Udikiteta Tanzania: Je, Rais Magufuli kweli ni dikiteta au wanamsingizia tu? Msikie Mwalimu Nyerere kuhusu udikiteta!

Hakuna Rais aliyekuwa anaogopwa Tanzania kama Mwl Nyerere.

Kama sifa ya udikteta ni kuogopwa basi Mwl. Nyerere alikuwa ni dikteta.

Kikubwa zaidi yeye aliamua hata kuondoa kwenye katiba kifungu kinachohusu haki za binadamu.

Yeye aliingia madarakani kwa njia ya vyama vingi lakini alipoapishwa akaamua kufuta vyama vingi lakini cha kushangaza zaidi, alipong'atuka kutokana na nchi kuelekea kufirisika, akaamua kuwalazimisha wengine waanzishe mfumo wa vyama vingi.

Ninakuhakikishia kama utawala wa Mwl. Nyerere ungekuwa ndio kwa sasa, hata hawa wanaosema Rais Mgufuli ni dikteta wasige thubutu hata kutamka maneno wanayotamka.

Huwa ninawashangaa sana watu wanajaribu kujenga hoja kuhusu haki za binadamu kwa kutumia kioo cha utawala,wa Mwl. Nyerete.

Kwa hiyo kama ji udikteta, basi tumwangalie Rais Magufuli kwa kutumia kioo cha matendo ya Mwl. Nyerere wakati akiwa Rais wa Tanzania.

Kwangu mimi sioni tofauti ya kuvunja katiba au kuibadilisha katiba na kuwa katika msingi wa udikteta.

Mwl. Nyerere alikuwa anaibadilisha katiba ili kuimarisha udikteta wake huku akidai ni kosa kuvunja katiba. Mwl. Nyerere hakuhitaji kuvunja katiba kwa sababu alikuwa na uwezo wa kuibadilisha apendavyo.
Dawa imekuingia kweri,kweri
 
“Tujenge utamaduni wa kudhibiti viongozi wetu kama wanavunja sheria ya nchi (Katiba) tusiogope, mkianza, mkiwa na woga, I’m, I promise you, mtatawaliwa na dictators, (huku anacheka), I promise you, mkiogopa ogopa namna hii, nyinyi, wabunge, nani, wote mkiogopa ogopa, mkisema mzee wanakuwa wakali, then you are making it absolutely certain, you will be under a dictatorship" mwisho wa kunukuu.
Indeed we are under a DICTATORSHIP now!!!!!!
 
Hii mada ni nzito kwelikweli na ni maji ya shingo kwa sie wengine!

Hivyo basi, binafsi nawaalika na kuwaachia mada hii Wachambuzi Mahiri, Nguli, Wakongwe na Kindakindaki kama ndugu yetu na kaka yetu wa miaka mingi Mzee Mwanakijiji.

Eti MM, with reference to your 2011 Thread inayoelezea Sifa za Madikteta; je unadhani JPM ni dikteta au wanamsingizia?

Ili nisikuchoshe, nimeonelea nikuwekee thread yako hiyo na kwa kutumia umahiri wa kiwango cha hali ya juu kabisa; hivi ndivyo ulipata kutudadavulia Sifa za Madikteta WOTE duniani:
Ikiwa Mchambuzi Nguli na Mahiri Mzee MM amesema; mimi nani nitie neno?

Naona mwanakijiji kamuanika Dikteta wetu mpaka na tabia zake ambazo hazijajitokeza.Mpaka future yake dikteta huyu imedadavuliwa na MM.
 
I promise you mtatawaliwa na dictactos mkiogopa ogopa namna hii nyinyi wabunge,nani wote mkiogopa you will be under dictatorship

Mwaka 1994 sio mbali sana leo takribani miaka 14 imeshapita hatimaye unabii unatimia

RIP Mwalimu Mungu alikupa jicho la rohoni uliona TZ itaangukia wapi sasa mwiba uko kooni mwetu

24 yrs
 
Pascal Mayalla Ukitaka kujua madhara ya demokrasia iapply nyumbani kwako.
Mwanao awe na uhuru wa mawazo, akiamua siendi shule - mwambie hewala.

akikwambia kuangalia katuni ni bora kuliko kusoma - mwambie sawa mwanangu! Hiyo ndio demokrasia.

