Udhamini Kagame Cup: No TBL | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Udhamini Kagame Cup: No TBL

Discussion in 'Sports' started by Pdidy, May 23, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  May 23, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,449
  Likes Received: 5,700
  Trophy Points: 280
  Vicky Kimaro

  KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) imejitoa katika udhamini wake wa michuano ya Kombe la Kagame litakalofanyika Uganda mwezi ujao kutokana na mashindano hayo kufanyika nje ya ardhi ya Tanzania.

  Kauli hiyo ya TBL ni pigo kwa Katibu Mkuu Mkuu wa Baraza la Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), Nicholaus Musonye ambaye amekuwa akiota kupata udhamini wa kampuni hiyo kwenye michuano ya mwaka huu.

  Meneja Masoko wa TBL, David Minja alisema kampuni yake imeshawaeleza wazi Cecafa kuwa haipo tayari kudhamini michuano hiyo ikiwa inafanyika nje ya Tanzania kwa kuwa kampuni yake haitapata kipaumbele chochote kibiashara.

  "Sisi hatuwezi kudhamini wakati hatutafaidika na chochote, lengo letu ni kujitangaza sasa ikifanyika huko hatuwezi kujitangaza na tulishamweleza Musonye wazi msimamo wetu hauwezi kubadilika,"alisema.

  TBL walitoa masharti kwa Cecafa kuwa iwapo wanahitaji udhamini huo ufanyike, michuano hiyo haina budi ifanyike
  nchini na Yanga ambayo imefungiwa na Cecafa kwa miaka mitatu iruhusiwe kushiriki michuano hiyo.

  Hata hivyo, Musonye amekuwa akieleza kuwa baraza lake linasubiri maombi yao kwa TBL ingawa michuano hiyo wamepanga ifanyike Kampala, Uganda.

  Mapema wiki hii viongozi wa juu wa Cecafa walikutana mjini Nairobi, Kenya kupanga mikakati ya michuano hiyo ikiwa ni pamoja na suala zima la udhamini.

  Hata hivyo, msimamo wa kikao hicho ulifikia kwa michuano hiyo ifanyike Kampala huku Musonye akipewa jukumu la kufuatilia kwa karibu maombi yao kwa TBL.

  Timu zinazotarajiwa kushiriki michuano hiyo ni pamoja na mwalikwa, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), El Merreikh, El- Hilal (Sudan) ambazo zimeingizwa baada ya kujitoa kwa Eritrea na Djibouti.

  Nyingine ni Tusker, Mathare (Kenya), SC Villa na KCC (Uganda), Miembeni (Zanzibar), Atraco (Rwanda), Inter Club (Burundi), mwakilishi wa Somalia na Prisons (Tanzania).

  Simba, imekuwa ikipigiwa debe na Musonye kama mwakilishi wa Tanzania, ingawa kanuni zinamtaja mshindi wa pili wa msimu uliopita.
   
Loading...