Udikteta ndani ya Mfumo wa Vyama Vingi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Udikteta ndani ya Mfumo wa Vyama Vingi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Regia Mtema, May 15, 2010.

 1. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #1
  May 15, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Tangu tupate uhuru hadi leo hatujawahi kuwa na Demokrasia katika maana yake na upana wake, tulikuwa na uongozi au utawala wa chama kimoja. Rais alikuwa na mamlaka yote, chama kilikuwa kinaongoza Serikali kwa mwongozo wa Rais. Huu ulikuwa ni Udikteta namba moja. Bahati tuliyokuwa nayo ni kwamba tulikuwa na Udikteta Mtakatifu. Udikteta huu ulitufaa kiasi chake kwa vile dikteta mwenyewe alitenda kwa manufaa ya wananchi. Huyu alikuwa Baba wa Taifa, hayati mwalimu J.K Nyerere (Mungu amweke mahali pema mbinguni, ampe Heri na Utakatifu).

  Mwalimu aliamua na kuelekeza siyo kwa manufaa yake au familia yake au kabila lake, bali kwa manufaa ya watanzania wote. Binadamu wote tunakasoro. Kinachoangaliwa ni makusudio mema japo watekelezaji waweza kupindisha makusudio hayo.Nyerere aliteua Wakuu wa Mikoa,Wakuu wa Wilaya, Jaji Mkuu, Mwanasheria Mkuu, Gavana wa BoT na viongozi wengine kama hao. Hawa walioteuliwa nao waliteua waliokuwa chini yao hadi ngazi ya tarafa. Huo ndio uliokuwa udikteta mzuri wenye nia njema kadiri ya dikteta.

  Utawala wa kiimla ndani ya chama kimoja waweza kuwa mzuri kwani hata Bunge linakuwa moja lenye msimamo mmoja kwa maslahi ya wananchi kwa sababu nalo linapata maelekezo kutoka kwa Waziri Mkuu aliyeteuliwa na dikteta mwema, mwenye kulenga maendeleo na maisha bora ya wananchi wake. Hiyo nayo ni Demokrasia ndani ya chama kimoja.

  Kasheshe, songombingo inaanzia pale unapokuwa na Demokrasia ya Vyama Vingi ambako kuna kutokukubaliana na kutofautiana kwa Mtazamo,Malengo na Itikadi lakini mfumo mzima unabakia kama ule ule wa chama kimoja hapo ndipo neno Demokrasia linapokosa maana yake na maendeleo ya nchi yanaanza kurudi mwendo hasi (Development of Underdevelopment).

  Rais anachaguliwa kidemokrasia kwa kupigiwa kura na wananchi,baada ya kuingia madarakani Rais huyu anaunda Baraza lake la Mawaziri na kuanza kufanya teuzi mbalimbali kama ifuatavyo;  Rais anateua Msajili wa Vyama Vya Siasa
  Rais anateua Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi.
  Rais anateua Wajumbe wa Tume hiyo
  Rais anateua Mwanasheria Mkuu wa Serikali
  Rais anateua Jaji Mkuu(Kada wa Siri)
  Rais anateua Waziri Mkuu-Mwanachama-Kada
  Raisa anateua Majaji-Wanachama
  Rais anateua Wakuu wa Mikoa
  Rais anateua Wakuu wa Wilaya
  Halmashauri za Wilaya zinaajiri Maafisa Watendaji wa Kata-ambao ni wawakilishi wa Mkuu wa Wilaya.

  Na Mauteuzi mengine kibao.

  Hapo ndipo Udikteta ndani ya Mfumo wa Vyama Vingi unakamilika.Hakuna kushirikisha wananchi.Wananchi wakimchagua kiongozi wao kuwa Mbunge,Rais anamchomoa anakuwa Waziri ,au Naibu Waziri au Mkuu wa Mkoa,Kiongozi huyu anakuwa upande wa Serikali,msemaji wa Serikali na sio mtetezi wa wapiga kura wake kwenye jimbo lake.Timu ya Udikteta inaimarika.

  Je tunayo Demokrasia Tanzania kwa muundo huo,Mabalozi wanatusifia nini?Au ndio kwa mgongo wa chupa wanatupaka mafuta waendelee kutupora?

   
 2. G

  Godwine JF-Expert Member

  #2
  May 15, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  demokrasia ni matokeo ya mfumo unaokubalika na wengi katika minajili ya uongozi uliochaguliwa na wengi , pili demokrasia maana yake si mfumo wa kuchagua viongozi bora bali ni mfumo wa kuchagua kiongozi anayekubalika na wengi hivyo basi ata kiongozi mbaya akichaguliwa na jamii basi huo na mfumo na matokeo ya demokrasia lakini kikubwa zaidi ni jinsi gani ya kuongoza kwa kufata misingi ya demokrasia? kwa mfano wawakilishi wetu (wabunge) kama wakishiriki katika kuandaa mfumo ambao si mwema kwetu na kuupitisha bungeni basi mfumo huo utakuwa umepita kidemokrasia ingawa unaweza usiwe na maslahi kwa jamii husika, hivyo basi kama tunawawakilishi wetu ambao wameendelea kuona mfumo wa rais kuteua watu mbali mbali bila wao kuupinga basi mfumo huu ni wa kidemokrasia na si wa kidikteta , hii si kwetu tuu kwani ata mataifa makubwa kwa mfano marekani wana mfumo wa kumchagua rais kwa minajili ya super deligate na wao wameona ni sawa ingawa kuna jamii ikiingia ndani zaidi inaweza kuona kuwa mfumo ule si wa kidemokrasia,
  kwahiyo basi mimi naona kama tunawawakilishi wetu na bado hawajapinga mfumo wa uteuzi wa rais basi mfumo huu ni wa kidemokrasia na ni mfumo huru mpaka pale wawakilishi wetu watapoukataa na kama rais akipinga mapendekezo yaliyoletwa na wawakilishi wa wawananchi.

  kazi hipo katika kujenga demokrasia
   
 3. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #3
  May 15, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,569
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  Very strong points GS,ngoja niyapeleke baadhi ya maswali haya kule kwenye ile thread ya maswali kwa CCJ.
   
 4. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #4
  May 16, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Demokrasia huendana na jamii. Kinacho onekana demokrasia sehemu moja sehemu nyingine inaonekana ni udikteta. Kwa hiyo kujitawala ni makubaliana ya jamii fulani kwamba hichi ndicho sisi tunacho kubali ndiyo demokrasia. Nitoe mfano. Kwenye familia nyingi za Kitanzania baba ndiyo mwenye sauti. Mama na watoto wanaweza kutoa mawazo yao lakini kitu baba aki sisitiza basi ndiyo inakua hivyo. Kwa nchi za ulaya baba(au mume) hana nguvu kama baba wa Kiafrika kwa maana kila kitu ni lazima akubaliane na mke kwenye maamuzi. Sasa kwa hali ya familia zetu mwanamke wa kizungu ana weza kuona ni kukandamizwa kwa mwanamke na wakati kwetu mwanamke asipo mtii mumewe basi hata mama ake hato mtetea.

  Demokrasia pia hukua. Ukiangalia historia nchi ya kidemokrasia ya kwanza utaambiwa ni Ugiriki. Walikua na bunge ambalo siyo kila mtu alikua na uhuru wa kupiga kura. Wapiga kura walikua wanaume wa tabaka fulani tu. Hiyo kwao ilikua iki julikana kama demokrasia lakini kwa leo hii ukiangalia hauwezi kuita hiyo ni demokrasia. Hata ukiangalia nchi za leo zinazo jiita vinara wa demokrasia kuna kipindi si muda mrefu sana wanawake na watu weusi walikua hawana haki ya kura. Kwa hiyo demokrasia hukua. Tanzania ili toka kwenye mfumo wa utawala wa kijadi mpaka "demokrasia" ya kisasa kwa hiyo ni gradual change. Ukiangalia baada ya vita kuu ya kwanza Ujerumani iliyo kuwa iki tawaliwa kiufalme ilikua na wakati mgumu kukubali na kupokea utawala wa kidemokrasia.

  Demokrasia pia ni uamuzi wa watu walio wengi. Tafsiri ya demokrasia ni kila mtu kuwa na uhuru wa kuchagua na chaguzi la wengi ndiyo linalo chukuliwa. Hiyo ndiyo demokrasia. Kwa hiyo mpaka hapo Watanzania walio wengi wakisema utawala tulio nao sasa si demokrasia basi mfumo uliyo baki uta baki kuwa demokrasia. Kwa hiyo basi tuki taka mabadiliko ya kweli ya kidemokrasia basi ina maanisha siyo kwamba mimi Mwanafalsa1 nataka nini au wewe Gender Sensitive una taka nini bali lazima iwe sisis Watanzania kwa pamoja tuna taka nini.
   
 5. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #5
  May 16, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Sisi ndio wawakilishi wenyewe na tunapinga hili.kwani hujasikia sera ya majimbo ya CHADEMA,hujasikia tukipinga baadhi ya teuzi za Rais?au labda mwenzetu u nataka wawakilishi gani hao wapinge ndio uone wamepinga na je labda unataka wapinge kwa staili ipi ndio uone wamepinga?
   
 6. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #6
  May 16, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Umeiwakilisha vyema signature yako.
   
 7. G

  Godwine JF-Expert Member

  #7
  May 16, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  nakubaliana na wewe kwamba mnapinga lakini kama ulivyoeleza katika msingi wako kwamba demokrasia inaelemea kwenye mahamuzi ya wengi kwa hiyo basi kama mkiweze kutawala vyombo vya mahamuzi au kuwa na ushawishi mkubwa katika vyombo hivyo mtaweza . pili inawezekana kwa upande mwingine wanaopenda rais awe na mahamuzi ya kuteua nao wanaweza wakasema wao ni wengi kuliko mnaopinga
  kwa mfano ukiangalia wakati wa kupitishwa kwa mswada wa usalama wa taifa wengi walipinga kifungu cha sheria kitachomuondolea rais uwezo wa kutangaza vita yani kuwa amiri jeshi mkuu hii inahashiria wananchi wengi wa tanzania wanapenda rais mwenye mamlaka makubwa zaidi kwa hiyo katika hoja yako ujatuthibitishia kwamba wangapi wanapenda uwezo wa rais kuteua upungue
   
 8. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #8
  May 16, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu.Demokrasia ni zaidi ya hapo.Umemsoma vizuri Mwanafalsafa1 hapo juu?ameeleza kwa kina kama Mwanafalsafa.Sio suala la wengi wape kama unavyodhani.
   
 9. G

  Godwine JF-Expert Member

  #9
  May 16, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  sema kitu cha msingi unachoweza wewe kufanya kukuza demokrasia ni kuelimisha umma upate kufanya mahamuzi mema katika kuchagua lakini msingi wa wengi wape ndio utaendelea kutumika katika anga za siasa kwani katika kila jamii itaendelea kuwa na misingi yake mpaka yatapotokea mabadiliko ambayo mara nyingi chanzo chake ni jamii yenyewe
   
Loading...