Udhaifu wa Azimio la Arusha na Mapokeo Potofu kuhusu Utajiri na Vipato | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Udhaifu wa Azimio la Arusha na Mapokeo Potofu kuhusu Utajiri na Vipato

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rev. Kishoka, Dec 21, 2009.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Dec 21, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Kwenye Biblia katika kitabu cha Mwanzo, baada ya mwanadamu kuasi, alipewa hukumu iliyosema kwa jasho lako utaishi. ukiendelea kuisoma Biblia, kuna mpambanu mwing wa kuhusu ajira, ujira na hata wenye mali na wasio na mali, tajiri na masikini.

  Katika agano jipya, kuna mfano wa waliopewa Talanta na wale waliozizalisha marudufu, walipewa motisha na yule aliyeilazia damu na kurudisha kile kile, akanyang'anywa alichokuwa nacho. Ama kuna hadithi ya wale walikwenda kazini asubuhi, na yule wa jioni lakini wakalipwa ujira ule ule. Zaidi kuna kauli inayosema mwenye nacho ataongezewa na asiyekuwa nacho atanyang'anywa.

  Hata hivyo Biblia hii hii, inatoa utata pale inapozungumzia kuwa ni heri ya Ngamia kupita tundu la sindano kuliko tajiri kuingia mbinguni. Ama kuna ilee hadithi ya yule tajiri ambaye baada ya kujidundulizia aliamua kunywa mvinyo na kushereheka matunda ya kazi yake na kusema moyo wake upumzike na Israeli akauchukua uhai wake.

  Sisi kama Taifa, mwaka 1967 tulilipokea Azimio la Arusha ambalo katika msisitizo wake, kuna lile linalosema kuwa binadamu wote sawa na linalosema kuwa lazima kuwe na uwiano wa kimapato.

  Napenda nijengee hoja yangu kwa sisi kutathmini sehemu hii ya Azimio kama kipimio cha upotofu na udhaifu wa Azimio ambao ndio umezaa na kuendeleza Umasikini wa kipato na juhudi na maarifa kutokana na mapokeo hasi yaliyofanywa na jamii.

  Aidha katika kufanya hivi, nafikiri Mwalimu Nyerere alilipuuzia lile ambalo Mkandara hulisema la Watu na Mazingira kwa mantiki ya kusema Mwalimu hakuwaelewa wafuasi wake na wananchi wa Tanzania iki kuhakikisha kuwa Azimio halikuleta utata au kujenga udhaifu wa kimapato na ufanisi katika ubunifu wa kazi na uzalishaji mali.

  Kifupi ni kwamba pamoja na kwamba Azimio lilisema tunataka kujenga jamii na nchi yenye kujitegemea, matendo ya kiserikali na chama tawala yaliifanya Tanzania iwe nchi tegemezi na ndio mana mpaka leo hii imekuwa ni vigumu kwa Tanzania kujinasua kutoka Umasikini au Utegemezi na hasa kuwa na juhudi za kujikwamua kibinafsi na kwa ubunifu katika kuleta maendeleo ya uzalishaji mali na hivyo kuongezeka kwa kipato cha Mtanzania.

  Nimeanza kwa kuleta mifano ya Biblia kwa kuwa ndani ya Biblia na Ukristo, tunaonyeshwa utata ambao upande mmoja unalaani vitendo vya matajiri, lakini kauli hizo zinapokelewa kama ni kulaani utajiri.

  Azimio nalo lililaani si Matajiri pekee, bali hata Utajiri na kuufanya Utajiri kuwa ni Ufedhuli, Unyang'au na Unyama kwa kudai kuwa Utajiri ni sehemu ya Ubepari.

  Nimemsoma Prof. Shivji hivi karibuni akitoa mada kuhusiana na Mwalimu Nyerere, napo nikaona tena yale yale maneno ya kulaani Utajiri na Uliberali kwa kuufanya ni sumu.

  Sasa katika mfumo wowote kuna pande mbili, kwa madhumuni makubwa ya hoja yangu, palipo na Umasikini, lazima pawe na Utajiri. hivyo katika jamii, ni lazima kuwe na pande zote mbili za Matajiri na Masikini.

  Lakini sisi tunadai hilo si sahihi, ni lazima tuwe na jamii ya kati ambayo si Tajiri sana wala Masikini sana ili kujenga jamii yenye nguvu na kujitegemea.

