UDART: kadi za kieletroniki kuanzwa kuuzwa kesho kwenye kwa Tsh 5000

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,829
43,276
Wana jamvi wasalaam!
Ule usumbufu wanao pata wana Dares- salaam kupanga foleni ili kukata tiketi kwajili ya mabasi yaendayo haraka sasa utakuwa historia baada ya kampuni ya UDART kutangaza kumalizika kwa utengenezaji wa kadi za kieletroniki zitakazo tumika kufanya malipo kwaajili ya usafiri huo!

Kadi hizo zitaanzwa kuuzwa kesho kwenye vituo vya mabasi yaendayo haraka kwa Tsh 5000!
uploadfromtaptalk1466349755940.png
uploadfromtaptalk1466349766716.png
 
Utaratibu wa sasa wa kununua tiketi kwa shilingi 650 utaendelea kuwepo, kwa kuwa siyo kila mkazi wa jiji la Dar ana uwezo wa kununua kadi hizo kwa shilingi 5,000
 
Kadi utatumia kutokana na matumizi yako kma uko na safari nyingi tegemea kutumia kwa siku chache
 
Tutabeba kadi ngapi? Mara kadi ya hosptl mara kadi ya supermarket. Mi sielewi. Kwann isiwe kadi moja itumike kwenye miamala yote.
 
kadi inauzwa 500, hyo 4500 utaitumia kwa root 8 tofauti kama sikosei, ila changamoto cjajua kwa wanafunzi itakuwaje maana yenyewe inatoa kwa kuswap... may b aje mtu mwenye ufaham zaid

Kama sijakosea wenzetu waliotutangulia kwenye teknolojia hii ya usafiri wa haraka wametenga madaraja 2 tuu kwa hizi credit card zitachaji bei ya kawaida bila kujali wewe ni mwanafunzi, mstaafu au mfanyakazi. Ticket zinazoendelea kuuzia ndo zitauzwa bei nusu kwa mtoto wa chini ya miaka 14 hadi miaka 6. Na mtoto wa miaka 5 hadi 0 ndo atapita bure akiwa na mwezi au mzazi wake.
Sijui Dart wamejipangaje.
 
Back
Top Bottom