziacha taasisi za ki utawala kibogoyo zikitegemea maamuzi kutoka kwake.

Kiongozi kama wetu angekuwa mzuri kama katiba yetu ingekuwa ya wananchi na si ya watawala dhidi ya wananchi.
 
""MTAZUNGUMZA MENGI MWAKA HUU ILA UKWELI UTABAKI PALE PALE ""

WATANZANIA WANAITAJI MAISHA BORA SIO BORA MAISHA

MANENO KAMA UDIKTETA, DEMOCRASIA SIJUI MAFISADI SIJUI DINI SIJUI KABILA HAYA MAMBO YALIKUWEPO TANGU ZAMANI ""

Maisha bora ndo mpango mzma kwanza
 
Back
Top Bottom