Udhaifu wa CCM kisiasa

MchunguZI

JF-Expert Member
Jun 14, 2008
4,012
2,180
Baada ya uchaguzi naanza kuona udhaifu wa CCM. Kama enzi zile za Mrema alipowapa taabu majimbo ya Kilimanjaro.

Sehemu zote ambako wameanguka sasa hawaoni kama ni uamuzi wa wapiga kura, bali wanaona ni uzembe wa viongozi wa chama hicho pamoja na wale wa serikali. Nahisi walitegemea kupewa ushindi bila kujali wapiga kura wanasemaje.

Kwa upande wa vyama vingine na hasa CHADEMA sasa wanawekewa mazingira magumu ya kupanga mipango ya halmashauri. Watendaji wa serikali wameanza eti kuogopa kufanya kazi na CHADEMA. Halmashauri nyingi na majiji ya Mwanza na Arusha ambako CHADEMA ilipeta, sasa wanapewa ushirikiano mdogo sana toka kwa watendaji wa serikali. Yaaminika ni kutokana na shinikizo toka serikalini kwamba wakwamishwe.

Hiyo ndo CCM ni bahati mbaya kwamba mwananchi ndiye ataumia na CHADEMA itakuwepo kwa miaka mitano ijayo. Lazima tusema CCM acheni kiwewe.
 
Back
Top Bottom