Udereva wa kujihami chukua tahadhari,chukua hatua usiseme una haki

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
21,713
35,524
UDEREVA WA KUJIHAMI

Je, unafahamu kuwa dereva wa kujihami ni kutumia akili ili
kuepusha ajali zinazozuilika? Na ili uweze kuepusha ajali unatakiwa uchukue maamuzi yafuatayo;

1. KUANGALIA (SEE)
Hapa dereva anatakiwa kuwa makini kwa kuangalia pande zote yani mbele, pembeni na nyuma ili kusoma mazingira ya barabara.

2. KUTAMBUA (IDENTIFY)
Baada ya kuangalia unaweza kubaini ni hatari au salama. Kwa mfano wewe umetambua kuwa mbele kuna watoto wa shule wapo kandokando ya barabara hivyo yakupasa utambue kuwa wanaweza kuvuka barabara bila kuangalia vizuri.

3. KUTABIRI (PREDICT)
Hapa ni baada ya kutambua kuwa ulichokiona na kukitambua kinaweza kuleta madhara au ni salama. Unatakiwa uwe mtabiri muda wote unapokuwa unaendesha gari, kwa mfano unapita maeneo yenye ukungu, vumbi au mvua hivyo tabiri kuwa hii barabara na hii mvua ama vumbi inaweza ikaniletea ajali muda wowote hivyo tumia macho mawili vizuri.

4. KUAMUA (DECIDE)
Wewe kama dereva unatakiwa kutoa maamuzi ya haraka kwani maamuzi yanapochelewa yanaweza kuleta madhara mfano kukupa kilema na muda mwingine hata kifo. Fanya maamuzi yenye busara ili kuepusha jambo baya ulilotabiri.

5. KUTEKELEZA (EXECUTE)
Tekeleza kwa kufanya maamuzi ya kiusalama. Kama umeamua kupunguza mwendo basi huna budi upunguze mwendo huo, kwani kuendelea kwenda na mwendokasi( speed) wakati mazingira hayaruhusu uwezekano wa kupata ajali ni mkubwa au mtu katanua upande wako na wewe unaona una haki basi unaweza kutekeleza hilo lililo kichwani mwako.

Ewe dereva, tumia mbinu/sifa za udereva wa kujihami ili kuhakikisha unafika salama katika safari yako.

Abiria ni haki yetu kufika salama.

COPY & PASTEView attachment 1027131
FB_IMG_1550612867394.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom