Udhaifu wa Azimio la Arusha na Mapokeo Potofu kuhusu Utajiri na Vipato

... Kujilimbikizia mali kwa sababu ya kujipatia mamlaka au hadhi si mawazo ya Ujamaa.

....Katika nchi ya namna hiyo mali inawaharibu mioyo wale wanaoipata.

....Mali inawapa hamu ya kuishi kwa raha zaidi kuliko wenzao, kuvaa mavazi bora zaidi, na kuwazidi kwa kila njia.

....Wanaanza kutamani kupanda ngazi juu zaidi iwezekanavyo kuwashinda wenzao.

....Ili waifaidi mali yao, lazima tofauti baina ya starehe zao na shida za wenzao nchini zionekane: na hivyo basi huanza mashindano ya kutaka kutajirika – na jambo hilo ni kinyume cha Ujamaa.

Source? ... https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=44705&d=1325749616
 
Lilikuwa Azimio lenye utu ndani yake na uzalendo si haya maazimio uchwara yasiyo na tija tunayoyasikia kila leo.

Nadhani, hakuna Chama chochote kwa sasa kinachoweza kutekeleza haya yafuatayo, asa, ukitazama mienendo ya Viongozi wa vyama hivyo:

A. Viongozi
1. Kiongozi wa TANU au wa Serikali sharti awe mkulima au mfanya kazi, na asishiriki jambo lolote la Kibepari au Kikabaila.
2. Asiwe na hisa katika makampuni yo yote
3. Asiwe mkurugenzi katika kampuni ya kikabaila au kibepari
4. Asiwe na mishahara miwili au zaidi
5. Asiwe na nyumba ya kupangisha
6. Viongozi tunaofikiria hapa ni wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, mawaziri, wabunge, wakuu wa Vyama vilivyoshirikishwa na TANU, wakuu wa Mashirika ya Kiserikali, Viongozi kutokana na kifungu cho chote cha Katiba ya TANU, Madiwani, na watumishi wa Serikali wenye vyeo vya kati na vya juu. (Kwa mujibu wa kifungu hiki kiongozi ni mtu au mtu na mkewe au mke na mumewe)
 
Muasisi wa Azimio hilo pia alishatamka kua lilimshinda! R.I.P Mwalimu! ulikua na nia nzuri lakini kina Oscar Kambona na wenzake walilihujumu Azimio hilo.
Huu ni UONGO mchana kweupe! Kama una RaiaMwema ya jana kuna "quote" ya Mwalimu imo mle inakanusha uongo huu.
 
Mchanganuo wako unajipinga wenyewe na biblia unayoitoa kama reference huijui. Biblia inasomwa sio kama historia bali inatakiwa uwe na unyenyekevu, ungalie lugha iliyotumika na nyakati. Sasa wewe una uchungaji wako unaleta vifungu vya biblia unapachika ktk Azimio la Arusha na huku huna fact findings za kuback your arguments. Kizazi hiki kinahitaji researchable facts na sio utopia.

Tuambie mtoto aliyezaliwa miaka ya 90 na ndio wengi na wanasomeshwa somo la ujasiriamali Azimio la Arusha liliuawawa na Mwinyi linamhathirii namna gani? Tunayo raslimali watu (human resources) ambayo haitumiwi hapa na ndio maana makampuni ya kigeni yaliyoingia baada ya kuua Azomio la Arusha kwa kegezo cha foreign direct investments (FDIs) yanaleta watu wao kufanya kazi ambazo Watz tungefanya na tumebaki kuwa secretaries, technicians and officers but at decision making level ni wageni.Nini mchago wa Azimio la ARUSHA? Madini yetu mengine tumetoa bure na tunauziwa mfano Songas na gesi na madini tunaambulia royalty ya 3% huku makumpuni yakiwa hayalipi ushuru. Je, ni Azimio la Arusha? Litany is quite long na ndio maana unatakiwa kuchambua mambo huku ukuangalia na makandokando. Wazalishaji wadogo wa Tz hawana incentives, wanakamuliwa kwa njia ya kodi na ushuru na hawawezeshwi kwa vigezo wanavyowezeshwa wa nje. Sasa unategemea nini? Na faida inayokusanywa na TRA inaishia kwenye matumizi ya serikali mpaka bajeti ya mavazi na chai ya ikulu inazidi bajeti ya wizara 3 za Tanzania. Azimio la Arusha ndio tatizo? Mungu ametuumba na kutupa akili na utashi. Tutumie zawadi hii wasiokuwa nayo wanyama na hayawani tuachae kulalamikia Aziimio lisilikuwepo
 
