Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Dont'e get me wrong, silaumu Azimio la Arusha kwa Umasikini wa Mtanzania leo, bali nahoji jinsi lilivyopokewa na jinsi lilivyojieleza kama lilileta kitendawili machoni mwa Wananchi na Watekelezaji na katika kufumbua kitendawili, tukafumbua visivyo.
Nimekuelewa vizuri mchungaji; lakini hapo juu umeweka mojawapo ya very conditional statement ambayo inasema "kama Azimio la Arusha lisingepiga vita utajiri... basi tungekuwa.." Kimsingi unasema kuwa Azimio la Arusha ndio libebe lawama ya sisi kutokuendelea. Lakini vile vile uko sahihi kwenye jambo la uelewa wa Azimio na ndio maana nasema Azimio lilikuwa mbele sana ya muda wake.
Leo hii baadhi ya viongozi waliokuwa wakilitekeleza Azimio la Arusha ndio tunaanza kuwasikiliza jinsi wanavyojenga hoja na kutetea misimamo yao. Watu hawa leo hii wanapofungua makanwa yao tunaweza kuona ni jinsi gani hawana uwezo wa uchambuzi, uelewa na hata usimamizi wa jambo zito kama Azimio la Arusha.
Nakubaliana na wewe kabisa kuwa kulikuwa na uelewa potofu wa Azimio la Arusha kwa viongozi wengi lakini naamini si kwa sababu azimio lilikuwa gumu kueleweka bali watendaji walikuwa ni wagumu kuelewa kama wanavyojionesha leo hii.