ACT Wazalendo
JF-Expert Member
- May 5, 2014
- 607
- 1,540
TUNALAANI VITENDO VYA UDHALILISHAJI KIJINSIA VILIVYOFANYWA NA POLISI HANDENI, TANGA.
Ngome ya Wanawake ya ACT Wazalendo imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya baadhi ya Askari wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga kutuhumiwa kuwafanyia vitendo vya udhalilishaji kijinsia wanawake wilayani humo.
Udhalilishaji huo umebainika kufuatia kikao cha hadhara cha Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Siriel Mchembe na Wananchi wa Wilaya hiyo katika kusikiliza kero na malalamiko mbalimbali.
Ngome ya Wanawake ACT Wazalendo kwa kuzingatia kuwa matendo ya udhalilishaji wa kijinsia yaliyotolewa na Wananchi wa Handeni na kura ya Siri kuwataja askari hao ni uthibitisho tosha kuwa askari wa jesho la Polisi wilayani humo wanahusika katika matendo ya udhalilishaji Wanawake kijinsia.
Ngome ya Wanawake ACT Wazalendo inamtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini kuwawajibisha haraka iwezekanavyo askari wote waliotajwa kwenye kura ya wananchi kuhusika na matendo ya udhalilishaji kijinsia dhidi ya Wanawake Wilayani Handeni Mkoani Tanga.
Jeshi la Polisi kwa mujibu wa sheria ndio linapaswa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha matendo yote ya udhalilishaji wa kijinsia dhidi ya Wanawake yanakomeshwa na wote wanaobainika kuhusika na kutenda matendo hayo wanakamatwa na kufikishwa mbele ya sheria ili ifuate mkondo wake kwa kutoa adhabu dhidi yao.
Ni jambo la aibu na lenye kulichafua jeshi la Polisi kwa baadhi ya Askari wake kutajwa kuwa vinara wa vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia dhidi ya Wanawake.
Ngome ya Wanawake ACT Wazalendo inawapongeza Wanawake wa Handeni kwa ujasiri waliouonesha kwa kusimama hadharani na kueleza matendo ya udhalilishaji yanayofanywa dhidi yao tena na wasimamizi wa sheria ambao kimsingi ndio wanaopaswa kuhakikisha wanalindwa dhidi ya matendo hayo.
Vile vile ngome ya wanawake taifa tunaliomba jeshi la polisi kupima akili za askari wake kabla ya kuwaajiri na wafuate taratibu za kipolisi. Polisi wanawake wapo kwa nini polisi wa kiume washughulike na jinsia ya kike? Vitendo hivyo havikubaliki.
Imetolewa na:
Husna Sungura,
Naibu Katibu, Habari, Uenezi na Mawasiliano.
Ngome ya Wanawake,
ACT Wazalendo
03 Septemba, 2021