UDART ichunguzwe kujua uhalisia kwanini wafanyakazi hawalipwi mishahara

ukawa2020

JF-Expert Member
Apr 1, 2016
332
1,000
Baada yq kushuhudia namna watu wanaotumia magari ya mwendokasi wanavyopata shida ya usafiri hadi kupelekea watu kuumia, kupoteza viatu vyao na msongamano mkubwa pindi waendapo na warudipo makazini, nikaamuamua kufanya uchunguzi kidogo kujua chanzo cha haya mambo ni nini

1. Hadi Leo tarehe 9.2.2019 wafanyakazi wa Mradi wa Mwendokasi (UDART) Hawajalipwa mishahara kwa miezi 4 Mfululizo tangu mwaka Jana mwezi wa 11.

Kwanini hawajalipwa na sababu wanazojitetea nazo ni zipi?

1. Mkopo wa NMB,ambao wanaulipa kila mwezi Tsh. Mil 50. ( 50,000,000/-)!!! Hili jambo linatakiwa kuchungwa na kubainika kinaga ubaga kama pesa wanayoitaja inauhalisia.. Taarifa za wafanyakazi za chinichini zinadai kwa mwezi UDART wanalipa NMB mil 35

2. Service za Magari, UDART wanadai eti kila siku wanatumia mil 40 za kitanzania kwa ajili ya Service. Uchunguzi wangu umebaini kuwa sio kweli katika hili wanalolisema.

Kuhusu mishahara: wafanyakazi wa UDART wamegawanyika katika maeneo matatu

1. Maboss, wao mishahara yao inakadiliwa kufika mil 100 kwa mwezi (100,000,000). Ambapo mishahara ya ni kati ya Mil 2.5 hadi Mil 3

2. Madereva, hawa Madereva mishahara yao kwa mwezi inakadiliwa kuwa mil 80 ( 86,000,000). Ambapo kila dereva analipwa laki 8 kwa mwezi ( 800,000)

3. Wafanyakazi wengine hawa wafanyakazi inakadiliwa mishahara yao kwa mwezi ni takribani mil 54 ( 54,000,000), Ambapo kila mfanyakazi analipwa kadi ya laki 590,000 hadi 700,000

Je UDART Wanakusanya kiasi gani kwa Mwezi?

Kwa sasa UDART Kila siku wanakusanya Kiqsi kisichopungua Tsh mil 100 (100,000,000). Ambapo katika makusanyo ya siku, kwa mwezi UDART wanakusanya kiasi kisichopungua Bil 3.

Je, katika takwimu hizo na zinginezo Hamna uwezo wa kuwalipa wafanyakazi? Sasa ni wakati wa UDART kuchunguzwa ili ukweli ujulikane na watumiaji wa Magari ya mwendokasi waondokane na kadhia wanazokutana Nazo kila siku

Mwendokasi umegeuka kuwa shida badala ya furaha kwa watanzania.

Na, REMIGIUS SELESTINESent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom