Udhaifu: Jiji laachia vibanda vya biashara kuzagaa, kurudi upya.

Ally Kombo

JF-Expert Member
Nov 11, 2010
11,429
2,645
Katika moja ya mambo ambayo ninamkubali Lowasa, ni lile la kushughulikia vibanda vya biashara (viosk) vilivyokuwa vimezagaa katika jiji la Dar haswa mjini kati. Katika kamoeni hiyo, vurugu zilitokea na mtu mmoja au wawili walipoteza maisha. Alisitisha zoezi, lakini kwa kutoa muda wahusika wajipange kuondoka. Baada ya miezi sita zoezi liliendelea kwa ufanisi mkubwa. Leo hii vibanda vinarudi kwa kasi ya hali ya juu huku watendaji wakitazama tuu ! Eti Jiji la Dar lina Mayor !? Jaribu kupita maeneo ya Mwenge uone vurugu inayozidi kupamba moto. Kwa sasa kuna vibanda vimewekwa sambamba na Kiwanda cha Shellys Pharm. na watu wa DalaDala wamegeuza ni kituo na kusabisha jam ! Waulize elimuu zao sasa (hao watendaji) utatolewa mpaka maPHd, hivi mmerogwa au ni "udhaifu" tuu !?
Nawasilisha !
 
Tatizo ni kuwa kila mtu ni mfanyabiashara bongo ... kazi hazilipi. Tunabadilishana hela hizo hizo na zinazidi kupungua thamani kila siku ingawa benki zinajifanya kuzistabilize lakini huwezi kumuuzia mtu shillingi ya Tanzania hata ukienda Zimbabwe.

We don't produce,we consume. na vibanda mpaka vya kuuza chupi za mitumba vimezagaa, kuna mtu wiki tatu zilizopita nilipokuwa huko alitaka kuniuzia maji ya upako kutoka kwa T.B Joshua kwa laki na nusu .... that was lame!!
 
Back
Top Bottom