Ikiwa anachofanya Magufuli ni "udikteta" basi nimegundua Demokrasia ndio ADUI mkuu wa waatanzania na ndiye chanzo cha UMASKINI wetu.

Hapo naona unachanganya dira na kanzu.Kama sheria za nyumbani zinamlazimisha mtoto kwenda shule unadhani akikataa kwenda ni haki yake?
 
sema wewe lazima uandamane usiwajumuishe wengine, mimi namuona ni kiongozi safi anayefanya juhudi kubwa kuwaletea maendeleo wananchi wake, anakomesha kwa vitendo ufisadi, anapambana na rushwa kwa vitendo, anahamasisha watu wafanye kazi ili kujipatia vipato halali. wale wote wanaosema ni dikteta ni wanasiasa uchwara tu.

Hata hitler aliwapatia maendeleo UJERUMANI.Kuna aina mbalimbali za maendeleo.
 
Sasa Hitler unamlinganisha na nani!

Unaweza ukajenga madaraja na mi fly over kila kona lakini ukafeli kwenye kuwaunganisha wananchi kuwa kitu kimoja.Unaweza kujenga madaraja barabarani na vilevile ukajenga madaaaja ya chuki katika jamii.Kiongozi mwenye busaraa hawezi kudili na misismamo yake binafsi bila kuangalia uelekeo wa Taifa kimahusiano LABDA KAMA NI DIKTETA.
 
Unapojaribu kulinganisha kauli za mwl Nyerere na Matendo ya Magufuli nadhani haitakuwa sawa.Hebu jaribu kuwalinganisha katika vitendo vyao ni kwa kiasi gani vinafanana na kutofautiana.Mwl Nyerere kipindi cha utawala wake wengi wa wapinzani wake waluiuliwa na wengine kukimbia nchi hadi leo hatujuwi kama wazima ama laa.
Mwl Nyerere alifuta vyama vingi kipindi cha utawala wake mbona huongelei kama kweli unatafuta usahihi wa matendo yake dhidi ya Magufuli tatzo lenu mnajaribu kumtukuza Nyerere na kumuweka katika kundi la watakatifu kitu ambacho sio sahihi.
Rais Magufuli hana udikteta wa aina yeyote ile kwa factors of dikteta sema ana mapungufu yake as human being kama walivyo watangulizi wake.Democracy ni dhana pana ambayo kila kiongozi anachukuwa sehemu fulani na kukifanyia kazi huwezi kutumia democracy fully hata hao ambao tunaona kama mfano wa kuigwa hawana demokrasia hiyo.Ni mara nyingi nimeshuhudia police wakitawanya waandamanaji USA hata Ulaya.
Maandishi yangu yanaweza yakachanganya sbabu niandika nikiwa kwenye bus from Mtwara to Dar
 
Mkuu Pascal Mayalla, hii kitu ina sura kadhaa ila kwangu mimi naona ina sura mbili. Kwanza niseme tu kuwa Mh. rais si dictator hata kidogo. As you said in your post, hii nchi ilipinda sana katika rushwa, ubadhilifu, na ujinga kibao ambao mpaka watanzania millennials walihisi ndiyo hali halisi ya nchi. As you know, HAKUNA nchi duniani iliyoendelea kiubabaishaji, I mean kama ilivyokuwa Tanzania before Magufuli, never.....! Udikteta una namna mbili nionavyo mimi: Kwanza kuna ule udikteta wa kuteka mawazo ya wananchi, yaani unawadanganya ili waamini uwongo wako na wewe ufanye yako bila kuingiliwa kama walivyofanya mkapa na Kikwete. Pili kuna ule udikteta wa Nyerere, mtu unaogopewa for nothing, yaani unaweka watu roho juu bila hata sababu na hakuna cha maana unachofanya katika nchi.

