Udhaifu wa Hoja za Mohammed Said katika Makala ya Uislamu na Siasa katika Tanzania

Mgambilwa ni mntu

JF-Expert Member
May 30, 2017
2,869
3,188
Kama Mkristo, naomba nitangaze wazi interest ili niweze kuhukumiwa vyema kwa mchango wangu katika kuijenga Tanzania tuitakayo. Wataalamu huwa wanasema uongo ukisemwa sana bila kukanushwa hubadilika na kuwa kweli. Yafuatayo ni Majibu dhidi ya Hoja za Saeed:
IMG_5010.jpg

Ni Ukanda upi Tanzania watu wamekuwa wakiongezeka nchini kwa kasi tangu Sensa ya 1957? Je, ni eneo gani nchini lina wapagani wengi?
Jibu: Mikoa iliyoongoza kwa ongezeko la watu kati ya 1957 - 2012, ni kama ifuatavyo:
1: Dar: 160,000 - 4,300,000.
2: Mwanza: 800,000 - 3,800,000.
3: Shinyanga: 700,000 - 3,500,000.
4: Arusha: 400,000 - 3,100,000.
5: Kagera: 510,000 - 2,800,000.
6: Mbeya: 600,000 - 2,700,000.
><
16: Ruvuma: 270,000 - 1,300,000.
17: Singida: 370,000 - 1,300,000.
18: Mtwara: 500,000 - 1,200,000.
19: Pwani: 360,000 - 1,100,000.
20: Lindi: 320,000 - 860,000.
Hapo mtaona ni Mikoa gani watu huongezeka sana.
Pia, ni vyema ijulikane kuwa, Uislamu unachanganya Dini na Utawala, so wananchi karibia wote (99%) wa Ukanda wa Pwani - Pwani, Dar, Lindi na Mtwara walikuwa Waislamu. Hivyo, usingetarajia kuwepo wapagani katika Mikoa hiyo wa kujiunga na uislamu kwa kuwa hawakuwepo. Hata katika Mikoa jirani ya Tanga, Morogoro na Ruvuma wapagani ni wachache kulinganisha na Mikoa mingine ya kikristo. Hivyo, ni wazi, wapagani wengi wamekuwa likely kujiunga na ukristo.
Swali: kama Wakoloni waliwaonea Waislamu na kuwabeba Wakristo, kwa nini walitoa takwimu zinazoonyesha Waislamu kuwa wengi kwenye Sensa za 1948 & 1957?

IMG_5011.jpg

Hapa unataka kuuambia umma kuwa, ni Waislamu waliopigana kwenye Maji Maji, Ndiyo maana Wakristo waliwasaidia Wajerumani? Ukisema baadhi ya Wakristo unaongelea waajiriwa ama wa kujitolea? Kama Waislamu ndio waliotaka kuwaondoa Wakoloni, mbona Vuguvugu la Kiislamu AMNUT ndilo lililotaka Tanganyika isipewe Uhuru 1961 eti mpaka tofauti ya kielimu kati ya Waislamu na Wakristo imalizwe? Je, hiyo haionyeshi kuwa waliona wenzao Wakristo kuwa ndio maadui kuliko Wakoloni?

IMG_5012.jpg

Wakristo walikuwa waajiliwa wa Wazungu, ungetegemea wafanyeje kipindi cha Inter-World Wars wakati pote Africa hakuna ambako Waafrika walifanikiwa kupata uhuru, zaidi ya Walowezi wa S. Rhodesia kupewa madaraka ya ndani na Uhuru wa Egypt in 1922? Mlitaka wafukuzwe kazi wawe kama ninyi mkafanye wote kazi za makuli? Baada ya Colonial Resistances kufeli vibaya Afrika nzima wananchi waligundua kuwa, mkoloni asingeondolewa nchini kwa mtutu wa bunduki bali kwa akili hivyo walianza kusomesha watoto wao kwenye shule za wamisionari. Suala la Wamisionari kuwakataza waumini wao kupinga ukoloni ni kitu cha kawaida coz Wazungu wenzao ndo waliokuwa watawala.

