ideal safarimate
Member
- Mar 17, 2016
- 71
- 91
Naibu spika wa bunge la Tanzania mama Tulia Atson ni msomi mzuri na mbobezi wa sheria lakini tangu mchakato wake wa kugombea kiti hicho na kipindi uongozi wake katika bunge umeendelea kuzua maswali kuhusu uwezo wake wa kiuongozi hasa kuongoza chombo hicho muhimu chenye misuguano mingi ya kisiasa.
Hivi leo katika suala la wanafunzi wa ualimu UDOM bungeni na uamuzi wake wa kupinga hoja ya kua na mjadala wa dharura anazidi kuacha maswali mengi:
-Je alishindwa kuona udharura wa suala la wanafunzi kufukuzwa na kupewa masaa 24 tu wawe wametoka eneo la chuo?
-Je hakuona umuhimu wa kuibana serikali kutoa maelezo zaidi hasa ukizingatia suala la kuwalipa walimu halikua jukumu la wanafunzi hivyo kuwafukuza kwa ghafla kama ni wakosaji ni uonevu?
-Katika nafasi yake ya mwanasheria(mbobezi) hakuona kuna uvunjifu wa haki za kibinadamu kuwapa siku 1 wawe wameondoka bila kuzingatia hali ya malazi, chakula na nauli kwa kosa ambalo si lao?
-Je alijiridhisha kwamba serikali ilikua imetoa maelezo ya kina kuhusu utatuzi wa mgogoro huo,lini utaisha na wanafunzi kurudi chuoni?
Kwa muda wote wa uongozi wake ndani ya bunge ameonyesha udhaifu mkubwa wa kiuongozi na maamuzi yanayozua sintofahamu bungeni hivyo kuthibitisha hofu walikua nayo watu wengi tangu wakati za mchakato wa uchaguzi wake.
Ikumbukwe kua hapo kabla alikua naibu mwanasheria mkuu wa serikali(executive) akachukua fomu ya kugombea uspika na kushindwa kisha akachuka fomu ya unaibu spika na kuteuliwa ubunge na rais haraka haraka ili apate sifa ya kuwa mgombea huku wagombea wengine
"wakilazimishwa"wajitoe.
Hii yote ilitia hofu kwamba angeenda kuwa kibaraka wa serikali kudhibiti bunge ili lisiwe na meno na tukio la leo linazidi kudhihirisha hofu hiyo ilikua na msingi sana na kuathiri mfumo wa kibunge wa jumuiya ya madola tunautumia ambao bunge ndio chombo kikuu cha uwakilishi wa wananchi na kusimamia serikali.