Hii nchi (Tanzania) ilibidi itawaliwe kwa umakini na itawaliwe na mtu anayeogopa Mungu like Magufuli.....uzuri ni kwamba hata yeye Magufuli anajuwa kuwa hii nchi ilichezewa na kuibiwa sana na watanzania wachache ila yeye alishindwa kufanya kitu pengine aliogopa kutumbuliwa uwaziri na aliyekuwa bosi wake, Kikwete. Hata wewe Pascal na watanzania wenye akili timamu wanajuwa kuwa Kikwete HAKUWA rais mzuri na ni mtu aliyendekeza ujinga hapa Tanzania. Alileta ujinga wa TAKUKURU kuja kuzuia rushwa, what happened then? TAKUKURU yake ndiyo ikawa inaongoza kwa rushwa. Binafsi nilishawahi kumwandika Kikwete barua na kuwataja baadhi ya viongozi wake wa TAKUKURU wala rushwa, sikupata jibu lolote. Huenda watu wake hawakumpa hiyo barua, nahisi. Kuhusu suala la madini yetu kuibiwa, Kikwete na Mkapa wote walikuwa wanajuwa ila walipiga madili kujinufaisha wao na familia zao bila kujali wananchi wao huku wakiwadanganya eti hiii nchi ni ya kimasikini, seriously? Hawa ni viongozi makini kweli?

Magufuli ilibidi atawale hii nchi and I know kwa mtanzania mwenye uchungu na nchi yake LAZIMA atakubaliana nami kuwa Tanzania tulimuhitaji mtu kama Magufuli kuja kututawala. Kutawala nchi iliyooza kwa rushwa, ubadhilifu, ubabaishaji, na ujinga uliotukuka usio na kipimo, ni LAZIMA rais anyooshe vile vilivyopinda. Kunyoosha huku pia kunaweza kutafsiriwa kama vita vya kiuchumi for baadhi ya wanaominywa (wezi wa mali ya umma na wababaishaji pamoja na wasiojitambua). Hata wewe Pascal kama kweli una uchungu na nchi yako ukaja kuwa rais wa nchii ungefanya kama haya anayofanya Magufuli ambayo ni kuthibiti ama kunyoosha vile vilivyopinda, na kama utafanya haya kwa kutetea maslahi ya wananchi wako, huu ni udikteta? Akili mukichwa....nasepaaaaa!
 
Hakuna Rais aliyekuwa anaogopwa Tanzania kama Mwl Nyerere.

Kama sifa ya udikteta ni kuogopwa basi Mwl. Nyerere alikuwa ni dikteta.

Kikubwa zaidi yeye aliamua hata kuondoa kwenye katiba kifungu kinachohusu haki za binadamu.

Yeye aliingia madarakani kwa njia ya vyama vingi lakini alipoapishwa akaamua kufuta vyama vingi lakini cha kushangaza zaidi, alipong'atuka kutokana na nchi kuelekea kufirisika, akaamua kuwalazimisha wengine waanzishe mfumo wa vyama vingi.

Ninakuhakikishia kama utawala wa Mwl. Nyerere ungekuwa ndio kwa sasa, hata hawa wanaosema Rais Mgufuli ni dikteta wasige thubutu hata kutamka maneno wanayotamka.

Huwa ninawashangaa sana watu wanajaribu kujenga hoja kuhusu haki za binadamu kwa kutumia kioo cha utawala,wa Mwl. Nyerete.

Kwa hiyo kama ni udikteta, basi tumwangalie Rais Magufuli kwa kutumia kioo cha matendo ya Mwl. Nyerere wakati akiwa Rais wa Tanzania na sio maneno yake.

Kwangu mimi sioni tofauti ya kuvunja katiba au kuibadilisha katiba na kuwa katika msingi wa udikteta.

Mwl. Nyerere alikuwa anaibadilisha katiba ili kuimarisha udikteta wake huku akidai ni kosa kuvunja katiba. Mwl. Nyerere hakuhitaji kuvunja katiba kwa sababu alikuwa na uwezo wa kuibadilisha apendavyo na wale waliomgomea walijikuta kwenye gereza au kuikimbia nchi.