IMG_5014.jpg

Mwanzilishi wa TANU - Labda utuambie vinginevyo, historia inaonyesha Nyerere alichaguliwa kuwa Rais wa TAA kabla TANU haijaundwa na ni yeye aliyependekeza kubadilisha jina la TAA kuwa TANU. Alitaka jina la Chama liakisi Utaifa (Nationalism) kutoka jina lililoakisi Uafrika (Pan Africanism) ili kubadilisha mtazamo wa Chama kutoka Chama cha kutetea maslahi ya wafanyakazi hadi Chama cha kupigania uhuru kamili.
Dunia nzima, kiongozi aliyeleta uhuru ndiye anayefahamika na kukumbukwa. Hata ukienda SA, Msumbiji, Zimbabwe, Kenya, Ghana na kwingine, watu kama: Mandela, Machel, Mugabe, Kenyatta, Nkrumah ndio walioandikwa sana but walikuwepo viongozi muhimu na waliofanya mikubwa kwenye vita ya ukombozi kama: Oliver Thambo, Eduardo Mondlane, Joshua Nkomo, Tom Mboya na JB Danquah. Hata hivyo, bila kupepesa macho, kabla ya Nyerere, Viongozi waliokuwepo hawakuonyesha sifa za kiuongozi za kuweza kuliunganisha Taifa, ndo maana TAA haikuweza kuunganisha watu wa mijini na wa vijijini.

IMG_5027.jpg

Suala la kufeli ama kufaulu halihusiani kabisa na Sera za Serikali. Kama EAMWS ilidhohofishwa na Nyerere, kwani Mwinyi na Kikwete walifanya kitu gani ili kuwainua Waislamu kielimu? Shule za Kata zipo kila mahali lakini iko wazi kuwa, zinazofelisha zaidi zinatoka katika maeneo hayo hayo tu? Ama kupewa nafasi za upendeleo ndicho unachomaanisha? Mbona Kikwete hakuwajengea Vyuo vikuu ukiacha kilichojengwa na Mkristo huko Morogoro? Viongozi huwa wanajua wazi kuwa elimu inatolewa nchini bila ubaguzi wa mtu bali ni uwezo tu.

ISLAM AND POLITICS IN TANZANIA
 
Ahsante kwa Darasa lako..Ila twende taratibu wengine sie vichwa vya panzi..

Mi nafikiri ukiichukulia sensa kimkoa halafu ukaifanyia hitimisho kimkoa hasa katika suala la kujua ni upande upi wa dini una watu wengi zaidi, hutapata jibu linalokaribia usahihi kabisa.

Sababu:
Sensa huhesabu idadi ya watu waliolala sehemu fulani kwa siku fulani tu. hii haimaanishi hao watu ni wa eneo husika.

Mfano:
Naamini wakiamua sensa ifanyike tarehe 15 June. Bila shaka Dodoma kama haitaongoza basi itakua katika 3 bora kwa maana ndy kipindi Dodoma inakusanya waheshimiwa wote katika bunge la bajeti na ukizingatia sasa ofisi nyingi za serikali zimehamishiwa huko kwahiyo kutakua na watu wengi huko..
Hii haitamaanisha mkoa wa dodoma una wakristo/waislamu/wapagani kwa kua kiasili dodoma ni mkoa wa kikristo/kiislamu/kipagani.

Ushauri:
Kwa maoni yangu chukulia sensa kwa ujumla wake ki nchi halafu kama kama katika hiyo sensa kuna kipengele cha dini utapata jibu tu.

Pia unaweza fanya ka utafiti halisi kwa kuangalia katika level za kifamilia tu..oanisha familia kama 20 unazozijua kwa imani zote uangalie wastani wa uzazi. Nikimaanisha ni waumini gani wanazaa sana watoto..hapo utapata jibu.

Lakini pia usishangae na data za mwaka 1967 kwa kuamini zimepikwa..vipi kuhusu za awali hazikupikwa?..lakino je huo mporomoko wa asilimia unaakisi kweli?..kwa chanya au hasi?..

...
Tuyafanye haya tukiwa tumevua miwani ya kiimani..ama tuwevaa miwani iliyo "clear"..

Tafadhali.
 
Babu Kivu,
Ahsante sana kwa fikra zako.
Hakika hili suala ni gumu sana.
 
