Udhaifu wa vyombo vya habari tanzania na uandishi na yaliyotokea kwenye operesheni tokomeza

2 PAC

Member
Apr 27, 2012
67
35
Ni ukweli usiopingika kuwa vyombo vya habari na waandishi wake havikufanya kazi kuweza kusaidia na kufichua mateso waliyoyapata wenzetu, namaanisha watanzania wenzetu.Laiti vyombo hivi vingekuwa vinafanya kazi yao kama inavyopaswa basi leo hii taifa letu na uongozi uliopo madarakani usingepata kadhia hii na pengine taifa lingekuwa kwenye sura nzuri. Mimi binafsi huwa nachukulia vyombo vya habari kama kioo na kiranja wa yanayotokea katika nchi.
Ni ukweli usiopingika kuwa watu wengi wamefahamu nini kilichokuwa kinaendelea kwenye operesheni tokomeza baada ya repoti ya tume kwa watanzania na ni nini kilitokea mpaka taifa likafika hapo.
Kiukweli hii inatishia sana amani ya nchi , pengine uhuru wa vyombo vyetu vya habari upo tuu kuandika ama kutangaza mambo yasiyo ya msingi ama tija kwa taifa letu
Narudia tena huu ni udhaifu mkubwa kwa tasnia ya habari nchini na inadidi kulichukua jamabo hili kwa uzito wake na kujipanga upya.
Pengine taifa lina mambo mengi yanayotukwamisha na yenye uvunjifu mkubwa wa haki za bainadamu hayafuatiliwi na kuandikwa ili kuweza kukemewa kwa pamoja kama taifa.
AMANI YA NCHI YETU INATUNZWA NA SISI WENYEWE NA SI TAIFA JINGINE, KUSHINDWA KWETU SISI BASI NI KUSHINDWA KWA TAIFA NA SISI WENYEWE
Naamini wachambuzi wa kina wa mambo ya taifa hili watanielewa kwa urahisi.
 
Umeniwahi Mpwa. Yaani wanaripoti habari za kifeisubuku tu, hazina mashiko kabisa, wananunulika kama pipi, ni wala rushwa wakubwa. Ngoja nitaaandaaa makala dhidi ya hawa wachumia tumbo. Wao wanaripoti mambo ya Nyepesi na ndugu zake Mwigulu. Wanasubiri Press Conference na bahasha. @sd@a@sfv#&&*$€¥*+~
 
Hii aibu nimeivumilia kwa siku kadhaa hasa kushindwa kupata muda wa kuandika hapa kutokana na majukumu mengine , binafsi sipo tasnia ya habari bali mimi kama mlaji wa habari nimesikitishwa kusikia habari nyeti kupitia bunge, namaanisha kupitia wanasiasa, na ukiona mwanasiasa anakwambia ukweli basi ujue mambo yameharibika zaidi ya ukweli wa mwanasiasa huyo.

Hili nalitangaza kama pigo kuu kwa tasnia ya habari, walikuwa wamekufa wakafufuka kuandika kuwa mawaziri wamasimamishwa kazi kwenye hizo media, je hayo kwa sasa yanatija kwa watanzania wenzetu waliopoteza maisha.????
Walioachwa vilema kwa mambo yaliyoweza kukemewa???

Zaidi watanzania walioonewa hawakuwa na upeo mkubwa wa elimu na matumizi mazuri ya mitandao