Nimezisoma hizi nyaraka mbili nikagundua Mwalimu alifaa zaidi kuwa mtumishi wa mungu kuliko kuwa mwanasiasa. Kwa kweli jmaa alikuwa amezama sana kwenye kuheshimu UTU wa mtu.

Na kwa kuwa UTU wa Mtu sio fashion ya magari, mavazi nk vinavyochuja na kupitWa na wakati .... !! THEN AZIMIO LA UTU WA MTU ... halichuji wala kupitwa na wakati! Ni ulimbukeni kufikiri UTU hupitwa na wakati kama Azimio la zanzibar lilivyodhani na kupitishwa!

Kula Tano kuhusu Utu nini ...Then Gundua Upuuzi wa Azimio la Zanzibar NA UTAMBUE MTU ALIYEUTUPA UTU WAKE KAMA ANA MAANA YEYOTE ...Alafu pata hamu ya AZIMIO JIPYA ...

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-lugha/192708-nini-hasa-maana-ya-utu.html
 
Na kwa kuwa UTU wa Mtu sio fashion ya magari, mavazi nk vinavyochuja na kupitWa na wakati .... !! THEN AZIMIO LA UTU WA MTU ... halichuji wala kupitwa na wakati! Ni ulimbukeni kufikiri UTU hupitwa na wakati kama Azimio la zanzibar lilivyodhani na kupitishwa!

Kula Tano kuhusu Utu nini ...Then Gundua Upuuzi wa Azimio la Zanzibar NA UTAMBUE MTU ALIYEUTUPA UTU WAKE KAMA ANA MAANA YEYOTE ...Alafu pata hamu ya AZIMIO JIPYA ...

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-lugha/192708-nini-hasa-maana-ya-utu.html
kwa nini watu wengi hawalitaki Azimio la Arusha ni kwa sababu tu wao wameambiwa kwamba "vitu" ni bora kuliko "utu" wao. Kama mtu anamiliki nyumba lakini kwa pesa alizozipata kuwa kuuza kimagendo dawa zilizotakiwa kupelekewa wajawazito, siyo tatizo. Lakini kama mtu anaishi "kifukara" kwa sababu siyo mwizi au dhulumati huyu ataonekana anaishi "kizamani" watu wetu hawana utu tena!!
 
Nimezisoma hizi nyaraka mbili nikagundua Mwalimu alifaa zaidi kuwa mtumishi wa mungu kuliko kuwa mwanasiasa. Kwa kweli jmaa alikuwa amezama sana kwenye kuheshimu UTU wa mtu.

Kuna wachambuzi waliwahi kumuita Mwalimu kuwa ni mdhanifu (idealist) - unaweza hata kusema "naive" - katika hoja yake nzima ya kusisitiza kuwa ujamaa ni "imani" kama vile kazi kubwa aliyokuwa nayo ni kuwaaminisha tu watanzania waone "utu" uliomo ndani ya ujamaa na nyenzo zake hasa Azimio la Arusha nao wataamua kuufuata/kuutekeleza kwa moyo mmoja. Kwamba binadamu ni watu wazuri tu (rational) hivyo wakieleweshwa kitu chema kama ujamaa na Azimio watavikumbatia mara moja!