Kama Mkristo, naomba nitangaze wazi interest ili niweze kuhukumiwa vyema kwa mchango wangu katika kuijenga Tanzania tuitakayo. Wataalamu huwa wanasema uongo ukisemwa sana bila kukanushwa hubadilika na kuwa kweli. Yafuatayo ni Majibu dhidi ya Hoja za Saeed:
View attachment 808994
Ni Ukanda upi Tanzania watu wamekuwa wakiongezeka nchini kwa kasi tangu Sensa ya 1957? Je, ni eneo gani nchini lina wapagani wengi?
Jibu: Mikoa iliyoongoza kwa ongezeko la watu kati ya 1958 - 2012, ni kama ifuatavyo:
1: Dar: 160,000 - 4,300,000.
2: Mwanza: 800,000 - 3,800,000.
3: Shinyanga: 700,000 - 3,500,000.
4: Arusha: 400,000 - 3,100,000.
5: Kagera: 510,000 - 800,000.
6: Mbeya: 600,000 - 2,700,000.
><
16: Ruvuma: 270,000 - 1,300,000.
17: Singida: 370,000 - 1,300,000.
18: Mtwara: 500,000 - 1,200,000.
19: Pwani: 360,000 - 1,100,000.
20: Lindi: 320,000 - 860,000.
Hapo mtaona ni Mikoa gani watu huongezeka sana.
Pia, ni vyema ijulikane kuwa, Uislamu unachanganya Dini na Utawala, so wananchi karibia wote (99%) wa Ukanda wa Pwani - Pwani, Dar, Lindi na Mtwara walikuwa Waislamu. Hivyo, usingetarajia kuwepo wapagani katika Mikoa hiyo wa kujiunga na uislamu kwa kuwa hawakuwepo. Hata katika Mikoa jirani ya Tanga, Morogoro na Ruvuma wapagani ni wachache kulinganisha na Mikoa mingine ya kikristo. Hivyo, ni wazi, wapagani wengi wamekuwa likely jiunga na ukristo.
Swali: kama Wakoloni waliwaonea Waislamu na kuwabeba Wakristo, kwa nini walitoa takwimu zinazoonyesha Waislamu kuwa wengi kwenye Sensa za 1948 & 1957?

View attachment 808995
Hapa unataka kuuambia umma kuwa, ni Waislamu waliopigana kwenye Maji Maji, Ndiyo maana Wakristo waliwasaidia Wajerumani? Ukisema baadhi ya Wakristo unaongelea waajiriwa ama wa kujitolea? Kama Waislamu ndio waliotaka kuwaondoa Wakoloni, mbona Vuguvugu la Kiislamu AMNUT ndilo lililotaka Tanganyika isipewe Uhuru 1961 eti mpaka tofauti ya kielimu kati ya Waislamu na Wakristo imalizwe? Je, hiyo haionyeshi kuwa waliona wenzao Wakristo kuwa ndio maadui kuliko Wakoloni?

View attachment 808996
Wakristo walikuwa waajiliwa wa Wazungu, ungetegemea wafanyeje kipindi cha Inter-World Wars wakati pote Africa hakuna ambako Waafrika walifanikiwa kupata uhuru, zaidi ya Walowezi wa S. Rhodesia kupewa madaraka ya ndani na Uhuru wa Egypt in 1922? Mlitaka wafukuzwe kazi wawe kama ninyi mkafanye wote kazi za makuli? Baada ya Colonial Resistances kufeli vibaya Afrika nzima wananchi waligundua kuwa, mkoloni asingeondolewa nchini kwa mtutu wa bunduki bali kwa akili hivyo walianza kusomesha watoto wao kwenye shule za wamisionari. Suala la Wamisionari kuwakataza waumini wao kupinga ukoloni ni kitu cha kawaida coz Wazungu wenzao ndo waliokuwa watawala.