aibu aibu aibu kwa waandishi na media tanzania

sipendi kuaminishwa na nape na kinana kuwa wao ndio waliofichua haya
 
Ni ukweli usiopingika kuwa vyombo vya habari na waandishi wake havikufanya kazi kuweza kusaidia na kufichua mateso waliyoyapata wenzetu, namaanisha watanzania wenzetu.Laiti vyombo hivi vingekuwa vinafanya kazi yao kama inavyopaswa basi leo hii taifa letu na uongozi uliopo madarakani usingepata kadhia hii na pengine taifa lingekuwa kwenye sura nzuri. Mimi binafsi huwa nachukulia vyombo vya habari kama kioo na kiranja wa yanayotokea katika nchi.
Ni ukweli usiopingika kuwa watu wengi wamefahamu nini kilichokuwa kinaendelea kwenye operesheni tokomeza baada ya repoti ya tume kwa watanzania na ni nini kilitokea mpaka taifa likafika hapo.
Kiukweli hii inatishia sana amani ya nchi , pengine uhuru wa vyombo vyetu vya habari upo tuu kuandika ama kutangaza mambo yasiyo ya msingi ama tija kwa taifa letu
Narudia tena huu ni udhaifu mkubwa kwa tasnia ya habari nchini na inadidi kulichukua jamabo hili kwa uzito wake na kujipanga upya.
Pengine taifa lina mambo mengi yanayotukwamisha na yenye uvunjifu mkubwa wa haki za bainadamu hayafuatiliwi na kuandikwa ili kuweza kukemewa kwa pamoja kama taifa.
AMANI YA NCHI YETU INATUNZWA NA SISI WENYEWE NA SI TAIFA JINGINE, KUSHINDWA KWETU SISI BASI NI KUSHINDWA KWA TAIFA NA SISI WENYEWE
Naamini wachambuzi wa kina wa mambo ya taifa hili watanielewa kwa urahisi.

Tanzania hakuna waandishi wa habari.... ni ma-zuzu majic machumia tumbo
 
Mkuu uko sahihi kupita kiasi. Walivyokomaa na press conference za Zitto na masalia wenzie utadhani hakukuwa na issues nyingine nzito nchini.

Wakati mwingine unajiuliza, hivi Zitto kusimamishwa nyadhifa zake ndani ya Chadema au wananchi kuuwawa, kubakwa, kuzinishwa na miti, kujeruhiwa, kunyanyaswa, kuporwa mali zao, na kudhalilishwa kwa kila namna na wenye mamlaka waliotokana na CCM kwa kushirikiana na majeshi yetu yenye dhamana ya ulinzi na uhai wa watanzania ni ipi habari nzito zaidi?

Kwa ufupi hatuna vyombo vya habari zaidi ya wachumia tumbo na mamluki wa kisiasa wasio na mwelekeo wowote.

Juzi, Mh. Mtutura Abdallah Mtutura wakati akichangia Bungeni alitoa statement ambayo kimsingi ni ya ukweli na ndivyo baadhi ya vyombo vyetu vinavyofanya kazi. Alidai kwamba, baada ya yeye (Mtutura) kuibua kadhia ile, aliandikwa vibaya na baadhi ya vyombo vya habari vikimhusisha na ujangili. Nikifikiria aina ya habari zinazoandikwa na magazeti kama Jambo Leo, Habari Leo (la Serikali!), Tazama Tanzania, n.k. napatwa na mashaka hivi vyombo viko kwa interest ya nani.
 
Tasinia hii ya habari imechafuka sana kwa kuendekeza rushwa(bahasha) yaani habari hata iwe na umuhimu kiasi gani kama haina bahasha hakuna anayeifuatilia. Ila waambie kuna press conference Serena na bahasha za kutosha basi mpaka mhariri mwenyewe anataka kwenda.
Tusipoangalia baada ya muda mfupi watu makini watajisikia aibu kujitambulisha kuwa ni waandishi wa habari hadharani.
 
baadhi ya waandishi wa tz ni waganga njaa tu wanaweza kuja kukutishia eti tuna habari zako mbaya kama vipi ili utoe chochote yaani wanakera.sasa matukio ya mauaji wakanyamazia nduu hadi kamati inaibua.shame on you makanjanja
 
Tatizo ni la tasinia ya habari Tanzania ni RUSHWA. Waandishi kwa tamaa ya maisha ya juu wanaandika habari zinazolipa kwao tu. mimi mwenzenu nimeacha kununua magazeti na kuziamini habari hadi nipige simu kuulizia chanzo cha habari. Acheni njaa waandishi wa Tanzania. andikeni habari za uchunguzi.
 
