UDASA: Tunaidai Serikali zaidi ya Bilioni 11, watulipe kabla ya Februari 28, 2019

Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDASA) imesikitishwa sana na tabia za baadhi ya Watumishi wa Serikali wanaochelewesha kwa visingizio visivyoeleweka malipo kuhusu stahiki mbalimbali za WanaUDASA

Kwa miaka 3 sasa Wanataaluma wanaostahili kulipwa posho ya nyumba ya kuishi (kwa mujibu wa standing orders for the public service 2009, section L, L.34 hadi L36 na Section M)

Kwa UDSM pekee Wanataaluma wanaidai Serikali kiasi cha za Kitanzania Bilioni 6, 272,357,696.00 ambalo ni deni la kuanzia Januari 2014 hadi Septemba 2018

Deni hili linaendelea kuongezeka kila mwezi ilhali hakuna maji ya kueleweka kutoka kwa wahusika

Wanataaluma wa UDSM wanaidai Serikali kiasi cha zaidi ya Shilingi Bilioni 5 kama malipo ya nyongeza ya mishahara (arrears). Baada ya malalamiko Juni mwaka jana WanaUDASA 102 walilipwa lakini 1060 hawakulipwa

"Zoezi hilo la ulipwaji lilikuwa na viashiria kama vya kutaka kuwaziba midomo baadhi ya wanajumuiya"

Kwa miaka mitatu Wanataaluma wanaokidhi vigezo hawapandishwi madaraja na waliopandishwa baada ya kuongeza elimu hawaongezewi mishahara

Pia kuna wana watumishi walioajiriwa 2017 hawakulip wa mishahara kwa muda wa miezi 5 na hadi sasa hawajalipwa

Hivyo UDASA tunashauri yafuatayo.

Serikali ilipe mara 1 malipo yote ifukapo Februari 2019.

Serikali ianzishe utaratibu wa kuambatanisha malipo ya posho ya nyumba kwa wanaostahili pamoja na mishahara yao

Ofisi ya Utumishi wa Umma iwapandishe mara moja Wanataaluma vyeto vipya na ianze kuwalipa mishahara inayoendana na vyeo hivyo

Kinyume na hapo Serikali itakuwa imetangaza mgogoro na Wanataaluma. Mgogoro huu utatulazinisha WanaUDASA kuondoa nguvu yetu kwenye majukumu yetu

Dkt. George Leonard Kahangwa
Mwenyekiti wa UDASA
Nani aliwatuma muache weledi na akili zenu nyumbani, mkaanza kutumika kama Condom kwaajili ya siasa za maji taka mkashindwa kutumia elimu zenu kuwasaidia wananchi masikini? pambaneni na hali zenu maana mliyataka wenyewe, virisechi vyenu uchwara vingi vikaegemea upande wa fisiemu sasa mnaisoma namba. Wasomo bogus kabisa nyinyi, haya na mafuta yanapanda tena bei na nyinyi mpo tu , taaluma zenu zinawasaidiaje watu wa chini? mmevuna mlichopanda stupid DON.
 
Back
Top Bottom