Udhamini wa TBL kwa Simba na Yanga unauwa soka ya Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Udhamini wa TBL kwa Simba na Yanga unauwa soka ya Tanzania

Discussion in 'Sports' started by Sajenti, May 1, 2009.

 1. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #1
  May 1, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Wakuu heshima mbele. Nimekuwa nikifatilia kwa ukaribu sana jinsi gani makampuni mbali mbali yanavyojitokeza kudhamini timu kubwa mbili za soka Tanzania yaani Simba na Yanga. Si jambo baya ingawa kwa mtazamo wangu naona linazidi kuporomosha kiwango cha ubora wa soka ya nchi hii. Nasema hivyo kwa kuamini kuwa Simba na Yanga ni kama mamba walioko kwenye mapitio ya wanyama wengine kwenye mto wanasubiri kudaka wachezaji wazuri wanaowaona. Na timu hizi kwa uzoefu wangu ndio huwa kaburi la kuzika vipaji vya wachezaji wengi walioibuka kutoka timu ndogo za wilayani au mikoani na mwisho wake hutupiwa virago.(Mfano Simba...Emmanuel Gabriel, Itutu Kigi, Michael Paul, Dani Mhoja na wengine wengi au Yanga Nico Bambaga, nk.) Kwa maoni yangu haya makampuni yasijifunge kudhamini hizi timu kubwa angalau wapanue wigo hata katika timu zilizoko mikoani ambazo nina imani nyingi hazina uwezo wa kujiendesha kutokana na ukata kuliko kujaza mapesa na misaada kwa Simba na Yanga kwani hizi timu kwa sasa hazina utamaduni wa kutengenza wachezaji vinginevyo tutakuwa tunadumaza vipaji vya wachezaji walioko katika timu ndogo au mwisho kuziimarisha Simba na Yanga ili ziendelee kuvutia wachezaji kwenda huko na mwishoe wachezaji kuishia kupoteza vipaji vyao.....

  Mkuu Invisible unasemaje najua wewe Simba kufa mtu lakini haya ndio maoni yangu...Naomba kuwasilisha.
   
Loading...