Udikteta na ukandamizaji haki wa Serikali za vyama kongwe vinavyotawala hadi leo. Sababu...

kagoshima

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
2,631
5,137
Mifano ni mingi lakini chukulia chukulia mifano ya hivi vyama na inchi husika hapa chini .

1. CPDM cha Cameroon
2. CCM cha Tanzania
3. ZANUPF cha Zimbabwe
4. Frelimo cha msumbiji
5. PDG huko garbon

Utagundua kwamba inchi zote tajwa hapo juu serikali zao zinaongozwa na vyama kongwe vilivyopokea madaraka mojakwa moja kutoka serikali katili za kikoloni. Na havijawahi kutoka madarakani mpaka.

Hizo inchi zote zinaongozwa kidictetor si kwa bahati mbaya. Ni kwamba vyama husika vili rithi mambo mengi kutoka serikali za kikoloni zikiwemo katiba za uendeshaji wa inchi. Hata baadhi ya sheria kandamiz za kikoloni ziliendelea kukumbatiwa na watawala hawa wapya.

Wataalam wa mambo ya wanyama poli wanasema nyoka aina ya koboko ni hatari zaidi jinsi anavyokuwa mzee.

Vivyo hivyo kwa hivi vyama kongwe. Jinsi miaka inavyoenda vinazidi kuchokwa na wananchi kwa sababu ya mkusanyiko wa maovu wa miaka mingi ya kukaa madarakani mfano rushwa, ufisadi nk.

Matokeo yake vyama dola hugeukia mbeleko ya dola huku wakihesabu siku ziende na hapo ndipo wenye inchi hukiona cha moto zaidi ya wakati wa ukoloni.

Wanachofanya CCM sasa si bahati mbaya. Usikute wangependa hata ugonjwa utokee uangamize wote wenye mtazamo mbadala.

Hapa bado huko tuendako ndo kutatisha zaidi.

Inchi kama Kenya, Zambia, Malawi, Senegal, Ghana, na zingine wana enjoy Uhuru na democracy ya kweli baada ya kupiga chini vyama kandamizi vilivyo rithi madaraka kutoka serikali za kikoloni. Kazi kwenu wabara na visiwani.
 
Back
Top Bottom