Wandishi wetu kanjanja! Wamejikita wote kwenye habari za siasa tu mara utasikia pimbi x amlimpua pimbi y,mara utasikia pimbi x aiteka kahama,pimbi z aiteka songea! Mara pimbi z hakamatiki! Mara utasikia pimbi f njia nyeupe ikulu.........hovyo kabisa wana acha kuripoti mambo mhumu ya jamii yetu
 
Tusiwalaumu sana, maana tatizo ni mfumo wenyewe, maana wangeandika wangeambiwa ni wachochezi na kufungiwa siku 90, maana ndio kazi akina nchimbi wanayifahamu

Ni ukweli usiopingika kuwa vyombo vya habari na waandishi wake havikufanya kazi kuweza kusaidia na kufichua mateso waliyoyapata wenzetu, namaanisha watanzania wenzetu.Laiti vyombo hivi vingekuwa vinafanya kazi yao kama inavyopaswa basi leo hii taifa letu na uongozi uliopo madarakani usingepata kadhia hii na pengine taifa lingekuwa kwenye sura nzuri. Mimi binafsi huwa nachukulia vyombo vya habari kama kioo na kiranja wa yanayotokea katika nchi.
Ni ukweli usiopingika kuwa watu wengi wamefahamu nini kilichokuwa kinaendelea kwenye operesheni tokomeza baada ya repoti ya tume kwa watanzania na ni nini kilitokea mpaka taifa likafika hapo.
Kiukweli hii inatishia sana amani ya nchi , pengine uhuru wa vyombo vyetu vya habari upo tuu kuandika ama kutangaza mambo yasiyo ya msingi ama tija kwa taifa letu
Narudia tena huu ni udhaifu mkubwa kwa tasnia ya habari nchini na inadidi kulichukua jamabo hili kwa uzito wake na kujipanga upya.
Pengine taifa lina mambo mengi yanayotukwamisha na yenye uvunjifu mkubwa wa haki za bainadamu hayafuatiliwi na kuandikwa ili kuweza kukemewa kwa pamoja kama taifa.
AMANI YA NCHI YETU INATUNZWA NA SISI WENYEWE NA SI TAIFA JINGINE, KUSHINDWA KWETU SISI BASI NI KUSHINDWA KWA TAIFA NA SISI WENYEWE
Naamini wachambuzi wa kina wa mambo ya taifa hili watanielewa kwa urahisi.
 
Wandishi wetu wana andika ujinga kama huu "Dk. Slaa azidi kuchanja mbuga;atoa maagizo nchi nzima
'waraka' wa uasi"
 
There is no independence of media in Tanzania. wanasubiri wapigiwe simu kutoka magogoni, Lumumba, Kinondoni mtaa wa Ufipa au kwenye ofisi za wizara siku waziri akiwa na press conference. Wengine wanavizia kuingizwa kwenye list ya msafara wa rais au waziri, wengine wanasubiri patokee ajali au sherehe au msiba wa wanamuziki ndo wakaripoti.
 
Tz waandishi wengi ni makanjanja tu. wao usubili kwanza wapewe hela ndo watoe habari flani. Tunao waandishi wachache kama si hakuna kabisa wataalamu wa fani hiyo. Jiulize mwandishi anasomea hii kozi ili aandike habari zipi?

Kuna habari za kisiasa, kijamii, kiuchumi, burudani, elimu,sheri nk, hapa kwetu siyo shida kumkuta mtu mmoja anaandika habari kutoka nyanja zote hizi alafu anajiita mtaalamu wa kuandika habari. Tasnia hii bado sana ndo maana matukio kama haya hawajuhi kama ni jukumu lao

