Udhaifu app ya AzamTV Max - wahalifu wanaweza kuitumia bure

guru_observer

Senior Member
Jan 25, 2020
171
295
Ikiwa zimepita siku chache tuu tangu Azam wazindue application yao ya AzamTV Max nimeweza kubaini udhaifu uliopo kwenye application hiyo ambao unampa ruhusa mhalifu wa mtandao kupata channel hizo bure na kushare kwa watu wengine streaming links za channel hizo na kuweza kuziplay nje ya app ya AzamTV Max bila kulipia na bila limitation ya device, kwa kuwa link za channel zote zilizopo kwenye app hiyo zipo uchi (unprotected)

Mapendekezo kwa AzamTV
Suluhisho lake wanapaswa kuzuia link za channel zao zisifanye kazi nje ya server zao, naamini Azam wana IT wazuri wanaweza kufanyia kazi suala hilo

NB: nilitaka kutoa angalau link ya channel moja hapa kama evidence, lakini nimeona si hekima kufanya hivyo kwa kuwa sina umiliki wa content hizo na kwa kufanya hivyo ni uvunjifu wa sheria za nchi pia, lakini ninachoweza ni kushirikisha udhaifu uliopo ili wafanyie kazi.

Ahsanteni, natumaini watafanyia kazi suala hilo na endapo hawatafanyia kazi siku nyingine nitakuja na link moja tuu iliyopo kwenye app yao as evidence waone jinsi unavyoweza bypass na kuitumia app hiyo bure.


--------------------------------------------
UPDATES
---------------------------------------------------
Wapendwa naomba nipeni ushauri wa nini nikifanye maana hadi leo hii Azam hawajanijibu chochote licha ya kuwatumia ujumbe kwenye kurasa zao za Instagram pia niliwaandikia Official email kwa kutumia my secure email yangu ambayo haijawapa utambulisho wangu wowote (for my persona security) nikawajulisha kuhusu udhaifu huu mkubwa pamoja na kuwapa sample ya links zao za video kama uthibitisho lakini bado hawajafanyia kazi na hawajajibu chochote.

Lakini pia kuna mtu wao alinifuata PM akasema atafikisha jambo hili kwa department husika ya IT ila naona bado hakuna mrejesho wowote hadi leo.

Kwangu mimi naona hiyo ni kama dharau kubwa kwa taarifa muhimu niliyowapa, pia inanifikirisha sana kuhusu usalama wa data za wateja utakuwaje ikiwa wamepuuza (maana siamini kama hawawezi) kufuata mbinu za kiusalama kulinda contents zao wenyenye?.

Nimeambatanisha hapo pia email niliyowatumia

Sasa wadau naomba ushauri wenu mahususi na wenye hekima na busara je niziachie link hizi zizagae online ili wajifunze kupitia hili, au nikae nazo chumbani kwa matumizi binafsi, au nizitumie kutengeneza free version ya mobile app? ili siku nyingine wawe makini na wafanyie kazi taarifa wanazopewa na wasamaria wema mfano wangu? karibuni
 
guru_observer,
Umechunguza wanatumia Authentification system ipi mkuu?? Coz kuwa na link sio shida, shida ni kama server itakuruhusu kuangalia content baada ya kuverify Auth keys au tokens zako.

Kwa jinsi ulivyoelezea unamaanisha hata ukiwa na links za dstv utaangalia tu!! Lakini hio haiwezekani kwa sababu ya Auth system zinazotumika, unless ufanye compromising kwenye Auth system zao.

Ni PM hio link nichk kama kweli zinafunguka kizembe hvo.
 
Umechunguza wanatumia Authentification system ipi mkuu?? Coz kuwa na link sio shida, shida ni kama server itakuruhusu kuangalia content baada ya kuverify Auth keys au tokens zako.

Kwa jinsi ulivyoelezea unamaanisha hata ukiwa na links za dstv utaangalia tu!! Lakini hio haiwezekani kwa sababu ya Auth system zinazotumika, unless ufanye compromising kwenye Auth system zao.

Ni PM hio link nichk kama kweli zinafunguka kizembe hvo.
I mean ukiwa na link tuu unaangalia ndio maana nimesema zipo uchi mfano hii ni link ya Azam Sports 2 https://1314348974.rsc.cdn77.org/***348974/index.m3u8 (hapo kwenye *** kuna number nimezitoa, ambapo ukiiweka haa kwenye VLC unapata kutazama mubashara ) kwa mfano hapa natazama mechi ya Simba na Mwadui via VLC free, link zipo kizembe sana
 

Attachments

  • simba - mwadui.PNG
    simba - mwadui.PNG
    506 KB · Views: 29
Mkuu kwanini unasadadia mambo yasiyokuhusu!! ?? Sio poa kwani hawa azam ni ndugu zako au ni wajomba zako acha tupate raha duniani buana, wakifunga we unafaidika nini acha iwe wazi tu tuliimisi hii app siku nyingi sana mi mwenyewe nishaipakua kweny device yangu mapema tena ikiwezekana futa mara moja huu uzi kabla hawajashikitua dili

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana, tunapaswa kusadia kuifanya internet kuwa sehemu salama zaidi kwa watoa huduma wa aina yoyote pamoja na wanufaikaji wa huduma hizo, ndio maana nimeweka hapa jukwaani ili ikitokea wameona basi wafanyie kazi, pia nimewatumia sms kwenye page yao ya instagram japo hawajajibu, nimefanya hivyo japo najua hata mimi pia nitakosa kuzipata bure wakifanyia kazi ushauri huu pia siwezi kuwafuata moja kwa moja kwa kuwa nafahamu sisi waafrika tulivyo naweza jikuta nabebeshwa cybercrime wakati nimefanya kuwasaidia.
 
Back
Top Bottom