View attachment 808998
Mwanzilishi wa TANU - Labda utuambie vinginevyo, historia inaonyesha Nyerere alichaguliwa kuwa Rais wa TAA kabla TANU haijaundwa na ni yeye aliyependekeza kubadilisha jina la TAA kuwa TANU. Alitaka jina la Chama liakisi Utaifa (Nationalism) kutoka jina lililoakisi Uafrika (Pan Africanism) ili kubadilisha mtazamo wa Chama kutoka Chama cha kutetea maslahi ya wafanyakazi hadi Chama cha kupigania uhuru kamili.
Dunia nzima, kiongozi aliyeleta uhuru ndiye anayefahamika na kukumbukwa. Hata ukienda SA, Msumbiji, Zimbabwe, Kenya, Ghana na kwingine, watu kama: Mandela, Machel, Mugabe, Kenyatta, Nkrumah ndio walioandikwa sana but walikuwepo viongozi muhimu na waliofanya mikubwa kwenye vita ya ukombozi kama: Oliver Thambo, Eduardo Mondlane, Joshua Nkomo, Tom Mboya na JB Danquah. Hata hivyo, bila kupepesa macho, kabla ya Nyerere, Viongozi waliokuwepo hawakuonyesha sifa za kiuongozi za kuweza kuliunganisha Taifa, ndo maana TAA haikuweza kuunganisha watu wa mijini na wa vijijini.

View attachment 809001
Suala la kufeli ama kufaulu halihusiani kabisa na Sera za Serikali. Kama EAMWS ilidhohofishwa na Nyerere, kwani Mwinyi na Kikwete walifanya kitu gani ili kuwainua Waislamu kielimu? Shule za Kata zipo kila mahali lakini iko wazi kuwa, zinazofelisha zaidi zinatoka katika maeneo hayo hayo tu? Ama kupewa nafasi za upendeleo ndicho unachomaanisha? Mbona Kikwete hakuwajengea Vyuo vikuu ukiacha kilichojengwa na Mkristo huko Morogoro? Viongozi huwa wanajua wazi kuwa elimu inatolewa nchini bila ubaguzi wa mtu bali ni uwezo tu.

ISLAM AND POLITICS IN TANZANIA
Mgambilwa...
Hii ni mada nzito sana lakini hii paper ni ya zamani sana 1989.
Kwa ajili hii nimejadili na wengi na mwisho kila mtu akabaki kwake.
 
Ahsante kwa Darasa lako..Ila twende taratibu wengine sie vichwa vya panzi..

Mi nafikiri ukiichukulia sensa kimkoa halafu ukaifanyia hitimisho kimkoa hasa katika suala la kujua ni upande upi wa dini una watu wengi zaidi, hutapata jibu linalokaribia usahihi kabisa.

Sababu:
Sensa huhesabu idadi ya watu waliolala sehemu fulani kwa siku fulani tu. hii haimaanishi hao watu ni wa eneo husika.

Mfano:
Naamini wakiamua sensa ifanyike tarehe 15 June. Bila shaka Dodoma kama haitaongoza basi itakua katika 3 bora kwa maana ndy kipindi Dodoma inakusanya waheshimiwa wote katika bunge la bajeti na ukizingatia sasa ofisi nyingi za serikali zimehamishiwa huko kwahiyo kutakua na watu wengi huko..
Hii haitamaanisha mkoa wa dodoma una wakristo/waislamu/wapagani kwa kua kiasili dodoma ni mkoa wa kikristo/kiislamu/kipagani.

Ushauri:
Kwa maoni yangu chukulia sensa kwa ujumla wake ki nchi halafu kama kama katika hiyo sensa kuna kipengele cha dini utapata jibu tu.

Pia unaweza fanya ka utafiti halisi kwa kuangalia katika level za kifamilia tu..oanisha familia kama 20 unazozijua kwa imani zote uangalie wastani wa uzazi. Nikimaanisha ni waumini gani wanazaa sana watoto..hapo utapata jibu.

Lakini pia usishangae na data za mwaka 1967 kwa kuamini zimepikwa..vipi kuhusu za awali hazikupikwa?..lakino je huo mporomoko wa asilimia unaakisi kweli?..kwa chanya au hasi?..

...
Tuyafanye haya tukiwa tumevua miwani ya kiimani..ama tuwevaa miwani iliyo "clear"..

Tafadhali.
Kuna data huwa zinatolewa na Taasisi za mbalimbali za kimataifa juu ya masuala ya kiimani kama Pew Research Centre na Joshua Projects. Hizi ni Taasisi kubwa zinazoaminika kutoa takwimu sahihi kwa kiwango kikubwa. Hebu angalia hapa chini estimates Pew Research Centre kwenye idadi ya waislamu Tanzania.