Ni ukweli usiopingika kuwa vyombo vya habari na waandishi wake havikufanya kazi kuweza kusaidia na kufichua mateso waliyoyapata wenzetu, namaanisha watanzania wenzetu.Laiti vyombo hivi vingekuwa vinafanya kazi yao kama inavyopaswa basi leo hii taifa letu na uongozi uliopo madarakani usingepata kadhia hii na pengine taifa lingekuwa kwenye sura nzuri. Mimi binafsi huwa nachukulia vyombo vya habari kama kioo na kiranja wa yanayotokea katika nchi.
Ni ukweli usiopingika kuwa watu wengi wamefahamu nini kilichokuwa kinaendelea kwenye operesheni tokomeza baada ya repoti ya tume kwa watanzania na ni nini kilitokea mpaka taifa likafika hapo.
Kiukweli hii inatishia sana amani ya nchi , pengine uhuru wa vyombo vyetu vya habari upo tuu kuandika ama kutangaza mambo yasiyo ya msingi ama tija kwa taifa letu
Narudia tena huu ni udhaifu mkubwa kwa tasnia ya habari nchini na inadidi kulichukua jamabo hili kwa uzito wake na kujipanga upya.
Pengine taifa lina mambo mengi yanayotukwamisha na yenye uvunjifu mkubwa wa haki za bainadamu hayafuatiliwi na kuandikwa ili kuweza kukemewa kwa pamoja kama taifa.
AMANI YA NCHI YETU INATUNZWA NA SISI WENYEWE NA SI TAIFA JINGINE, KUSHINDWA KWETU SISI BASI NI KUSHINDWA KWA TAIFA NA SISI WENYEWE
Naamini wachambuzi wa kina wa mambo ya taifa hili watanielewa kwa urahisi.
 
kuna kitu kinaitwa work boundary au territory so waandishi wa habari na vyombo vya habari hawatakiwi kutoa maana taifa la weza kudumbukia kwenye umwgaji damu.sisi 2natakiwa kulaumu watendaji wakuu wa serikali
 
Waandishi wenyewe ndo kama hao wa Clouds Fm unategemea nini? Kila saa ni Facebook na tweeter na kurudiarudia maneno. Unategemea kupata habari makini au kuuliza kiongozi yeyote maswali magumu? Never
 
Ni ukweli usiopingika kuwa vyombo vya habari na waandishi wake havikufanya kazi kuweza kusaidia na kufichua mateso waliyoyapata wenzetu, namaanisha watanzania wenzetu.Laiti vyombo hivi vingekuwa vinafanya kazi yao kama inavyopaswa basi leo hii taifa letu na uongozi uliopo madarakani usingepata kadhia hii na pengine taifa lingekuwa kwenye sura nzuri. Mimi binafsi huwa nachukulia vyombo vya habari kama kioo na kiranja wa yanayotokea katika nchi.
Ni ukweli usiopingika kuwa watu wengi wamefahamu nini kilichokuwa kinaendelea kwenye operesheni tokomeza baada ya repoti ya tume kwa watanzania na ni nini kilitokea mpaka taifa likafika hapo.
Kiukweli hii inatishia sana amani ya nchi , pengine uhuru wa vyombo vyetu vya habari upo tuu kuandika ama kutangaza mambo yasiyo ya msingi ama tija kwa taifa letu
Narudia tena huu ni udhaifu mkubwa kwa tasnia ya habari nchini na inadidi kulichukua jamabo hili kwa uzito wake na kujipanga upya.
Pengine taifa lina mambo mengi yanayotukwamisha na yenye uvunjifu mkubwa wa haki za bainadamu hayafuatiliwi na kuandikwa ili kuweza kukemewa kwa pamoja kama taifa.
AMANI YA NCHI YETU INATUNZWA NA SISI WENYEWE NA SI TAIFA JINGINE, KUSHINDWA KWETU SISI BASI NI KUSHINDWA KWA TAIFA NA SISI WENYEWE
Naamini wachambuzi wa kina wa mambo ya taifa hili watanielewa kwa urahisi.

katika taifa ambalo wandishi wanauliwa kwa kulipuliwa na mabomu wakiwa kazini, katika taifa ambalo waandishi wananyofolewa macho. binadamu ameumbwa na hofu.
 
Back
Top Bottom