  Hata hivyo Azimio katika sehemu hii ninayonukuu hapa chini, ni wazi lilikatisha ule mwendo na mwenendo wa Watanzania kuwa Wabunifu kwa kushuhudia Utajiri kuwa ni sumu badala ya kushuhudia vitendo dhalilishwaji kuwa ni uovu.

  Kama Azimio lisingepiga vita Utajiri na badala yake likajijenga kwa kupiga vita vitendo vya kidhalimu na udhulumu, leo hii tungekuwa tumepiga hatua ya kuondokana na Umasikini.

  Ilikuwa ni makosa kwa Azimio kutoa tamko ambalo lilidumaza maendeleo ya viwanda na ustawi wa Watu binafsi kama Wazalishaji huru kwa kutamka kuwa kuhodhi mali au kujizalishia kwa ziada ni sumu na si sahihi katika mfumo wa Kijamaa.

  Azimio lilizungumzia pato la haki, lakini pato la haki kutokana na kazi bado halijaweza kupatikana kwa Mtanzania kutokana na Serikali na Chama kuingilia kati mfumo wa Uzalishaji mali kwa kisingizio cha kujenga Ujamaa, bila kutafakari kuwa Serikali haiwezi kuwa mzalishaji mali, mtunga sheria, mdhibiti sheria na mkusanyaji wa mapato.

  Ama pale Azimio lilipotoa kauli la kudai hakuna tabaka la Wafanyakazi na Wanaofanyiwa kazi (waajiri), kauli hiyo ilipokelewa kinyume na Watanzania na ndio maana hata leo hii, pamoja na Tanzania kujitahidi kuingia katika mfumo wa Uchumi huria au wa Kibepari, bado kuna msuguano wa kifikra wa kuona wanaoajiri wafanyakazi hasa katika sekta binafsi kuwa ni wahujumu na ni mabepari ambao ni sumu tuliyoitolea ushuhuda kwenye Azimio la Arusha na azma yetu ya kujenga jamii ya kijamaa na kujitegemea.

  Kingine kibaya zaidi ni kile cha kuondoa ushindani katika sekta za uzalilshaji mali kwa kuhakikisha kuwa kila kitu kinadhibitiwa na Serikali badala ya kuhakikisha kuwa sheria na Kanuni ambazo zingemlinda kila mtu, kuanzia mtumia bidhaa, mzalishaji wa idhaa, mwajiriwa na mwajiri vinakuwa bayana na haki inatumika katika kuhakikisha hakuna uonevu na dhuluma.

  Basi ni vema tukalirudia Azimio kwa kunyoosha udhaifu na mapokeo potofu ambayo yametudumaza si kifikra tuu bali hata kwa vitendo na kutufikisha hapa tulipo.
  FULL VERSION ya Azimio - https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=44703&d=1325749444
   
 2. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #2
  Dec 21, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Rev Kishoka:

  Spot on, spot on. Azimio la Arusha lina kama sehemu nne au tano. Mpaka sasa vipenzi wa Azimio hilo wanaangali maadili ya viongozi ambayo kwa ujumla ni sehemu moja tu ya Azimio lenyewe.

  Sehemu zingine za Azimio hilo zinazohusu maendeleo ya uchumi na umilikaji wa uchumi huo ni disaster.
   
 3. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #3
  Dec 21, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Zakumi,

  Mimi ni mmoja wa vipenzi vya Azimio la Arusha. Lakini ni wazi lazima tuchangue pale ambapo lilishindwa kutuletea maendeleo na ufanisi. Bila kukaa chini na kucham bua makosa yaliyofanyika ama kwa makusudi au bila kukusudia ni kujinyima haki ya kuwa na maendeleo na demokrasia ya kweli.

  kitendo cha Azimio la Zanzibar kufuta miiko ya maadili ya viongozi na kukumbatia Ubepari wa mamboleo (globalization na free market economy) havikuwa sahihii katika kurekebisha kasoro za Azimio la Arusha.

  Kila tulichokifanya kama kutengua Azimio la Arusha tumelifanya kinyume na hivyo kuvurunda zaidi badala ya kujirekebisha.

  Nawakaribisha wanamapinduzi Companero, Blue Ray, JMushi, Julius na Bob Mkandara waje kutetea hoja!
   
 4. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #4
  Dec 21, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Zakumi,

  La nyongeza, katika vipengele vya Azimio la Arusha nilivyo vinukuu, vinatoa hisia kuwa kila mtu ni sawa na lazima tusimame sawa na tuishi maisha yanayofanana.