IMG_0154.JPG

Linganisha hao Waislamu wa Tanzania milioni 13 dhidi ya Watanzania milioni 43 (2010). Angalia tena hilo ongezeko, inaonyesha kufikia 2030, waislamu watakuwa ni milioni 19. Kwa sasa tu Tanzania ina watu wapatao milioni 56, so kufikia 2030 watakuwa wangapi? Utaona kuwa, wastani wa waislamu nchini unazidi kupungua dhidi ya Wakristo kutokana na kuzaliana kupungua hasa Mikoa ya Ukanda wa Pwani.tg
Angalia kwenye Sensa ya Watu na Makazi 2012, uone ni Mikoa gani ambayo ina familia zenye uzazi (watoto) mkubwa. Mikoa hiyo ni:
1: Simiyu - 6.9
2: Geita - 6.1
3: Tabora - 6.0
4: Shinyanga - 5.9
5: Mwanza - 5.7
6: Kigoma - 5.7
><
19. Pwani 4.3
21: Iringa - 4.2
22: Njombe - 4.1
23: Dar - 4.0
24: Lindi - 3.8
25: Mtwara - 3.7
 
Attachments

  • IMG_0153.JPG
    IMG_0153.JPG
    167.9 KB · Views: 86
Mgambilwa...
Hii ni mada nzito sana lakini hii paper ni ya zamani sana 1989.
Kwa ajili hii nimejadili na wengi na mwisho kila mtu akabaki kwake.
Ok, angalizo zuri sana. Though ukweli unabaki wazi kuwa, andiko lako lilikuwa brilliant sana. Shida ni kwamba kuna mengi Nyerere aliyajua hakutaka kuyaweka wazi kwa ajili ya umoja wa kitaifa. Kwa kuwa, sisi ni kizazi kipya, ni vyema tuyajadili exhaustively ili tufanye informed decisions kama Taifa.
 
Angalia Mikoa ya Tanzania, uone ni wapi wana familia (households) kubwa.
IMG_5044.jpg

Ukiangalia Tanzania nzima kwenye Sensa ya Watu na Makazi, idadi ya Wilaya zenye familia (uzao) kubwa zaidi ya watu 5 na kuendelea ni Wilaya 53, kati hizo zenye Waislamu wengi (Muslim majority) ni tisa (09) pekee - Kilindi, Handeni, Kigoma, Uvinza, Uyui, Tabora, Kaliua, Urambo na Manyoni.
Wilaya za kikristo (Christian majority) ni arobaini na nne 44 - Longido, Karatu, Gairo, Nkasi, Sumbawanga, Nzega, Igunga, Iramba, Singida, Ikungi, Mkalama, Kasulu, Kakonko, Buhigwe, Shinyanga, Kishapu, Kahama, Biharamulo, Ukerewe, Magu, Kwimba, Sengerema, Misungwi, Tarime, Serengeti, Bunda, Musoma, Rorya, Butiama, Babati, Hanang, Mbulu, Mpanda, Mlele, Bariadi, Itilima, Meatu, Maswa, Busega, Geita, Nyang'hwale, Mbogwe, Bukombe na Chato.
 
Toka Sensa ya watu ya 1948, idadi ya watu imeongezeka kwa kila Mkoa kama ifuatavyo:
1: Dar es Salaam - X 53 (mara 53)
2: Rukwa - X 18
3: Arusha - X 10
4: Tabora - X 7
5: Mwanza - X 6
6: Shinyanga - X 6
7: Kigoma - X 6
8: Kagera - X 6
9: Mara - X 6
10: Mbeya - X 5
11: Ruvuma - X 5
12: Morogoro - X 4
13: Tanga - X 4
14: Dodoma - X 4
15: Kilimanjaro - X 4
16: Singida - X 4
17: Iringa - X 3
18: Mtwara - X 3
19: Pwani - X 3
20: Lindi - X 3.

Of course, ni wazi kuwa, Wakazi wengi wa Dar es Salaam, wametokea Mikoa ya Ukanda wa Pwani, hasa Mikoa ya Pwani, Morogoro na Lindi lakini bado ukweli unabakia kuwa, kuzaliana katika Mikoa ya Pwani ni kidogo kulinganisha na Mikoa ya Ndani.
 
