UDASA Wagomea JAKAYA Kutunukiwa PHD ya HESHIMA

nguvumali

JF-Expert Member
Sep 3, 2009
4,923
1,325
Katika kuadhimisha miaka 50 Ya Uhuru wa Tanganyika , utawala na uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam umepanga kumtunuku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete, mzaliwa wa Msoga Mkoa wa Pwani Shahada ya Uzamivu/PHD ya Heshima.

Sasa katika hali isiyotabilrika wasomi wa chuo hicho kupitia UDASA wamekua wakigomea kutunukiwa kwa huyu bwana kwa madai kuwa hastahili kupewa Heshima hiyo kwakua hakuna la maana alilolifanya kustahili Tuzo na hakika wametoa wito kwa Utawala wa chuo kujitenga na propaganda za ajabu ili tu kuupumbaza Umma kuwa anakubalika na kuheshimika sana miongoni mwa wasomi katika Tanzania hii.


(.Note..................................habari hii nimeipata pale ofisi za UDASA kwa Mkufunzi aliegoma kunitajia jina.)
 
safi sana watakua wamempunguzia mzigo wa PhD huyu mzee sorry kijana wa watu
 
  • Thanks
Reactions: Nzi
Huyo atakuwa ni Mukandara anataka kulipa fadhila kwa kupewe u vc, kama UDSM watatoa hiyo honoral PhD basi vyuo vyetu vya umma vitageuka kuwa vya makada wa vyama na si wanataaluma.

watch out UDSM, msiporomoshe hadhi yenu ambayo japo inashuka tayari,kwa hilo mtaiporomosha mno.
 
UDASA ni wasomi na wapo right kabisa. kafanya nini cha maana hadi apewe heshima hiyo? endapo mkandala aking'ang'ania apewe basi atakuwa amekishushia hadhi chuo chetu ukitilia maanani kinaheshimika afrika.
 
Utakuwa ni upuuzi kuendesha chuo kwa misingi na pressure za kisiasa. Phd ni kitu cha kusotea jamani, sio ya kugawa kama maandazi au mananasi chalinze. Ni bora waandae bonanza kwa watu wooote waliopitia ud iwe kama maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru.

Na waalike wale walioko ndani na nje ya nchi hata maraisi pia waliopitia hapo kama akina Museven wa uganda, sa si kuja kutunuku mj'@,@-¡ìga mmoja analiletea taifa anguko la uchumi,nyabafu zake mkandara.
 
makamu mkuu wa chuo Bwana Mukandara na wale wenzie wameng'ang'ana kuwa lazima mkuu atunukiwe
 
JK bwana, yuko so busy kutafuta cheap popularity! na sijui kwa nini watu bado wanajipapatikia kwake waqt wanajua kabisa kuwa hastahili kupewa fadhila yoyote! inasikitisha kwa taasis nyeti na kubwa na ya kisomi kama UDSM ku-contemplate kumpa PhD mtu kama JK. wamwachie alizokuwa nazo zinamtosha. si zimeshamfanya aitwe Dk JK, nyingine ya nini? tuache unafiki, hatujengi chochote
 
naona sasa tunakoelekea siko,tutafute maana na nani anastahili kupewa PHD ya heshima tuwasaidie hawa UDSM inaonesha wamesahau au wanalinda masrahi yao binafsi.
 
naungana na wasomi wasikubali. hii itaonyesha kuwa mko makini. kafanya nini kama vijiti vya kutoa uchafu kwenye meno/masikioni vinatoka nje ya nchi kuna nini kumefanyika hapa home.
 
Tena wasimpe huyo bwana, katika uongozi wake na katika kipindi chote cha usomaji wangu/uanafunzi wangu huyo bwana hajawahi hata kutia mguu pale. Amekuwa akieneza uvumi mbaya juu ya udsm na amekitenga ktk maendeleo, jitihada zake zipo UDOM kwake Udsm nikama kambi ya upinzani. Kifupi NAWAUNGA MKONO UDASA KWA MSIMAMO WAKE, HIYO PHD HAITAKUWA NA MAANA, NI KAMA VIONGOZI WA UDSM WANAJIPENDEKEZA!
 
naona sasa tunakoelekea siko,tutafute maana na nani anastahili kupewa PHD ya heshima tuwasaidie hawa UDSM inaonesha wamesahau au wanalinda masrahi yao binafsi.

apewe dr. wilbroad slaa (samahani jina nimeandika kwa kichagga)
 
nimesikia rais mpya wa Zambia miongoni mwa mageuzi anayofanya ni pamoja na ku-nullify baadhi ya titles zilizotolewa bila sababu za msingi. Hiyo ni pamoja na majina ya sehemu (kama barabara, viwanja, na majumba ya umma) na si ajabu akaenda mbali kutaka kufuta hata hizi honorary titles kama PhD zisizo na base inayoeleweka
JK bwana, yuko so busy kutafuta cheap popularity! na sijui kwa nini watu bado wanajipapatikia kwake waqt wanajua kabisa kuwa hastahili kupewa fadhila yoyote! inasikitisha kwa taasis nyeti na kubwa na ya kisomi kama UDSM ku-contemplate kumpa PhD mtu kama JK. wamwachie alizokuwa nazo zinamtosha. si zimeshamfanya aitwe Dk JK, nyingine ya nini? tuache unafiki, hatujengi chochote
 
Back
Top Bottom