  Azimio linapiga vita watu binafsi kuwa na nafasi ya kipekee (priviledge), lakini linasahau kuwa Viongozi wote wa Serikali, Taasisi zake na Wanasiasa walipewa priviledge ya namna ingine ambayo si ya mishahara, kama nyumba za kuishi, gari la usafiri, huduma za matibabu na hata zawadi (takrima) kama chakula na bidhaa za matumizi ya nyumbani kwa matumizi binafsi.
   
 5. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #5
  Dec 21, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  nadhani walioandaa hilo azimio hawakuiangalia tanzania ya miaka 30 baadae!......
   
 6. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #6
  Dec 21, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,324
  Likes Received: 1,790
  Trophy Points: 280
  .
  Naunga mkono hoja hii ya kuwa mwalimu kuna watu ambao hakupata muda kuwaelewa vizuri na kuendelea kuwapa madaraka ili hali walikuwa sio implementers wazuri wa azimio la Arusha.Pengine alikuwa deceived na unafiki wa watu ambao leo umekuwa kama ni tabia ya muhimu na ya msingi kabisa ili uweze kudumu kwa muda mrefu katika utumishi wa umma. Walichokuwa wanafikiri wafuasi wa mwalimu sio kile ambacho mwalimu alitegemea angepata kutoka kwao.
  Hata hivyo as evolving nation, mapungufu ya azimio la arusha yangetakiwa kufanya kwa namna ya uwazi na yenye kujari utaratibu. Kilichofanyika wakati wa kulipiga chini azimio la arusha ndio kumetuletea mauti makubwa zaidi ya yale mapungufu yaliyomo kwenye azimio hilo maana kama Taifa hatuna agenda inayotupa mwelekeo wa wapi tunataka kwenda.
   
 7. Companero

  Companero Platinum Member

  #7
  Dec 21, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mchungaji toka Azimio la Arusha liuliwe na kuzikwa rasmi miaka zaidi ya 20 imeshapita. Kwa tafsiri zenu za Kibiblia hii ni sawa na kipindi cha kizazi kimoja. Hivyo acheni kabisa kulilaumu Azimio la Arusha kwa Umaskini tulio nao leo. Msingi wa Azimio la Arusha mliouondoa hivyo umaskini tulio nao sasa chanzo chake ni Azimio lililopo sasa, yaani Azimio la Zanzibar ambalo liliwaingiza kwenye mfumo wa kupunguza umaskini badala ya kuondoa umaskini. Tangu lini tajiri akakusaidia kupunguza umaskini, ili iweje?

  P.S. Nashangaa sana kitu kilichodumu kwa miaka isiyozidi 25 tu (1967 -1991) kinalaumiwa kuliko kitu kinachoendelea kudumu tu (1991-2010+) na kuliko kitu kilichodumu kwa miaka zaidi ya 50 (1884-1961) kwa kutufikisha hapo tulipo kwenye kisiwa cha fikra duni, elimu bugizi na sera maskini!
   
 8. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #8
  Dec 23, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Rafiki,

  Lakini mbona unatahamaki badala ya kuingia chini kujibu? au kwa kuwa haijakaa mkao wa precise?
   
 9. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #9
  Dec 23, 2009
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Rev kishoka siku hizi hasa ninyi mnaojiita mareverend ndiyo watunza pesa za mafisadi mnafadhiliwa hata kuanzisha mabenki.

  Kumbuka ni yesu mwana wa mungu aliyesema tajiri ni vigumu kuingia ufalme wa mungu. Unaposoma biblia unatakiwa kustudy plot nzima ya maandiko, siyo kukurupuka kama unavyokurupuka.
   