Nimependa facts. Na niseme mpaka hapa uzi unajadiliwa kwa ustaraabu ingawa una habari sensitive
Thanx. Muhimu ni ustaarabu ulioonyeshwa na Mohammed Saeed coz yeye ndiye mwandishi. Wengi huwa hawapendi kusikia mitazamo ya wengine inayokinzana na ya kwao.
 
Nimependa facts. Na niseme mpaka hapa uzi unajadiliwa kwa ustaraabu ingawa una habari sensitive
James na ndugu zangu wote hapa Majlis,
Nakuwekeeni hapo chini msome uzoefu wangu katika somo hili:

Suala la takwimu nchi petu baina ya Waislam na Wakristo ni jambo nyeti sana na kwa hakika Afrika yote hili ni jambo linaloleta ubishani mkubwa sana.

Wakati naandika kitabu cha Abdul Sykes ilifika mahali lazima hili suala nilizungumze.

Naweka hapo chini kile nilichosema:

''According to the 1957 population census, Muslims outnumbered Christians at a ratio of three to two. This, at that time, meant that Tanzania was a leading Muslim nation South of the Sahara. But in the first post-independence census of 1967 the total figures for Tanzania Mainland were 32% Christian, 30% Muslim and 37% local belief (August H. Nimtz Jr, Islam and Politics in East Africa, University of Minneapolis, 1980, p.11). These figures show Pagans as a leading majority in Tanzania. The 1967 census has not been able to show the reasons for the sudden decrease of Muslim population nor the growth of animists amidst believers in the span of the last ten years.

This was the last population census showing religious distribution.

Unfortunately power sharing in the political system in Tanzania is very much skewed against Muslims, although it is known that the stability of any nation depends on proper balancing of these facts. Different sources provide different Muslim -Christian religious distribution figures. These conflicting figures are as a result of sensitivity of the issue. Among African countries with sizable population of Muslims and Christians, like Tanzania and Nigeria,[1] the inquiry as to which faith commands a leading majority, is a source of potential conflict and controversy. Tanzania is of no exception. D.B. Barret[2]gives figures which show Muslims as a minority in Tanzania. The Muslim population is purported to be 26%, Christian 45%, local belief 28%. Tanzania National Demographic Survey figures for 1973 put Muslims in Tanzania slightly above Christians at 40%, Christians 38.9% and local belief 21.1%. But according to Africa South of The Sahara, [3] Muslims in Tanzania are a leading majority at 60%. This figure has remained constant in all its publications since 1982. Since research by Tanzanian Muslims on Islam is scant or almost non-existent, the issue of Muslim population has yet to be tackled from an Islamic point of view. [4]

Distribution of authority and power sharing is a factor which should not have been a cause of conflict in independent African countries. Ironically this has become a point of controversy only under indigenous governments.

It is a sensitive issue because ethnicity, religious identity and clanship is an important factor in independent African states. Power distribution and numerical strength has also to be reflected in the sharing of political power along those lines.

During colonial rule, distribution of power under ethnicity and religious bias in Africa by colonising powers were not perceived as so serious a breach of trust by subjects as to warrant civil upheavals.

Fortunately tribalism is not pronounced in Tanzania, but religion has been a factor of discrimination since colonial days.''

[1] Ali A. Mazrui, ‘African Islam and Competitive Religion: Between Revivalism and Expansion’, in Third World Quarterly Vol. 10. No. 2 April, 1988, pp. 499-518.

[2] D.B.Barret, Frontier Situations for Evangelisation in Africa,Nairobi, 1976.

[3] Africa South of The Sahara, Europa Publication, London, No. 20, 1991, p. 1027.

[4]The only conclusive Muslim research is by Dar es Salaam University Muslim Trustee (DUMT), see 'The Position of Muslims and Islam in Tanzania', in Al Haq International (Karachi) September/October 1992.

Bahati mbaya nimeandika haya katika Kiingereza lakini tunaweza tukafanya mjadala kwa Kiswahili.

Katika hayo niliyoweka hapo juu nimefuta kipengele kimoja kinachosema kuwa takwimu za sensa ya mwisho iliyokuwa na kipengele cha dini ''zilichezewa.''

