Ni ukweli usiopingika kuwa vyombo vya habari na waandishi wake havikufanya kazi kuweza kusaidia na kufichua mateso waliyoyapata wenzetu, namaanisha watanzania wenzetu.Laiti vyombo hivi vingekuwa vinafanya kazi yao kama inavyopaswa basi leo hii taifa letu na uongozi uliopo madarakani usingepata kadhia hii na pengine taifa lingekuwa kwenye sura nzuri. Mimi binafsi huwa nachukulia vyombo vya habari kama kioo na kiranja wa yanayotokea katika nchi.
Ni ukweli usiopingika kuwa watu wengi wamefahamu nini kilichokuwa kinaendelea kwenye operesheni tokomeza baada ya repoti ya tume kwa watanzania na ni nini kilitokea mpaka taifa likafika hapo.
Kiukweli hii inatishia sana amani ya nchi , pengine uhuru wa vyombo vyetu vya habari upo tuu kuandika ama kutangaza mambo yasiyo ya msingi ama tija kwa taifa letu
Narudia tena huu ni udhaifu mkubwa kwa tasnia ya habari nchini na inadidi kulichukua jamabo hili kwa uzito wake na kujipanga upya.
Pengine taifa lina mambo mengi yanayotukwamisha na yenye uvunjifu mkubwa wa haki za bainadamu hayafuatiliwi na kuandikwa ili kuweza kukemewa kwa pamoja kama taifa.
AMANI YA NCHI YETU INATUNZWA NA SISI WENYEWE NA SI TAIFA JINGINE, KUSHINDWA KWETU SISI BASI NI KUSHINDWA KWA TAIFA NA SISI WENYEWE
Naamini wachambuzi wa kina wa mambo ya taifa hili watanielewa kwa urahisi.