 10. K

  Kleptomaniacs Member

  #10
  Dec 23, 2009
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Rev, Comapnero hajatahamaki kagonga kwenyewe! na jibu lake ni precise na huo ndio ukweli, mara nyingi tunaukimbia ukweli, ukweli unauma, pamoja na hayo myaitayo mapungufu ya AZIMIO, azimio la matumaini mie nadhani kama tunataka kurejea kwenye mzizi tuanze kwanza na suala la maadili hasa ya viongozi, kisha baada ya hapo tuangalie suala la nidhamu binafsi, kumbuka Mwanamapinduzi Walter Rodney katika tafsiri ya maendeleo katika ngazi ya mtu binafsi alisisitiza suala la nidhamu, je sisi tuna nidhamu katika yale tuyatendayo? tujitathmini mmoja mmoja picha tuipatayo ndiyo hasa picha ya Jamii nzima ya Watanzania. Wengi wetu nidhamu zetu ni za uwoga na hatujitumi hata kidogo hatuna self motivation so pamoja na kasoro na vikwanzo mbalimbali tutaendelea kupiga danadana na sera zetu za eti kupunguza umaskini! umasikini huku nidhamu binafsi hatuna. Azimio halikusema kuwa watu wasiwe wabunifu katika kujiletea maendeleo, sema tu tatizo kubwa lilikuwa katika utekelezaji na sisi hata katika mipango yetu mbalimbali issue kubwa huwa ni utekelezaji, unarudi kulekule no displine mambo hayawezi kwenda.
   
 11. K

  Kleptomaniacs Member

  #11
  Dec 23, 2009
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakosoaji wa wakosoaji wa sera za kiliberali mamboleo wanadai kuwa pamoja na ukosoaji wote huo wakosoaji wa sera za kiliberali mambo leo wameshindwa ama hawana ujuzi wa kupendekeza sera mbadala ama mikakati mbadala ya uliberali mamboleo au ubepari.

  Hii nadhani ni upotoshwaji wa hoja za wakosoaji wa uliberali mamboleo na ubepari, jamii iliyo na misingi ya usawa inawezekana na nadhani hapa kidogo kwa upande wa lugha bila shaka wanapatia wale wanaosema tumekuwa tukitumia lugha za wenzetu na kufikiri kwa lugha za wenzetu ndio maana maendeleo kwetu inakuwa ndoto! kwa mfano kwa Ki inglish kuna tofauti kati ya equity na equality! Sasa kwa mfano kama tunataka kuongelea usawa kwa maana ya equity tunaiwekaje kiswahili?

  Azimio la Arusha wakati likisisitiza kazi kuwa ndio msingi wa utu na kufanya kazi kwa ushirika kama mbinu ya kujikwamua kutoka katika lindi la umasikini kumbuka pia watu binafsi waliachiwa nafasi ya kufanya kazi katika mashamba ama miradi yao binafsi, kulikuwa na siku za kufanya kazi za ushirika ama umma na siku za kufanya kazi katika maeneo ama mashamba binafsi huo utaratibu katika baadhi ya maeneo ya nchi yetu ungalipo mpaka leo, ila tofauti yake ni kuwa wakazi hukutana tu kupiga soga ama kusikiliza kama kuna ujumbe wowote toka serikalini ama kwa viongozi wa wananchi.

  Je twaweza kurudisha wakati nyuma kidogo na kukopa baadhi ya vitu vya wakati huo na kuvileta kwenye hii 21st Century?
   
 12. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #12
  Dec 23, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Mimi nimetoa sehemu moja ya Azimio na kuichangua na kuitaja ni kitu kilicholea hali ya umasikini na woga wa watu kuwa na ziada, hata kujenga tabia ya kuwa wazalishaji wa kujikimu. Kama ningetaka kuzungumzia suala la Azimio la Zanzibar au Viongozi kujinyakulia ningeliongelea kama nilivyofanya mara elfu humu ndani.

  Lengo langu ni kumchambua Mtanzania na fikra zake na kujiuliza ikiwa tulipanda mbegu ya kusema maisha bora ni ya Umasikini au kujikimu tuu, je hatuoni kuwa tulipokelewa kwa asilimia 200 na ndio maana inakuwa vigumu kwa jamii kusonga mbele kiuchumi
   
 13. Companero

  Companero Platinum Member

  #13
  Dec 23, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mkuu lazima tuweke muktadha sawa, hatuwezi kujibu suala la uongo!
   
 14. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #14
  Dec 23, 2009
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,566
  Likes Received: 1,933
  Trophy Points: 280
  Rev Kishoka; Nilisoma maoni ya Mkapa kuhusiana na Azimio la Arusha kwenye hotuba yake ya hivi majuzi, na baada ya kusoma posting hii hasa paragraph niliyoi highlight,nimegundua kuna connection flani hivi ambayo tunaweza kuitumia kupata pa kuanzia kwenye mjadala huu.