Nimekifuta makusudi kwa kuwa ingawa ipo ''citation,'' nina hakika kitasababisha mapambano makali hapa jamvini.

Sasa turudi latika hizi takwimu za CIA.

Nilikuwa nafanya mhadhara Chuo Kikuu Cha Iowa, Marekani kuhusu ''Uislam na Siasa Tanzania Historia ya TANU na Uhuru wa Tanganyika.''

Katika mhadhara ule nilieleza sababu za Waislam katika takriban miaka 20 iliyopita kuwa na maandamano na mapambano ya mara kwa mara na serikali.

Nikaeleza sababu kuu ni kuwa Waislam wamekuwa pembeni katika elimu na hivyo kuwa pembeni katika kugawana madaraka ya kuendesha nchi.

Waislam walitaka hili liangaliwe na serikali kwani ipo harufu ya hujuma.

Katika kipindi cha maswali na majibu na ilipobaki kama dakika tatu hivi nihitimishe, ndipo likaja swali hili lililokuwa na takwimu za CIA na muulizaji alikuwa profesa wa historia akasema kuwa wakipatacho Waislam wa Tanzania hiyo ndiyo haki yao kwa kuwa wao ni wachache, yaani ni ''minority.''

Hili swali naamini liliwekwa hadi mwisho kwa kuwa katika mazungumzo yale walitaabika sana ni historia ya uhuru niliyokuwa nawafunulia, historia ya wazalendo Waislam katika kupambana na ukoloni, historia ambayo kwao wao ilikuwa ngeni.

Wao walizoea mihadhara ya kuja na historia rasmi iliyomtaja Mwalimu Nyerere peke yake kuwa ndiyo aliyoikomboa Tanganyika kutoka kwa Waingereza.

Hawakutaka nitoke pale kichwa juu kifua mbele walitaka wanifedheheshe kwa hizi takwimu za CIA zinazonyesha kuwa Tanzania ina Waislam wachache na mambo yote ni shwari ila kwa vurugu hizi za, ''Waislam wa siasa kali.''

Historia yangu ilikuwa imewahuzunisha.

Katika hadhira ile alikuwapo Prof. James Giblin aliyafanya utafiti na kuandika kitabu

kuhusu Vita Vya Maji Maji.

Alikuwapo pia Prof. Michael Lofchie aliyeandika kitabu kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar, ''Revolution in Zanzibar,'' na hawa wote wameishi Tanzania na wanaijua vyema.

Jibu langu kwao halikuwa kwangu mimi kugonganisha takwimu zangu kama zilivyo katika kitabu cha Abdul Sykes, na takwimu zao za CIA, la hasha.

Mimi nilijibu swali lao kwa kuwauliza wao swali.

Niliwaambia kuwa naomba wanionyeshe nchi yoyote duniani katika historia yao wananchi walio pungufu yaani, ''minority,'' walionyanyuka na silaha mikononi kupambana na taifa lililoingia katika nchi yao kwa nia ya kuwatawala.

Nikawarejesha katika hitoria ya Vita Vya Maji Maji na kuwaambia wafanye rejea na waangalie ni nani waliunda majeshi ya kupambana na Wajerumani.

Nikawakumbusha kisa cha Sultani Abdulrauf Songea Mbano wa Wangoni alivyonyongwa na Wajerumani kwa kuongoza vita dhidi yao.

Nikawaambia wafanye tena rejea waangalie harakati za siasa za uhuru zilipoanza baada ya Vita Vya Pili Vya Dunia (1938 - 1945) ni nani walikuwa mstari wa mbele katika, ''nationalist politics,'' Tanganyika?

Kweli inawezekana adui aingie katika nchi bila ya ridhaa ya wenye nchi na ikawa walionyanyuka kupinga uvamizi huu wakawa ni wale, ''minority?''

''Majority,'' ya wenye nchi wako wako wapi hadi mapambano ya kuikomboa nchi iwe mikononi kwa ''minority,'' na katika Tanganyika iwe Waislamu?

Ukumbi wote ulikuwa kimya. Kama ungeangusha sindano ungesikia mlio wake.