Hii kwangu mimi inadhihirisha jinsi ambavyo Mwalimu hakuweza kuona umuhimu wa kujenga na kuimarisha mifumo thabiti ya uongozi na uendeshaji wa shughuli za umma; mifumo ambayo itakuwa juu ya utashi wa mtu binafsi (individual) na hivyo kuhakikisha jamii nzima inafuata misingi bora inayozingatia haki na utawala bora katika nyanja za kiuchumi, kijamii na kisiasa. Hivyo, hata uendeshaji wa utekelezaji wa siasa ya ujamaa na Azimio la Arusha uliachwa utegemee zaidi busara/utashi wake binafsi na wa wateule wake bila kujali kama wao wote ni binadamu tu wanaoweza kufikwa na chochote hapa duniani.

Aidha, naweza kusema kwa kujiamini kabisa kwamba Mwalimu alikuwa na maadili ya kiwango cha juu sana na nia ya dhati ya kuwaelekeza watu wake kwenye maisha bora. Na aliamini kabisa kwamba Azimio lilikuwa ndo muongozo muafaka wa kutimiza azma hiyo. Lakini nashindwa kuelewa kwa nini (kwa uwezo wake mkubwa wa kufikiri) hakuweza kuona kwamba wengi wa wateule wake hawakuwa na tunu alizokuwa nazo yeye? Kwamba hawakuwa "rational" kama alivyotaka kujiaminisha? Akaishia kujenga kada kubwa ya wanafiki. Hata utekelezaji tu wa Azimio ungetosha kumstua kuwa unafiki, visasi, na kukomoana kulishamiri tangia mwanzoni mwa operesheni za Azimio lenyewe. Tukija kwenye uendeshaji wa mashirika ya umma, vyama vya ushirika (baada ya makada kuingizwa), n.k. ndio hatusemi kitu.

Kwa kifupi, Mwalimu alikuwa "mtu mzuri" lakini asiye na mikakati thabiti ya uongozi endelevu (sijui kama angefaa kuwa kiongozi wa dini). Nadiriki pia kusema kwamba katika kutimiza nia yake njema kwa watanzania alitumbukia kwenye "tamaa" ya kujijengea "ukuu binafsi" (personality cult) and kuzungukwa na "yes men" huku akiwaona wakosoaji (critics) wa baadhi ya sera, mikakati na maamuzi yake kama ndio tatizo kubwa la kuharakisha maendeleo ya nchi. Hata wale waliotaka kuboresha mawazo yake nao hawakupata nafasi hiyo kirahisi.

Tutake tusitake, mfumo wa kisiasa na uongozi tulio nao leo katika uendeshaji wa sekta nzima ya umma ikijumuisha hasa serikali na chama tawala (CCM) ni "legacy" ya Mwalimu ya kutokazania kujenga mifumo thabiti ya uongozi na uendeshaji wa nchi na badala yake kuacha yote yategemee utashi wa watu binafsi (individuals). Na kwa bahati mbaya sana, watu kama yeye ama hawapo au hawapati nafasi kabisa katika dunia halisi tuliyomo. Hiyo ndiyo sababu ya kufa na kutupiliwa mbali kwa Azimio la Arusha na kuanguka kwa jamii yetu kiuchumi na kijamii.
 
kwa nini watu wengi hawalitaki Azimio la Arusha ni kwa sababu tu wao wameambiwa kwamba "vitu" ni bora kuliko "utu" wao. Kama mtu anamiliki nyumba lakini kwa pesa alizozipata kuwa kuuza kimagendo dawa zilizotakiwa kupelekewa wajawazito, siyo tatizo. Lakini kama mtu anaishi "kifukara" kwa sababu siyo mwizi au dhulumati huyu ataonekana anaishi "kizamani" watu wetu hawana utu tena!!


Hapa ndipo tunagusa swala muhimu sana kama tukichagua kutokuwa vipofu!

Swali!

Ni Nani yuko tayari kudhalilisha Utu wake HADHARANI ili kuupta Utajiri au Nafasi ya Uongozi?