  Viongozi wetu waligunduwa kuwa watakuwa "wagawaji" tu kwenye zoezi zima la ubinafsishaji mara litakapoanza kwasababu wao ni kama wasimamizi wa shughuli nzima. Maadili ya uongozi yaliyokuwepo kwenye Azimio la Arusha ndo ilikuwa kikwazo kikubwa kwa mafisadi hao.

  Kwenye makala yako hapo juu umetofautiana kimawazo na viongozi hao especially Mkapa kwani alisema wazi kabisa juzi kwamba maadili ya uongozi ndiyo yalipewa kipaumbele na hilo ndio lililokuwa tatizo kubwa la Azimio la Arusha, tatizo ambalo walilipatia ufumbuzi kupitia Azimio la Zanzibar...To trully let the dogs out!

  Kama kweli wangekuwa ni viongozi wenye kulitakia mema Taifa hili na wala siyo majangili, basi wangefuatila udhaifu halisi wa Azimio la Arusha na kukiacha kipengele cha maadili ya uongozi kama kilivyo kwasababu ofcourse maadili ya uongozi kutokuwepi ndiyo yametufikisha hapa tulipo, kwani ufisadi ni nini?

  Matatizo yote tuliyonayo leo hii be it ya kijamii ama kiuchumi na kisiasa yametokana na ufisadi.....

  Leo hii mtu anakuja anakwambia kuwa Azimio liliwapinga mafisadi na ndio maana lilituangusha, really Mr Mkapa? Siyo kwamba lilipinga ufisadi na nyie mafisadi ndo mmeliangusha?

  Azimio la Zanzibar si azimio la wananchi, bali ni Azimio la tabaka la viongozi lililoamua kujimilikisha njia kuu za uchumi wa Taifa ama kuziuza ama kujiuzia kwa bei chee kwa njia za rushwa kwa kutumia mwamvuli wa ubepari. (Magufuli na Mkapa ni ushahidi hapa!)

  Mwalimu aliliona hilo tatizo vilivyo na aliwabana vilivyo hao mafisadi, na jibaba Mkapa lilijificha dhamira yake!

  Hawa walikuwa ni wanafunzi wa mwalimu ambao ni wanafiki na wabinafsi, wakajijengea mazingira ya wao binafsi kunufaika,kinyume kabisa na mapenzi ya mwalimu wao....

  Hata ubepari wenyewe una maadili ya uongozi, (leadership ethics), lakini kwa maajabu ya wengi, viongozi hao wametengeneza system mbaya sana ambayo ni sumu kwa Taifa na wanachezea amani in a long run.

  Kwa hivyo basi wakati mjadala huu ukiendelea, nadhani ni vyema tukaangalia nia na madhumuni ya halisi ya mabadiliko yaliyozaa azimo la Zanzibar.

  Tukipima matokeo yake tutaweza kujuwa nini hasa nia ya mabadiliko hayo kwasababu kiukweli direction tuliyoko ni wrong...

  Ni kweli kabisa azimio la Arusha lilihitaji mabadiliko lakini ni wazi tumetofautiana na viongozi wetu kuwa ni mabadiliko yepi yalitakikana kwenye azimio hilo, kuondoa maadili ya uongozi kutoka kwenye Azimio la Arusha ni umafia!

  Ni sawa na kusema nyumba hii haifai kwasababu nimeuvunja msingi wake? Does it make any sense?

  Viongozi wangefanya mabadiliko zile sehemu ambazo zilizuia ushindani wa haki kwenye biashara kwa kuzingatia qualifications zitakazowekwa zinazozingatia maslahi ya Taifa.

  Mazingira ya incentive kama alivyosema Zakumi yawe constructed ili serikali iwe na jukumu la ku oversee, na kama ikitokea viongozi wana interests flani,basi ni muhimu waka declare ili kuondoa conflict of interests nk.

  Tafsiri ya "kumyonya mwenzio" isiwe kipingamizi cha mendeleo binafsi yanaotokana na jitihada halali chini ya mfumo halali,kipaumbele kiwe ni pale wafanyakazi kwa ujumla wanapolipwa mishahara midogo isiyostahili ambayo haitawawezesha wao kujikimu,hiyo ndiyo misingi mibaya ya ubepari ambapo kwa wenzetu wameweza kuifukia kwa kutumia system za serikali za welfare, Unemployment benefits (mambo ambayo yamo kwenye Azimio la Arusha) na institutions kama YMCA, YWCA nk....Hayo ndo yameulinda ubepari licha ya kwamba hayaendani na principle za ubepari!

