Udhaifu wa wabunge; hawaelewi kutafsiri Bajeti kwa kuandikwa Kiswahili cha kitaalamu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Udhaifu wa wabunge; hawaelewi kutafsiri Bajeti kwa kuandikwa Kiswahili cha kitaalamu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Mar 1, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 1, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=2]01 MARCH 2012[/h][h=3][/h]

  Salim Nyomolelo na Grace Ndossa
  WAKATI wabunge wengi wakishinikiza kuongezewa posho kutoka sh. 70,000 hadi 200,000, imebainika kuwa baadhi yao hawaelewi kutafsiri lugha ya bajeti ya Serikali, kwa kuandikwa kwa kiswahili cha kitaalam.

  Akizungumza katika kipindi cha mahojiano cha dakika 45 kilichotangazwa na Televisheni ya ITV juzi, Waziri wa Ofisi ya Rais na Utawala Bora, Bw. Mathias Chikawe, alisema kutokana na wabunge wengi kutoelewa lugha hiyo, itabidi iwekwe kwenye kiswahili rahisi.

  "Baadhi ya wabunge hawaielewi bajeti, hivyo itakuwa vigumu kwa mwananchi wa kawaida kuielewa," alisema Bw.Chikawe na kuongeza kuwa kutokana na hali hiyo wabunge wanashindwa kusaidia wananchi kuielewa.

  Alisisitiza kuwa wananchi wanatakiwa kujua bajeti ya nchi yao, lakini kutokana na lugha ambayo inatumika kuiandika ni vigumu wao kuielewa kwa sababu baadhi ya wabunge hawaielewi lugha inayotumika kuiandaa.

  Katika hatua nyingine Bw. Chikawe alikiri kuwa fedha nyingi zinazotengwa kwa ajili ya miradi mbalimbali ya halmashauri nchini, zinapotea bila ya kuwafikia walengwa, hali inayochangiwa na mchakato mrefu wa kuzifikisha kwa walengwa.

  Kutokana na hali hiyo alisema Serikali imekuwa ikipoteza fedha nyingi kwenye halmashauri nchini hivyo kusababisha miradi iliyopangiwa kukwama.

  Alisema asilimia 75 ya bajeti hupolekwa katika halmashauri nchini, hasa katika sekta ya elimu ambapo mafanikio ya utekelezaji wa miradi hayaonekani badala yake fedha hizo zinaliwa na wajanja wachache.

  "Kuna mianya mingi ya upotevu wa fedha hapa katikati bila ya kuwafikia walengwa na hatujui zinafanya kazi gani,"alisema Bw.Chikawe

  Alisema wanashangazwa na matokeo ya kidato cha nne kuendelea kuwa mabaya zaidi, wakati halmashauri zinatengewa fedha nyingi kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu msingi na sekondari.

  Akizungumzia kuhusu mikakati ya iliyowekwa ili kudhibiti hali hiyo, Bw.Chikawe alisema wameanzisha mfumo mpya wa utawala bora, ambapo utawashirikisha wananchi kupata taarifa za miradi mbalimbali pamoja na bajeti itakayotengwa ili waweze kufuatilia na kutoa taarifa pale, ambapo utekelezaji hautofanyika.

  Alisema mifumo ya uwazi itasaidia zaidi kuwapa wananchi taarifa, ambapo wanatakiwa kujua na kushirikishwa katika kila mchakato wa maendeleo ili waweze kutoa taarifa pale ambapo mambo hayatakwenda sawa.

  Akizungumzia suala la uwajibikaji alisema kuna mchakato wa kupewa ahadi hewa ambapo unapewa muda wa kujibiwa bila ya utekelezaji wowote kufanyika.

  "Unaomba fedha hazina unaambiwa usubiri baada ya siku saba utapewa lakini siku hizo zinapita hakuna utekelezaji wowote,"alisema   
 2. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #2
  Mar 1, 2012
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  so??? PELEKA KWA ZITTO ALETE HOJA BINAFSI BUNGENI HAPA HAIHUSIANI
   
 3. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #3
  Mar 1, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Sasa hawa Wabunge wetu wanaelewa Lugha gani? Kiingereza taabu, Kiswahili sanifu taabu - ila posho hata ukiiweka kwa number za kirusi wanajua ni hatari kushibisha tumbo kama halishibi.
   
 4. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #4
  Mar 1, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Una Maana Gani? Acha Chuki !!!
   
 5. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #5
  Mar 1, 2012
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  HUMJUI ZITTO WEWE?/KINARA WA HOJA BINAFSI,MPELEKEE NA HII ALETE BUNGENi AKISHIRIKIANA NA JANUARI MAKAMBA NA HAMISI KIGWAGWALA ITANOGA SANA
   
 6. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #6
  Mar 1, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Yeye Ni Mwanachama hapa ataiona na ataifikisha Bungeni kama kawaida yake...
   
 7. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #7
  Mar 1, 2012
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  MPELEKEE KAMA VIPI ATAKUPENDA SaNA
   
 8. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #8
  Mar 1, 2012
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  wewe unaelewa ipi??
   
 9. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #9
  Mar 1, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Kuna haja ya kuangalia kigezo cha elimu katika nafasi za ubunge na udiwani. Sifa ya kujua kusoma na kuandika kiswahili ama kiingereza ni kigezo kilichopitwa na wakati katika dunia ya leo.
   
 10. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #10
  Mar 1, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  Orientation course pleaseee
   
 11. kakakuona40

  kakakuona40 JF-Expert Member

  #11
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 300
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  We bungeni kuna wasanii wa kizazi kipya, waimba taarabu! wao na kingereza cha kitaalamu wapi na wapi?
   
 12. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #12
  Mar 1, 2012
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0


  heeeeeeeeeee we chizi kweli unadharau wabunge kiasi hiki??hukawii kumdharau mama yako wewe,4444%%%%%$$$$
   
 13. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #13
  Mar 1, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Umeniona kwenye Ubunge? Sina haja ya kuelewa Lugha yoyote sina tamaa ya Uongozi ndani ya Serikali ya Tanganyika
   
Loading...