Udhaifu wa TCU kusimamia elimu sasa kila mtu anajipa cheti cha PhD

robinson crusoe

JF-Expert Member
Oct 22, 2020
740
1,214
Jana, leo, watu wanajitangaza kupewa PhD. Bunge sasa limekuwa ni kama chuo cha kutafuta PhD. Yaonekana hata semina za ndani ya CCM hawapeani maonyo juu ya tabia mbaya.

Kubwa zaidi ni udhaifu wa TCU. Yaani TCU wapo kwa ajili ya kusimamia udahili wa wanafunzi wa vyuo vikuu tu! Hawasimamii taratibu zinazondoa heshima ya elimu ya juu kama vitenbdo hivi vya wabunge.

Hawa wanaojitangaza kupewa PhD ni wazazi je, watoto wao wanaona kuna sababu yoyote ya kusoma PhD? Maana baba zao hawakusoma hata cheti, lakini wanapewa PhD. Bahati mbaya kizazi cha wanasiasa ndio hicho tena kinaingizwa katika siasa kwa mbinu zote.

Baba ni mwizi, ana Phd ya mchongo na mtoto amekuwa akiona hayo. Ndio maana tunaona watoto wa wansiasa walioko katika siasa, hakuna mtu wa maana zaidi ya kubebwa.
 
Jana leo, kesho watu wanajitangaza kupewa PhD. Bunge sasa limekuwa ni kama chuo cha kutafuta PhD. Yaonekana hata semina za ndani ya CCM hawapeani maonyo juu ya tabia mbaya. Kubwa zaidi ni udhaifu wa TCU. Yaani TCU wapo kwa ajili ya kusimamia udahili wa wanafunzi wa vyuo vikuu tu! Hawasimamii taratibu zinazondoa heshima ya elimu ya juu kama vitenbdo hivi vya wabunge.

Hawa wanaojitangaza kupewa PhD ni wazazi je, watoto wao wanaona kuna sababu yoyote ya kusoma PhD? Maana baba zao hawakusoma hata cheti, lakini wanapewa PhD. Bahati mbaya kizazi cha wanasiasa ndo hicho tena kinaingizwa ktk siasa kwa mbinu zote. Baba ni mwizi, ana Phd ya mchongo na mtoto amekuwa akiona hayo. Ndo maana tunaona watoto wa wansiasa walioko ktk siasa, hakuna mtu wa maana zaidi ya kubebwa.

Tatizo ni wananchi wanapo chukulia PhD kama ni kitu cha ajabu ni ushamba wetu tu. PhD ndugu zangu ni utafiti tu hii haina uhusiano wowote na uongozi wowote! Mfano Magufuli alipata PhD ya kwenye kemikali za korosho lakini hata hiyo hiyo korosho biashara ilimshinda mpaka Bashe ndiye anarekebisha vitu tena baada ya miaka! Sasa sembuse uongozi wa nchi!

Serikali isipoteze muda kwa mambo ya kijinga kama haya.
 
Tatizo ni wananchi wanapo chukulia PHD kama ni kitu cha ajabu ni ushamba wetu tu. PHD ndugu zangu ni utafiti tu hii haina uhusiano wowote na uongozi wowote! Mfano Magufuli alipata PHD ya kwenye kemikali za korosho lakini hata hiyo hiyo korosho biashara ilimshinda mpaka Bashe ndiye anarekebisha vitu tena baada ya miaka! Sasa sembuse uongozi wa nchi!

Serikali isipoteze muda kwa mambo ya kijinga kama haya.
Hiyo PHD uliyoandika ndiyo nini mkuu?
 
Walizopewa zinaitwa honorary causa,, "sio sawa na Ph.D,, they are just bunch of honorary degree ambazo ukipata mkwanja na ww utaipata tu,, mwenye hyo honorary causa hawezi kuwa lecturer unless awe na PhD
 
Sioni tatizo katika hilo.as long as real PHDs zinatakiwa kujipambanua kwa matokeo,otherways nazo ni maembe kama hao wengine.
 
Kwaiyo babutale hiyo masters kapewa kutoka chuo gani? Pia na msukuma na Mama suluhu ? Hawa wote walifeli lasaba leo wanawapa udokta

Hizi PhD ni za heshima hazina uhusiano na masters hata high school. Kisheria waliompa wapo sawa ni sisi tu tunachukulia hizo PhD kwa ukubwa ambao haustahili
 
Tatizo ni wananchi wanapo chukulia PhD kama ni kitu cha ajabu ni ushamba wetu tu. PhD ndugu zangu ni utafiti tu hii haina uhusiano wowote na uongozi wowote! Mfano Magufuli alipata PhD ya kwenye kemikali za korosho lakini hata hiyo hiyo korosho biashara ilimshinda mpaka Bashe ndiye anarekebisha vitu tena baada ya miaka! Sasa sembuse uongozi wa nchi!

Serikali isipoteze muda kwa mambo ya kijinga kama haya.
We mbona huna huo utafiti?
 
Ilimshindaje ikiwa mlimua kabla ya kumaliza muda wake wa uongozi?,wewe na mama yako wapumbavu kwerikweri
 
Wala suala la PhD za heshima au za kusomea zisitupigize kelele. Mwenye PHD ya heshima manake kaheshimika. Mwenye ya kusomea atuonyeshe tija ya PhD yake. Mbona simpo tu?
 
Kwa heshima ipi Sasa ya Dr Tale

Kawaulize chuo sio mitandao. Kuna watu wengi wanapewa PhD za hivi na hakuna mtu wala sheria yeyote inaweza kuwazuia kutoa PhD ya heshima wewe kina kuuma kipi. Tatizo unathaminisha sana hizo PhD
 
Kawaulize chuo sio mitandao. Kuna watu wengi wanapewa PhD za hivi na hakuna mtu wala sheria yeyote inaweza kuwazuia kutoa PhD ya heshima wewe kina kuuma kipi. Tatizo unathaminisha sana hizo PhD

Swali sio kupewa, swali unapewa kwa lipi? Hizo wananua tu wala hamna la maana. Nafahamu watu wengi Sana walio nunua hizo PhD.
 
Mbona zipo zinauzwa, nipe dollar elfu 10 nikufanyie mpango, TCU achana nao elimu ya juu imewashinda.
 
Katiba yetu unamfanya kila mkuu wa taasisi kuwa chawa wa rais. Kumbuka mkuu wa TCU anateuliwa na rais
 
Tatizo ni wananchi wanapo chukulia PhD kama ni kitu cha ajabu ni ushamba wetu tu. PhD ndugu zangu ni utafiti tu hii haina uhusiano wowote na uongozi wowote! Mfano Magufuli alipata PhD ya kwenye kemikali za korosho lakini hata hiyo hiyo korosho biashara ilimshinda mpaka Bashe ndiye anarekebisha vitu tena baada ya miaka! Sasa sembuse uongozi wa nchi!

Serikali isipoteze muda kwa mambo ya kijinga kama haya.
Bashe karekbisha nini? Magufuli qlinunua korosho kilo 3,000 sasa hivi kilo 1500, hapo nani alifanikiwa?
 
Back
Top Bottom