  Kwa wenzetu, ayo yamesaidia kuneutralize yale machungu yanayosababishwa na mfumo wa ubepari, ie big income gaps etc....Na mfano huo ni wa nchi ya marekani.

  Lakini kwa viongozi wetu wa kiafrika, wao wanaendelea kutumia mabavu kusimamia ubepari na kujinufaisha wao moja kwa moja.

  Wanachukua different directions kwa kutoa kipaumbele kwenye ubinafsi na kujijengea tabaka lao hatari, kama nilivyosema hapo nyuma kuwa mixture yao hiyo ni very dangerous,hilo hawajalitambua na wanakuja na kauli za kuendelea kuwafanya wananchi ni "wajinga" kauli kama vile "Madini pekee hayawezi kutuletea maendeleo" na kauli kwamba "Taifa letu ni masikini" na hii ya sasa kuwa "Tatizo la Azimio la Arusha lilikuwa ni kipaumbele kwenye maadili ya viongozi" nk....

  Na kwa hivyo Mchungaji naamini mabadiliko waliyoyafanya hayakuwa na nia njema kwa maendeleo ya Taifa bali kwa manufaa yao binafsi.

  Tuanzie hapo....Tuone kiini hasa, na nia ya mabadiliko hayo kama kweli vinakidhi haja ya maendeleo ya Taifa letu, baada a hapo, then tupime kama ni combination gani itawork out for the best results...kwa kulinganisha, na kupima kwa kuweka kwenye mizani yale mabaya na mazuri ya mifumo hiyo....Ubepari, Azimio la Arusha, la Zanzibar nk.

  NB:Hata kama mawazo ya wananchi walio wengi "yamedumazwa" na mfumo huo wa ujamaa,bado unaweza kuona kuwa nia halisi ya mwalimu ilikuwa ni kufanya kinyume na yaliyotokea,ni kweli alitaka tujitoe kwenye ile mentality ya utegemezi ie misaada yenye strings attached nk....

  Lakini wanafunzi wake hawakuona kwamba hilo ni tatizo,walishajiamulia kwamba watanzania ni wajinga na wavivu wa kufikiri, so either walifanya makusudi ama hawakumwelewa mwalimu...

  Binafsi naamini walifanya makusudi na kuamua kwadanganya wananchi kwa maneno ya kisiasa kwa kuutumia "Ujinga" wa watanzania ambao mwalimu ndio aliona ulikuwa "Kikwazo kikubwa" Na kwahivyo basi binafsi bado naamini kuwa tatizo si kwa wananchi,bali tatizo ni kwa viongozi walioachana na mikakati ya kiukweli ya kuliondoa taifa letu kutoka kwenye umasikini uliokithiri....

  We need a knowledgable society first, and then the society that can utilize that knowledge under a fair and balanced system, a system that rewards innovation.
   
 15. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #15
  Dec 23, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Mimi sio mshabiki wa Azimio la Arusha kwa sababu Azimio hilo haliangalii mifumo ya maisha ya watanzania, uwezo na vipaji vyao. Azimio lilitaka kujenga nchi kwa kutumia taratibu ambazo ni kinyume na maisha ya Mtanzania au taratibu ambazo hazikuwahi kutumika. Hivyo huwezi kutumia weakness ya mtu kama ndio vehicle ya kuinua maisha.

  Azimio la Zanzibar nimelisoma na sioni kuwa ndio kiini cha matatizo yaliopo sasa.

  Matatizo ya sasa ni wizi. Lakini kutokana na kuonea aibu wezi, mmehamua kuuita wizi ufisadi.

  Kwa mfano Al Gore ana nyumba hapa Washington DC. Na alipochaguliwa kuwa Makamu wa rais ilibidi apangishe nyumba yake na kuhamia kwenye makazi ya makamu wa rais. Azimio la Arusha lingemkataza Al Gore kupangisha nyumba yake. Azimio la Zanzibar linamruhusu.

  Sio kwamba nalitetea Azimio la Zanzibar, lakini nataka kuonyesha tu kuwa matatizo yaliopo sasa hayatokani na Azimio la Zanzibar.

  Huwezi kuwafanikiwa kwenye free market bila kuwa na practitioners wa free market. Hivyo huwezi kulaumu Azimio la Zanzibar wakati mkulima wa mihogo au mahindi bado anahitaji elimu ya kuweza kulima vizuri.
   