Wapo!!!

Ni nani yuko tayari kuudhalilisha Utu wake kwa KUJIFICHA na Kuupta Utajiri na Nafasi kubwa Ya Uongozi?

Wapo!!!!

Ni nani hayuko tayari kabisa kabisa kuusaliti UTU NA HESHIMA YAKE YA KIBINAADAMU ili kuupata Utajiri na hata Uongozi ?

Kama Wapo ni wachache sana siku hizi!!

Hapa nafungua Mjadala wa kweli kuwa Maendeleo ni nini bila UTU?

Hivi kukuua kwa uchumi na utajiri wa mali na vitu mbalimbali Kwa KUSALITI UTU WA MTU, HAYO NI MAENDELEO?.

Yaani kama mwan Dada anaweza kumaua kuuza mwili ili kuendesha gari zuri mjini kama wenzie hayo ni maendeleo..: ? Na HESHIMA NA UTU VITAKUWA WAPI ?

Kama vijana wetu wanakutakubaliana na ndoa za jinsia moja na kulipwa mammilioni ya shilingi ...na kujijengea majumba makubwa na magari ya kifahari hayo ni maendeleo? Taifa haliwezi kufikishwa hapo?

Kama mtu atakubaliana na yote hayo ili kuupta Uongozi ..ni maendeleo hayo?

Maendeleo ni nini Bila mendeleo ya UTU kwa wakiti huo huo?

HIVI Kweli kama Taifa hatuhitaji wote KUAZIMIA kwa pamoja kuufuata UTU NA USAWA katika maendeleo yetu?

Kwani Azimio la Arusha halikuwa kwa sababu hiyo?
 
Tunapozungumzia Utajiri na Tajiri, ni lazima tuangalie watu na mazingira na si kujipima kwa kuangalia sehemu nyingine za dunia.

Mfano, hatuwezi kumfananisha Mzee Kyauka wa pale Moshi mjini mwenye vi-Guest vyake na watu kama Hilton.

Ni lazima tuangalie ni mazingira gani tuliyonayo na ni uchumi wa namna gani tulionao, tunapozungumzia Utajiri na Tajiri.

Maasai, Mkurya na Mbarabaig, utajiri wao tunadai ni ng'ombe, lakini tumeshatoa tathmini kuwa ni ng'ombe wangapi? Ikiwa Maasai ana ng;ombe 100, halafu Mbena ana ng'ombe 20, lakini Mbena anazalisha na kujipatia zaidi ya Mmasai, kutokana na mbinu bora za ufugaji, je tutawezaje kuwapima hata na kuwatofautisha?

Je tutadai Mmbena ni masikini kwa kuwa ana ng'ombe wachache au tutadai yeye ni tajiri kwa kuwa kajizalishia kwa ziada kwa ng'ombe wachache?

Je ni yupi kati ya Mmbena na Mmasaai tutamuona yu karibu yetu?
Dhana za kuhusu utajiri zinatofautiana base on the society etc.

Kwasasa dhana yetu ya utajiri ni ile ya kibepari...yani mali nyingi, investments, phat bank account etc.

Mmasai hata awe na ng'ombe milioni hilo peke yake kwenye dunia yenye kutukuza dhana ya utajiri ya kibepari halina maana wala mantiki

Halitakuwa na maana yoyote kama ng'ombe hao hawana thamani ya dunia ya kibepari, na kama mmasai huyo hatauza nyama wala maziwa ili kuongeza pato, basi hao ng'ombe peke yake mean nothing.

Kwa culture ya wamasai, ambapo posa hutolewa kwa njia ya vitu kama ng'ombe, basi ule uwezo wa kutoa mahari ya ng'ombe wengi, ni dalili na imani kwamba mke huyo utamtake care vyema kwasababu una "utajiri" ama kwa mujibu wa jamii usika; mali za kutosha.
 
Back
Top Bottom