UDART: Sasa nimeelewa kwanini hamtaki kuleta kadi tena

Mtemi mpambalioto

JF-Expert Member
Aug 23, 2015
3,261
7,395
Tumekuwa tunapgwa danadana kuhusu uletaji wa kadi zingne kwa ajili ya mwendokasi

Habari kutoka insider zinasema wakileta kadi wanakosa mapato ya watu wa MBEZI kwenda mjini kwa kuwa mtu akitumia kadi analipa 800 ila asiye na kadi analipa 1,050

Huu uhuni kuna watu tena itakuwa ndani ya serikali wanafaidika na kinachofanywa!

Kwa kweli mateso ya kupanga folen kupata vikaratasi ni makubwa na wananchi wanateseka sana! sielewi DART ambao ndo serikali wanafanya kazi gani zaid ya kula hela za bure!
Majipu mengne yapo usoni sijui kwa nin yanafumbiwa macho
 
Udart washachemsha Mapema tu ktk uendeshaji wa mradi huo
Kwanza kuna hati hati ya Kupata tb kwa jinsi wanavyojaza abiria kwenye mabasi Yao

Ova
 
Labda wanafanya hivyo ili kupata pesa za kurekebisha barabara ya jangwani!
Unashangaa tangia mji wa Dar es Salaam ubuniwe karibia miaka 200 iliyopita Jangwani iliachwa maana walijua ni 'makao' ya maji ambapo wanaostahili kuishi huko ni samaki badala ya binadamu. Lakini, all over the sudden mwaka 2014 watu 'wenye akili kupitiliza' kutoka chama kimoja wakaidhinisha miradi ya umma kujengwa humu!
 
Kabla hujalaumu ni vema ujue mpk ss zimetolewa kadi ngapi na ngapi ziko Active
Zimetolewa kadi laki mbili tu, swala la kadi kutokuwa active ni issue ya kadi kuharibika, kupotea au mwenyekadi kutokuwepo, sio sababu kabisa ya kutokuleta kadi mpya kwasababu kila uliponunua kadi ulikatwa kiasi cha pesa ambacho ni gharama ya itengenezaji kadi. Hakuna sababu ya msingi kwa kushindwa kuleta kadi mwaka mzima.
 
Huu usafiri ni jipu mno.. mnakandamizana kwenye basi utadhani viazi vinavyotolewa mbeya kuletwa mjini.. na kila kituo lazma wasimame hata kama gazi ziko full, wanashisha, wanapakia.. mnakaa kituoni nusu saa hadi 45 minutes gari haifiki na hakuna maelezo...kuna namba za customer service zao pale wameweka ukipiga hupati au haipokelewi.. Kuliko kutoka mbezi kuja morocco ambayo inabidi kulipa 1050 pamoja na kero zote hizo bora upitie Goba uje kawe, then kawe morocco na hapo unakuwa umelipa 900
 
Kwa nini wasiweke machine za kukatia ticket .Machine sinazoallow kupata kadi yako ,una recharge mwenyewe kwa kutumia mitandao ya simu kama Mpesa ,airtel money nk ,bank card au cash.Kila safari iwe na price yake kadi ziwe na chip inayoweza pia kufungua ile milango au visehemu vya kuingilia ili upande mwendokasi.Yaani Tanzania tumeshindwa kweli kufikiria!We need to invest more in system ila tuko busy tunapambana na watu
 
Kwa nini wasiweke machine za kukatia ticket .Machine sinazoallow kupata kadi yako ,una recharge mwenyewe kwa kutumia mitandao ya simu kama Mpesa ,airtel money nk ,bank card au cash.Kila safari iwe na price yake kadi ziwe na chip inayoweza pia kufungua ile milango au visehemu vya kuingilia ili upande mwendokasi.Yaani Tanzania tumeshindwa kweli kufikiria!We need to invest more in system ila tuko busy tunapambana na watu
mitambo yenyewe wameleta used! karatas mpaka kulenga sana ndo inakubali kwenye barcode reader
 
Najiuliza sipati jibu,magari ya kawaida wameamuru walimu wapande bure wakati wenzao wanapeleka hesabu,lkn kwnye mabasi yao walimu wanalipa,wakati wao ndo ilibidi wawasafirishe walimu bure
 
ndio maana mashirkika ya umma yanakufa..waliopewa majukumu hawataki kusikiliza wanajiamuali kama Mungu watu
 
Back
Top Bottom