jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 24,989
- 22,521
Wanajamvi,
Kumekuwepo na maneno kutoka kila pande za siasa! Maneno yenye kuzungumzia kauli aliyowahi kuitoa John Mnyika pamoja na Dr Slaa!
Sasa hayo maneno ambayo ni kama “tafsiri” zenye kuelezea au kudokeza, kuhusu udhaifu huo!
Spika wa Bunge Ndugai, amesema kuwa serikali ya sasa siyo dhaifu kwasababu kuna watu wako Segerea. Hapa naona spika mwenyewe pengine haelewi hata anachoongea! Kama anazungumzia kina Mbowe kuwepo segerea kwamba ndo kuonyesha uimara wa Maghufuli, basi hajaonyesha werevu wala weledi kwenye mambo yenye kuhitaji sifa hizo.
Kiukweli Mnyika alitaja jina kabisa! Hakusema “serikali ni dhaifu”! Pia tukumbuke kuwa serikali ina mihimili mitatu.
Kama anazungumzia kuwepo ndani kwa viongozi wa chadema kuwa ni uimara wa Maghufuli, basi hapo inaonyesha wazi kabisa kuwa hakuna uhuru kwenye mihimili!
Na ndiyo maana hakuna checks and balances! Hata yaliyotokea juzi dhidi ya CAG, yana akisi hilo la uelewa mdogo miongoni mwetu especially viongozi Mfano wa Ndugai!
Labda angesema “muhimili wa mahakama siyo dhaifu”!, Lakini alichokisema Mnyika? Siyo sawa na anachokisema huyu Spika!
Mambo yaliyokuwa yakitokea hadi JK kuitwa dhaifu na Mnyika pamoja na Dr Slaa, siyo kwasababu aliacha kuwafunga wapinzani, kuminya demokrasia nk. Ila ni kutokuwachukulia hatua wale ambao ni “wenye ccm”, na haya yalichagizwa na ile kauli ya Waziri Mkuu wa wakati ule Mizengo Kayanza Pinda, ambaye alisema wazi kabisa “kuna watu hawagusiki” na kwamba wakiguswa, “uchumi utayumba”, kiukweli, hilo ndilo lilikuwa msingi mkuu wa kuitwa dhaifu! Na siyo vinginevyo kama wengi wetu wanavyotaka kutuaminisha!
Watu wa ccm walitengeneza kitu kinaitwa “spin”, ambapo ni njia ya kuugaragaza ukweli na kupindisha maana halisi ili kuweza kukidhi haja ama mahitaji yao!
Wengine wanasema “JK aliwapa demokrasia mkamuita dhaifu”, kauli ambazo zinaonyesha kuwa hatuko serious hata kiodogo. Tuko kama zecomedy!
Kusema eti “JK aliwapa demokrasia”, maneno ya jingalao , inaonyesha jinsi ambavyo tuko kwenye “different paradigms” kwenye mustakabali wa Taifa hili, yani kumbe demokrasia wao wanachukulia kama ni privileged au kama favor flani hivi wanayotupatia, na wala siyo haki inayolindwa na katiba yetu! Katiba hiyo hiyo anayoitumia mkuu wa nchi kuapa!
Hadi usawa huu! Wale wa ccm wana mentality flani hivi kuona kwamba wapinzani ni kama favor tu wanapewa, mentality hii, ni mbaya sana, maana ni kama wengine wana haki milki ya nchi yetu na wengine wanategemea huruma zao! Haya yote kwa maoni yangu, yanasababishwa na katiba iliyopo.
Ni katiba hii hii, ambayo anaweza akaja rais akawa dhaifu ama akawa dikteta!
Sasa spika wa Bunge hajui hata maana halisi inayozungumziwa! Na ndiyo maana hata CAG aliposema Bunge ni dhaifu, yeye akakimbilia mambo ya polisi na pingu! Hapo utafahamu kuwa kichwani ni mtupu kabisa! Sijui hata hawa watu huwa wanafikaje kwenye hizo nafasi? Ama ndo udhaifu wenyewe huo?
Kwasababu bunge likiacha kuburuzwa kwasababu ya udhaifu na uelewa wa spika, hapo ndipo tutakuwa na taasisi ama mihimili imara! Kama mahakama inafuata matakwa ya rais, haina maana kwamba hakuna udhaifu. Hapo serikali ni dhaifu kwani muhimili wa mahakama unaburuzwa!
Wana ccm wengi, Maghufuli akiwa mmojawapo, walitafsiri udhaifu wa ccm kuwa ni pamoja na ku “leak” kwa zile kashfa Mfano EPA, KAGODA, MEREMETA, BUZWAGI, RICHMOND, Rada, mapanki nk, vyote kujulikana kwake, ndivyo walivyochukulia kuwa ni udhaifu.
Yani kuficha ufisadi Mfano ile trillion 1.5, ndo kuwa “strong “... Mfano angekuwa upande wa CAG, basi asingekuwa dhaifu kwa maoni yangu, zaidi ya hapo ni dhaifu kuliko JK!