Wengi wamegeuza jambo hili kama la Rais dhini ya CDM. Wengi, hata waliomsifu JK kwa kukutana na CDM, sasa wanailaumu CDM na kusema kuwa JK kapata ushindi. Katika hali ya ukweli, CDM na Rais wameshinda na walioshindwa ni sisi wananchi wa kawaida.
CDM imefanikiwa kumwonesha sio Makinda tu, bali hata Rais ni nini kiliwafanya watoke Bungeni. Hata walipokutana nae waliyasema mapungufu yale yale waliyoyataje Bungeni. JK kawaonesha kuwa alichowaahidi wazee wa Dar es Salaam nimetimia licha ya "kelele za wapinzani" ambao kufanya nao mazungumzo hakukuwa na maana yoyote.
Niliandika katika post jana kuwa JK amedhalilisha Urais kama taasisi. Ikiwa Rais anakubaliana na mtu kuboresha muswada na siku moja baadae anausaini katika hali ile ile ya mwanzo, anajionesha ni muongo, mnafiki na mtu asiyeweza kuaminiwa. Bahati mbaya anayoyafanya anadhani ni sahihi kama mtu, anasahau ni taasisi ya Urais ndiyo inaharibiwa.
Haiwezekani tayari JK amekwishaboresha muswada, siku moja baada ya mazungumzo. Na sasa ni sheria na hawezi kuibadilisha sheria, labda ifutwe na kuna taratibu zake pia. JK amelikosesha taifa hili njia ya kumaliza mambo kwa kujadiliana. Akiona sasa njia nyingine zinatumika, asilalamike!! Ametumia mamlaka yake kama Rais na sasa aache wengine watumie mamlaka yao. Na mamlaka hizo zimeainishwa katika Katiba hii ya sasa. Anaendeza utaratibu wa kuamua mambo ya kitaifa kwa mtazamo wa kiCCM.
Ndio maana hata ufisadi unaoliathiri taifa, unaachwa kuendelea au hauadhibiwi kwa sababu CCM itaumizwa!! Akiwa mwenyekiti wa CCM anaona wajibu wa kwanza ni kwa CCM na kwa taifa ni jambo la pili. Binafsi sitapenda kuona chama chochote cha siasa kinapewa umuhimu kuliko maswala ya kitaifa yanayoathiri maisha ya watu wengi wawe ni wanachama au si wanachama wa chama kilicho madarakani. Bila shaka, udhaifu au wa serikali ya CCM au chama hicho, unamwathiri kila mtu isipokuwa viongozi wakuu wa serikali hii na CCM.
JK amelikosea taifa hili kuliko hata Makinda, CCM na CDM!! Yeye ndiye alikuwa na mamlaka ya mwisho au kuleta matatizo au kuyamaliza! Bila shaka ataishi kuona uzuri au ubaya wa maamuzi yake. Nadhani atakuwa tayari kupokea zao lolote la uamuzi wake!!
Huenda sasa ni zamu ya wananchi kusikilizwa!!