Udhibiti wa uvushaji wa sukari na mazao mengine kagera. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Udhibiti wa uvushaji wa sukari na mazao mengine kagera.

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Kachocho T.K, Sep 26, 2011.

 1. K

  Kachocho T.K Member

  #1
  Sep 26, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  siku chache zilizopita waziri mkuu alisikika akiongelea suala la kupanda bei kwa sukari na mazao mengine kama mchele, mahindi na maharage kuwa sababu kubwa ni biashara ya magendo inayofanywa na wafanya biashara haramu, wanavusha biashara hii nje ya nchi. Waziri aliagiza jeshi la polisi kuhakikisha watu hawa wanadhibitiwa na ikibidi jeshi la wananchi liingilie kati. Mnavyojua wanajeshi wetu walivyo sharp kutekeleza agizo la wakubwa. Mkoani kagera kagera belia zimezagaa kila mahali hata kwenye njia za ng'ombe, wakitekeleza agizo la mkubwa. haiingii akilini kuona raia wa ndani wanakosa bidhaa hizi kwani hata mfanya biashara anayenunua kilo 50 za sukari kutoka Bukoba mjini akapeleka katoma km5 ili aweke kwenye duka lake na wananchi wa katoma wapate sukari karibu, lkn mfanya biashara huyo ananyanganywa kilo 50 kwa madai alikuwa anavusha sukari, sijui kwenda wapi kwani katoma si Tanzania? na je hawaoni kuwa hali hii itasababisha baadhi ya maeneo kukosa sukari kabisa? kwani wenye maduka huko vijijini wanazuiwa belia kupitisha sukari. mwisho agizo la waziri mkuu ilikuwa ni kudhibiti usafirishaji ndani au nje ya nchi. Na kama ni hivyo kwa nini belia hizi zisiwe mipakani ambapo bidhaa hizi zinavushiwa kwenda nje?.
   
 2. JamboJema

  JamboJema JF-Expert Member

  #2
  Sep 26, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,148
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Nimeliona hili. Nilishalilia hapa lakini wapi! Wanakagera, hasa wana - mtukula mwaka huu mnalo!
   
 3. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #3
  Sep 26, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,980
  Likes Received: 6,626
  Trophy Points: 280
  polisi watazuia kila mahali lakini hawana ujanja au mbinu za kuzuia bidhaa yoyote ya magendo isivuke pale rusumo mpakani kwenda Rwanda.kwa sababu polisi wetu wanaolinda mpakani mwa rwanda hawana ujuzi wa kuogelea.hiyo sukari inavushwa kwa kubeba viroba kichwani huku wakiogelea.halafu sehemu za kuvukia zipo nyingi.labda wapeleke boat na sijui itapitaje kwnywe yale mapolomoko ya rusumo.polisi wanawaonea bule coz hawana vitendea kazi labda hizo beria.mia
   
 4. d

  dotto JF-Expert Member

  #4
  Sep 26, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Sijajua nyuma ya hili Sakata kuna nini zaidi: Kwamba watumiaji wa Sukari Tanzania wameongezeka kwa ghafla au kuyumba kwa sarafu ya Tanzania? Pls wachumi mtujuze zaidi. Siamini kuwa Serikali inasema kupunguza bei na wakati huohuo inapanda bali lakini pia Sukari yenyewe haipo!. Naona tatizo kubwa limejificha zaidi kwa serikali. Kuna kitu inajua lakini kwa kuwa kuna dola basi nguvu nyingi inatumika badala ya kusolve mambo ya msingi kiurahisi. Exchange rate inakaribia Tzs.1700/$ je, hii haina effect? Tunazuia kuuza nje sukari je Exportation inafanyikaje ili ku curb Inflation?
   
 5. Alexism

  Alexism JF-Expert Member

  #5
  Sep 26, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 2,443
  Likes Received: 1,015
  Trophy Points: 280
  Hiyo yote nikuweka mianya ya rushwa si mkuu unakumbuka wakati wa asekido ilikuwa je.Wanakagera hasa bk vijijini,muleba,karagwe na misenyi poleni saana kwani hamna mtu wa kuwatetea mh mh mpola bojo! sasa mjifunze jinsi ya kuchagua hah.
   
 6. M

  Magenyi Nshekela Member

  #6
  Sep 27, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa mkoa kagera tuna bahati mbaya na uongozi.Viongozi wanaongoza mkoa huu mara nyingi ni wanajeshi kama tunavyojua wenzetu hawa utekeleza amri bila kutafakari.Operesheni zote zinazofanywa na nchi hii wanamkoa kagera uathirika tofauti na mikoa mingine.Na hii si leo tokea enzi za "uhujumu uchumi" Kuna matumizi mabaya ya busara katika kudhibiti uvushaji wa sukari.Angalia vizuizi haviko mipakani viko kilomita chache toka mijini.Belia iko katoma na iko Nyamugaba.Hizi za katoma na Nyamugaba niza nini?Hakuna mpaka katoma wala Nyamuga.Hii inasababisha kero kubwa kwa wananchi hasa wa MISSENYI na KARAGWE sisi tunaonekana tuko nje ya nchi.Si hizi maeneo haya hana sukari pamoja na kuwa na kiwanda cha sukari.WABUNGE wetu amka kumekucha.
   
Loading...