Maprofesa wa historia ya Afrika walikuwa wanajaribu bila shaka kutafuta mfano utakaoweza kupambana na hoja yangu.

Hawakuweza kuupata.

Nchi zote duniani mapambano ya ukombozi huongozwa na wale waliokuwa, ''majority.''

Nikamaliza kwa kusema kuwa sina ugomvi na takwimu za CIA lakini Waislam wa Tanzania wanaujua ukweli.

Palepale Jonathon Glassman bingwa wa African History kutoka Northwestern University, Evanston Chicago akaniomba niende chuoni kwake tukafanye madahalo kama ule tuliofanya pale Universty of Iowa.

Glassman amekaa sana Pangani na Tanga mjini wakati anafanya utafiti wake na kaandika kitabu ''Feats and Riots,'' anaijua vizuri Tanzania.

Nilikubali mwaliko na nilizungumza Northwestern University, Ukumbi wa Eduardo Mondlane.

Lc_X5YAp92iCk3KksuJjQUeXBudAvnFxOmhuSi6zl3i2ey8c_ozCfdXiC5e2G6MvjPn56gSe_8mxsIQg4FUTRPo6w_KiDjhyYtuOb12Xr0ZgQDDCtrZgrQBAyZAKGBVeeVtD-UFT79oh8pSCzPWL0hVlsGCdI4AQlYZtWW6n-oqWiDA_fzzNYW5FRLiJgiXAvaWBywHch6rflr_yA1XoSSY-4o-3Av3qQ5Ylse0gQV3XH23eE9mf8Lfc4qBydBvGpUsDLpLvmiXuq6sJ7HKoL5eNmhz2gUe-a2bnJiMYrcHavaOcMLis_XKZrJjSNy3xWplPsVJXKXsrHGoqhxIaOdB0UNvYhyGdYc6HSxMPusSZ4Ndgv1-c1dWseCPzuu07jgwXrDUk_VqOjBGswQraj_b4pN1OGqb6nXaTkWKUQpIviZgTIEXejgeSzpFyzxzHZa2VEBkROIqNGEeK8Fh-b-0P_674ZtwhVrX9-JNWyNBwXkNxU9Q0pbyAa8dkHJlt9oAlmi8_mbJKazyFAxGSG9UT0nP9NiYANTjs_h23WMyE521RaLdzfxjQgVWdTSrS9lKAWS2KPZFNkNRPV71nLDGnVXC_pcF5YLdwpXvSoMjgqDamsfEbgdqRmmojtW3AiosJUqh4-zPKCdxYKfXjvC54tABp4P4nlQ=w412-h297-no
 
Thanx. Muhimu ni ustaarabu ulioonyeshwa na Mohammed Saeed coz yeye ndiye mwandishi. Wengi huwa hawapendi kusikia mitazamo ya wengine inayokinzana na ya kwao.
Mgambilwa...
Ikiwa huna moyo wa kuwasikiiza wengine daima utakuwa mtu wa kupungukiwa.
Kuna mengi mtu unajifunza kwa kuwasikiliza wengine.

Lakini kubwa nilisomeshwa ilm ya ''mnakasha'' yaani majadiliano na Sheikh Haruna
siku zote akisisitiza adabu na staha na akisema kuwa jadili kuelimisha au kuelimishwa
na sio kufanya kelele zisizokuwa na tija.
 
Kupata jibu sahihi zaidi mi naona ni kheri kipindi cha sensa wakarudisha kipengele cha dini..sioni ubaya wake. La sivyo kila mtu atavutia kwake..sababu ni ngumu kuamini katika hali ya kawaida kuwa waislamu watakua 19m ifikapo 2030.. Na ndy jamii ambayo mara nyingi tunaaminishwa kuwa inapenda "kuzaazaa" sana..

Na jamii inayopatikana sana maeneo ya pwani. Maeneo ambayo tukienda katika upande mwingine (nje ya mada) wa siasa tunaaminishwa ndy upande ambao chama cha siasa kikiweza kuuteka basi kitajihakikishia kushika dola sababu ni eneo kubwa lenye watu baada ya eneo linalohodhiwa na Wasukuma na Wanyamwezi..

Hapo tumezungumzia Tanzania Bara peke yake.
 
Back
Top Bottom