Mfano mzuri kambona
Hahaha
Akawa anaimbwa mpaka michakamichaka ya mgambo
"Eti kambona kaolewa uko ulaya" dah
Aisee kazi kweli eti kisa katofautiana na mwl misimamo take
Mali za kambona zote zilitaifishwa na jamaa aliishi magumu mno
 
Duuuuu ambaye hajui, ni kiziwi na kipofu na babu na bibi yangu wa kule nyumba zetu za nyasi na pembeni na bango la hapa kazi tu
 
Mkuu Pascal Mayalla, hii kitu ina sura kadhaa ila kwangu mimi naona ina sura mbili. Kwanza niseme tu kuwa Mh. rais si dictator hata kidogo. As you said in your post, hii nchi ilipinda sana katika rushwa, ubadhilifu, na ujinga kibao ambao mpaka watanzania millennials walihisi ndiyo hali halisi ya nchi. As you know, HAKUNA nchi duniani iliyoendelea kiubabaishaji, I mean kama ilivyokuwa Tanzania before Magufuli, never.....! Udikteta una namna mbili nionavyo mimi: Kwanza kuna ule udikteta wa kuteka mawazo ya wananchi, yaani unawadanganya ili waamini uwongo wako na wewe ufanye yako bila kuingiliwa kama walivyofanya mkapa na Kikwete. Pili kuna ule udikteta wa Nyerere, mtu unaogopewa for nothing, yaani unaweka watu roho juu bila hata sababu na hakuna cha maana unachofanya katika nchi.

Hii nchi (Tanzania) ilibidi itawaliwe kwa umakini na itawaliwe na mtu anayeogopa Mungu like Magufuli.....uzuri ni kwamba hata yeye Magufuli anajuwa kuwa hii nchi ilichezewa na kuibiwa sana na watanzania wachache ila yeye alishindwa kufanya kitu pengine aliogopa kutumbuliwa uwaziri na aliyekuwa bosi wake, Kikwete. Hata wewe Pascal na watanzania wenye akili timamu wanajuwa kuwa Kikwete HAKUWA rais mzuri na ni mtu aliyendekeza ujinga hapa Tanzania. Alileta ujinga wa TAKUKURU kuja kuzuia rushwa, what happened then? TAKUKURU yake ndiyo ikawa inaongoza kwa rushwa. Binafsi nilishawahi kumwandika Kikwete barua na kuwataja baadhi ya viongozi wake wa TAKUKURU wala rushwa, sikupata jibu lolote. Huenda watu wake hawakumpa hiyo barua, nahisi. Kuhusu suala la madini yetu kuibiwa, Kikwete na Mkapa wote walikuwa wanajuwa ila walipiga madili kujinufaisha wao na familia zao bila kujali wananchi wao huku wakiwadanganya eti hiii nchi ni ya kimasikini, seriously? Hawa ni viongozi makini kweli?

Magufuli ilibidi atawale hii nchi and I know kwa mtanzania mwenye uchungu na nchi yake LAZIMA atakubaliana nami kuwa Tanzania tulimuhitaji mtu kama Magufuli kuja kututawala. Kutawala nchi iliyooza kwa rushwa, ubadhilifu, ubabaishaji, na ujinga uliotukuka usio na kipimo, ni LAZIMA rais anyooshe vile vilivyopinda. Kunyoosha huku pia kunaweza kutafsiriwa kama vita vya kiuchumi for baadhi ya wanaominywa (wezi wa mali ya umma na wababaishaji pamoja na wasiojitambua). Hata wewe Pascal kama kweli una uchungu na nchi yako ukaja kuwa rais wa nchii ungefanya kama haya anayofanya Magufuli ambayo ni kuthibiti ama kunyoosha vile vilivyopinda, na kama utafanya haya kwa kutetea maslahi ya wananchi wako, huu ni udikteta? Akili mukichwa....nasepaaaaa!

Umeeleza vizuri sana mkuu.
RAIS JPM aliletwa na Mungu tena kimiujiza saaana!
Maana walikuwepo waliokuwa wamejipanga saanaa.
Allah alituonea huruma tu.
 
Unaweza ukajenga madaraja na mi fly over kila kona lakini ukafeli kwenye kuwaunganisha wananchi kuwa kitu kimoja.Unaweza kujenga madaraja barabarani na vilevile ukajenga madaaaja ya chuki katika jamii.Kiongozi mwenye busaraa hawezi kudili na misismamo yake binafsi bila kuangalia uelekeo wa Taifa kimahusiano LABDA KAMA NI DIKTETA.
Mkuu ni wananchi gani na wa wapi hao ambao walikuwa wameungana mwanzoni lakini Magu kawatenganisha?
 
Back
Top Bottom