Udhaifu wa Viongozi Wetu Katika Kutoa Takwimu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Udhaifu wa Viongozi Wetu Katika Kutoa Takwimu.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Job K, May 26, 2011.

 1. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #1
  May 26, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,884
  Likes Received: 2,833
  Trophy Points: 280
  Takwimu hizi za Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi zimekaaje? Ng'ombe 600,000 wanakamuliwa na wanazalisha lita 110,000 kwa Siku. Haiingii akilini kabisa hivi ng'ombe nao wamekuwa mbuzi wa kienyeji? Maana hata kama watatoa 1/2 lita maanake ni lita 300,000 kwa siku sasa wapi na wapi Mh. Mathayo?

  ‘Maziwa yanazalishwa kwa tekolojia finyu Send to a friend Wednesday, 25 May 2011 21:29 0diggsdigg

  [​IMG] Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk David Mathayo

  Nora Damian
  SERIKALI imesema kuwa Tanzania inazalisha lita 1.65 bilioni za maziwa kwa mwaka huku maziwa mengi yakizalishwa kwa teknolojia ya kizamani.

  Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk David Mathayo alipokuwa akifungua mkutano na maonyesho ya wadau wa Sekta ya Maziwa Kusini mwa Afrika(ESADA).

  Alisema ng'ombe 600,000 kati ya 21 milioni walioko nchini wanazalisha maziwa na kwamba kila siku zinazalishwa lita 110,000.

  Alisema bado uzalishaji ni mdogo ukilinganisha na nchi nyingine kama Kenya ambao wanazalisha zaidi ya lita 1,000,000 milioni kila siku na Uganda wanazalisha lita 500,000.

  "Uchache huu ndio umesababisha tushindwe kuuza maziwa nje ya nchi na kupata fedha za kigeni,"alisema Dk Mathayo.

  Alisema unywaji wa maziwa nchini pia uko chini na kufafanua kwamba mtu mmoja anakunywa lita 40 kwa mwaka tofauti na viwango vilivyowekwa na Shirika la Chakula Duniani(FAO).

  Kwa mujibu wa waziri huyo, viwango vya FAO vinataka kila mtu anywe maziwa lita 200 kwa mwaka.

  Waziri huyo wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, alisema sekta ya maziwa nchini inachangia asilimia 1.30 ya pato la taifa na kwamba inategemewa kukuza ajira,uchumi na chakula.

  Dk Mathayo aliwataka Watanzania kuhamasiska zaidi katika kuzalisha na kunywa maziwa kwa wingi.

  Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB), Charles Mutagabwa alisema uzalishaji maziwa ya kutosha nchini ni tatizo na kwamba viwanda vya kusindika nchini hulazimika kwenda umbali mrefu kutafuta maziwa.

  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa ESADA, Alnoor Hussein alisema mkutano huo wa saba ni wa kwanza kufanyika nchini na umeshirikisha watu 200 kutoka nchi mbalimbali duniani.

  Baadhi ya nchi hizo ni Uganda, Mauritius, Rwanda, Malawi, Zambia, Kenya, Sudan, Zimbabwe, Afrika Kusini na mwenyeji Tanzania
   
Loading...