 16. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #16
  Dec 23, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180

  Msilaumu Azimio la Zanzibar hili kuonyesha kuwa Azimio la Arusha lilifanya cha maana.

  Sio ni utekelezaji wa Azimio wa Arusha uliowaacha ndugu zako waBaragaig bila vipande vya ardhi?

  Na mifano yako ya kusema kuwa Azimio la Arusha lisilaumiwe haina maana. Maendeleo ni kama mbio za kupokezana vijiti. Hivyo mkimbiaji wa mwanzo akishindwa ku-set pace, basi atawapa matatizo hata wanaofatia.
   
 17. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #17
  Dec 23, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280

  Ingawa nakubaliana nawe kwa sehemu kubwa, nakuomba uwe makini katika kutumia mifano ya biblia itokanayo na agano la kale hasa hicho kitabu cha Genesis kwa sababu kuna mahali (Genesis 9:20–25, 10:1-32) kitakuambia kuwa "... MIAFRIKA ndivyo ilivyo!!!.
   
 18. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #18
  Dec 24, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Jamani, mantiki ya mimi kuleta mada si kuangalia maadili bali ni kujiuliza kama Azimio lilitufanya tuamini kuwa kuta Tajiri na Utajiiri ni kitu kibaya; dhambi, sumu, unyonyaji na kadhalika.

  je kutokana na hali hiyo kujaa kwenye fikra, tumeamini mpaka leo kuwa ukiwa na cha ziada ni dhambi na ni unyonyaji?

  Mwaka 2004, nilikuwa Dar, nikaenda kanisani Jumapili moja, baada ya kutoka huko, nikaenda Lumumba kuna bucha plae nyuma ya Shoperite (not sure if the place is still there). Nimeshuka kwenye gari nikiwa na tai yangu na mwenzngu kavaa suti, wananchi waliokuwa pembeni wakatukata jicho baya na kuanza kusema "ruksa hiyo, ruksa hiyo" sasa mimi nikang'amua kinachoendelea na kujiuliza, je ni dhambi mtu kuwa pasinaa ukiwa umetokea kanisani au kama unajiendea mahali? Mpaka leo hii najiuliza kilichowatuma wale mabwana waliokuwa wamekaa wakibarizi na kucheza bao na karata kututupia jicho la inda na kutuita ruksa!
   
 19. Companero

  Companero Platinum Member

  #19
  Dec 24, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mchungaji yaani wewe unaona ni sawa kuwa na cha ziada wakati wenzako hawana kwa kuwa umepata cha ziada kwa kuwanyonya? Yaani wewe uwe na nyumba inayokarabatiwa kwa bilioni moja zinazotokana na kodi zetu ila mimi nisiwe na hata kibanda halafu hiyo ziada yako tuone ni sawa tu? Wewe uniajiri kwa mshahara wa kima cha chini wakati una marupurupu kedekede yanayotokana na vijisafari vya Copenhagen na kwenye bembea za Kingston wakati mimi mlipa kodi wa Kibugumo sina hata nauli ya kwenda Mlimani City kuwaonyesha watoto wangu kielelezo cha utajiri wa kipebari?Sisi tukae tu nje ya 'Bell Jar' ya De Soto wakati ninyi mko ndani na uzao wenu mteule mnakula matunda na mema ya nchi kwa mgongo wetu na kusaza ziada mnayotupa majalalani wakati wana wetu wanakufa kwa njaa?
   
 20. Companero

  Companero Platinum Member

  #20
  Dec 24, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Zakumi kwani Wabarabaig sio ndugu zako? Au ndio chuki binafsi dhidi ya Azimio inakufanya hata usikubali kukiri 'Binadamu wote ni ndugu zangu' na 'Binadamu wote ni sawa'? Hivi wamekukusea nini ndugu zetu wafugaji?

  Nimeshasisitiza, kama alivyosisitiza muasisi wake, kuwa Azimio la Arusha halikutekelezwa. Kama lilitekelezwa basi ni kidogo kati ya 1967 na 1977. Hivyo hilo suala la Wabarabaig sio matokeo ya Azimio - ni matokeo ya sheria mbovu mlizorithi kwa wakoloni na kuziongezea makali ya kiimla na kuzitumia kule Hanang mkishirikiana na ndugu zenu kutoka Canada/CIDA!
   
Loading...