Udhibiti wa Ujenzi wa Miradi ya Maendeleo Katika Nchi ya Kufikirika (isiyokuwepo kiuhalisia)

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,214
3,587
Mheshimiwa Rais Chokambaya Bin Mwaminifu wa Jamhuri-ya-Mazuzu amefanya uamuzi mgumu kwa nia ya kuokoa fedha za serikali yake katikati ya upinzani mkali wa wadau wa sekta ya ukandarasi. Katika kikao cha Baraza la Mawaziri, alitangaza uamuzi wake huo kama ifuatavyo:-

Ili kudhibiti matumizi ya rasilimali-fedha za serikali na kuwapa wananchi fursa ya kufuatilia mienendo ya miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye maeneo yao; kama namna ya kudhihirisha nguzo za dhana ya Utawala Bora za uwazi na uwajibikaji hususan kwenye eneo la matumizi ya rasilimali-fedha, serikali sasa ama itarekebisha au itatengeneza sheria au kanuni itakayomlazimisha mkandarasi wa mradi wa maendeleo kuandika thamani ya pesa ya mradi, muda wa mradi na hatua iliyofikiwa (Project Phase) kwenye ama jiwe la msingi la uzinduzi wa ujenzi wa mradi au kwenye bango la ujenzi/ukandarasi (Project Billboard) inayosimikwa kwenye sehemu ya wazi kuelezea aina ya mradi, wakandarasi na mnufaika. Aidha, thamani ya mradi itaandikwa kwa lugha-rafiki (rahisi) na kwa maneno na tarakimu vinavyosomeka kwa wazi (human legible). Hii itaondoa ubabaishaji wa wakandarasi wanapotosha hesabu za miradi ya maendeleo kwenye ziara za viongozi na kwenye mikutano ya hadhara inayofanywa na viongozi hao, lakini pia sheria hiyo au kanuni hiyo itawapa wananchi (walipa kodi ambao ndiyo wanufaikaji wa miradi) mamlaka ya kuhoji utekelezaji wa miradi husika ama kama mtu mmoja mmoja au kama kundi. Sambamba na hilo, Mheshimiwa Rais Chokambaya Bin Mwaminifu wa Jamhuri-ya-Mazuzu ameamuru mabango yote ya miradi kwenye safu ya chini ya bango yaandikwe maneno yafuatayo:

MottoFight Corona Pandemic by Vaccination
Akisisitiza kwamba ujumbe wa Ukimwi umefika na unazingatiwa kwa mafanikio, sasa tugeukie Corona.

Mfano wa bango-pendekezwa la mradi wa maendeleo (Proposed Project Billboard)

Proposed ProjectConstruction of Juakali Village Council Ultra-Modern Health Centre
Building Permit No0000019/21
Project SiteWalalahoi Street, Plot No. 159, Block C
ClientCounty Director – Hustlers’ County Council
Financier/DonourWasotaji Investments Group
Project Monetary ValueTzs.900,200,000.00 (Tzs. Nine hundred million and two hundred thousand only)
Project TimeframeNine calender months, August 2021 – May 2022
Main ContractorCounty Engineer – Hustlers’ County Council
Architectural EngineerWachovu Civil Contractors
Quantity SurveyorWababaishaji Survey Enterprises
Project PhasePhase Two
Sub Contractors:
Building EngineerWapigaji Structural Works Company
Electrical EngineerTen–Percent Electrical Installation Company
PlumberWafujaji Plumbing Works
LandscapingWakwapuaji Landscapers and Gardeners
MottoFight Corona Pandemic by Vaccination

Kisa na Douglas Majwala.
 
Back
Top Bottom