Udharura wa kuyatoa mabasi ya mwendokasi 200 yalikwama bandarini.

mbenge

JF-Expert Member
May 15, 2019
4,560
9,791
Nakubaliana kabisa na rai iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuhusu kuondolewa kwa urasimu ktk masuala ya kikodi, na hatimaye mabasi ya mwendokasi yapatayo 200 yaruhusiwe kufanya biashara ili kukabiliana na gonjwa la COVID-19 na sharti la kiusalama la afya la "social distance" na kile kinachoitwa "level seat" ktk usafiri wa mabasi ya umma.

Aidha nashauri watu binafsi wenye magari ambayo yanaweza kusafirisha watu kwa mfano Alphard, Noah na mengine kama hayo yaruhusiwe kutoa huduma mbadala ktk kipindi hiki cha ugumu wa usafiri wa umma ambacho tunakipitia, hasa kwa wale wenye vipato visikuwa na uhakika.

Mwisho, nawaombeni wale wenye kumiliki magari binafsi, msiache kutoa msaada kwa wamama wajawazito, wazee na watoto ambao tutawaona wakikabiliwa na matatizo na adha za sasa za usafiri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom